BUBERWA D.
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 2,293
- 1,170
Haya mambo si ya kila mtu kuelewa; bali wachache wataelewa. Iwe press conference ya polisi au mtu awaye yote, inakuwa sio kesi mpaka imesajiliwa katika masjala ya mahakama. Na kesi hainaga press conference. Ndo maana nakueleza kesi ni iliyosajiliwa mahakamani hizi nyingine ni kesi zenu za twitter,fb, jf, insta, n.kKumbwe ile kwamba alikamatwa na Immigration ilikuwa ya twitter, so spokesperson aliyeitisha press conference naye ni polisi wa twitter pia, so that implies na system yote ya utawala ni ya twitter pia which concludes kuwa hata "kesi iliyosajiliwa na mahakama" ni ya twitter pia kama "zile zetu za twitter".
Hahaha asante best, ila kuna watu humu wanashabikia, wakipata breaking news kwamba Pascal Mayalla kauwawa, hao hao watakuja kusikitika humu.
Huu sio utani mzuri kabisa, mwenzenu kazi zake zinategemea public, kumu acuse kiasi hiki lazima uwe na,solid evidence, na sio vitu vya kufikirika.
Tupingane kwa hoja lakini hili linaweza kumuharibia mahusiano na watu, wakati kazi yake inategemea mahusiano na watu.
Nchi za wenzetu hili linaweza kumfunga mleta mada, kumsababishia Pascal Mayalla msongo wa mawazo, na psychological effects. Madhira ya hili yanaweza kupelekea mtu kujiua, kwasababu reputation yake kwa jamii imevurugwa. Tusishabikie haya kama hatuna uhakika nayo.
Sio poa mkuu! Usimjengee chuki mwenzako. Ina maana unataka watu wabadili utambulisho wao humu kila siku kukwepa likes za Mayalla? Acha hizo bhana....Ukiona Pascal kale comment kwako basi uwe makini sana ikiwezekana change ip zako the guy is so fukin dangerous Men.
Wewe umeamua kumshambulia PASCAL MAYALA. Lakini pascal yeye hakumshambulia Eric , alijenga hoja na ikajengeka: mwache eric apate haki yake mahakamani na uache kumjengea chuki pascalJe, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?
Hawa jamaa wafia PAKA ndiyo zao. Waache wabwabwaje ila dawa imeshawaingiaHuu ni upuuzi na nimeshindwa kusoma kwa sababu unachanganya r na l,
👍!Tumwelewe Pasco,
Haandiki hapa kuitetea Serikali bali kutupa Habari. Someni vizuri maandiko ya Paskali, someni katikati ya mstari. Pasco hawezi mchoma Kabendera kamwe. Pasco alikuwa anataka tusome magazeti bila kuonekana anayaunga mkono. Ni falsafa
Hahaha mimi simtetei, wabongo tulivyo wanafiki chochote kinawezekana, ila natoa tahadhari msije mkawa mnamzushia tu bila uhakika.
Niliwahi kumshauri Mungu next generation angeumba watu wasio na matumbo ili njaa isiwasumbue.
Typing errors nijambo la kawaida tu otherwise hukuelewa kilichozungumziwa.
Kama hujasoma ulijuaje kwamba amechanganya R naL?
andika uzi wako tuone utakaa aje,huwezi elewa kilichoadikwa sababu ya uelewa wako mdogo
Kwahiyo sikweli kwamba jamaa yenu anateka nakuua watu
Usome hivo hivo.
Unafki ni janga kubwa kama umeshindwa kusoma ulijuaje kama zimechanganywa R na l
Kwahiyo mkosoaji hakutakiwa kukosolewa? Hizi akili gani? Mayalla alitumia utashi wake kukosoa Magu na huyo Bendera. Na wewe leo unatumia utashi wako kumkosoa Mayalla na Magu. Lakini Kibendera asipingwe? Kila mtu apambane na hali yake, kwani hakujua ana wanaomtegemea wakati anafanya maamuzi aliyokuwa anafanya?Niombe wasomaji wangu muelewe kuwa sina nia mbaya ninapojaribu kuja na uchambuzi wa namna hii. Lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale taaluma moja ambayo Taifa linawategemea wanaposigana katika jamii nani anayeumia zaidi!
Nakumbuka siku za hivi karibuni gazeti la the Economist lilikuja na habari ambazo Mkuu Pascal aliziita kuwa ni habari za uongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.
Gazeti ilo liliwahi kuja na habari kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewa"
Gazeti ilo baada ya kuchapishwa Pascal Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habari ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.
Alikwenda mbali zaidi akamnukuu Rais wetu kuwa aliwahi kuwaambia wanahabari kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha na kwa hoja.
Pascal Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye Pascal Mayalla ni moja ya wanahabari ambao waliwahi kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.
HOJA.
Kwanza lazma watu mjue kuwa andiko la Pascal kupinga habari ya the Economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufuatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?
Hapa naomba nieleweke,hata watumishi idara nyeti walianza kufatilia gazeti ilo baada ya kusoma bandiko la Pascal Mayalla hapa JF, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habari zile na nyeti kupitia gazeti lile ni ndugu yetu Erick Kabendera.
Kwanini walifuatilia,kiukweli kilichoandikwa na mwandishi huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100%ingawa huyu Ndugu Mayalla alikipinga kwa lengo la kujipendekeza kwa msukuma mwemzake.
Je, Pascal Mayalla alijua tangu awali kuwa Kabendera ndie anayeandika habari nyeti na kuziripoti The Economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?
Kimsingi kifungo cha Kabendera nadhani ni furaha kwa Mayalla kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabisa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.
Je, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?
Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu Kabendera awekwe korokoloni hajawahi jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndio kwanza anatafuta makala zote zilizoandikwa huko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.
Andiko la Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa JF linaudhi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.
Nasisitiza waandishi wa habari mtengeni Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabila na wanaoshindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuhofia uhai wao.
Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Kabendera. Tusipomdai kwa kiswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozuia kiongozi yeyote kuingia mkoa wa Kagera mpaka "omwana weitu mumutaishure.""