Pascal Mayalla: NEC ni Tume huru ya uchaguzi kama lilivyo bunge na mahakama kwa sababu vyote hivi msingi wake ni Rais

Mleta uzi ina maana unasubiri mpaka tume itoe ufafanuzi ndio ujue kuwa sio huru? Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu anajua tume hii sio huru, haya yanayotokea ni kusaidia wale wazito wa kuamini kuwa tume sio huru.
Mkuu tindo, kuona ni kuamini, unaweza kuangalia hiyo program na kuona jinsi uchaguzi unavyoendeshwa, na NEC japo sio Shirikishi lakini ni Tume Huru!. Kitu ambacho ni ukweli wa wazi, hakuna uchaguzi wowote very smooth, hata wa Marekani, dosari ndogo ndogo ni kitu cha kawaida, lakini dosari hizo, sio za kuathiri matokeo ya jumla ya uchaguzi. Tuambizane tuu ukweli, Tanzania kuna upinzani wowote wa maana wa kushindanisha na CCM?. Kwa track record ya JPM, kuna mtu wa kushindana nae akamshinda?.

P.
 
Kwa kifupi kwny matukio makubwa kama uchaguzi popote duniani huwa kunatokea changamoto ndogo ndogo.
 
Huyu njaa hana lolote mpuuzi
 
Sasa kama ana record nzuri mbona hataki tume huru wala katiba mpya? acheni drama za kipuuzi watu wanatekwa na kuuliwa wewe unashangilia, umaskini isiwe chanzo cha kukosa akili huku tukitafuta teuzi za kijinga.
 
Huyo ni mwanasheria nguli wa undumilakuwili,hajawahi shida hata kesi ya mtu kaiba kuku.
Yani ccm imejaa wachumia tumbo tu
 
Kweli kabisa Both NEC and ZEC ni huru kabisa. We see as the years go by the opposition are getting worse. The percentages keep dropping in the results, so these two organizations must be doing a very good job of being free and fair. Hongera kwao.
 
Kweli kabisa Both NEC and ZEC ni huru kabisa. We see as the years go by the opposition are getting worse. The percentages keep dropping in the results, so these two organizations must be doing a very good job of being free and fair. Hongera kwao.
Nileteeni Mayalla, Nileteeni Mayallaaa, Nileteeni Mayallaaaaaaaaaaaa....
 
Mkuu wakurochi , nimedanganya wapi?.
P
P.
Tume kuwa huru ni suala Pana Sana lenye kuhitaji busara na hekima zinazoelekeza watendaji kutii na kufuata Sheria, misingi na taratibu zilizoisimika na siyo kufuata takes la mtu aliyepewa mamlaka ya kuteua Wala chama Cha siasa!
Tume Haina wajibu wa kumuondoa mgombeaji wa nafasi walizozitangaza na badala Yake wanatakiwa wawasahihishe kwenye vigezo walivyokosea ili wakakataliwe na wapigakura! Huo ndio Uhuru wa tume. Ona ilivyofanya madudu ambayo naamini hata wewe yalikuduwaza!
Nature ya mwanasheria ni kuwa muumini wa haki siku zote! Unavyojitanabaisha kuwa mwanasheria huku ukishindwa kuiishi haki Basi utakuwa famba badala ya nguli! Wawezaje kuiona time kuwa huru huku ikiwa imekanyaga na kugalagaza haki matopeni? Nimekudiss from now on!
 
Mkuu ZZK, Zitto , pokea baadhi ya nondo, zipime, mkiona zina sifa, zijumuishe katika maazimio ya kikao chenu cha TCD, leo yanayokabidhiwa Kwa kile kikosi kazi, yatue mezani Kwa Mama, ili sheria zifanyiwe mabadiliko kabla ya uchaguzi wa 2025.

NEC ni Tume huru, ifanywe tuu kuwa shirikishi.

Waliosusa waacheni wasuse, maana kama awamu ya 5, la katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM, na hatukumlazinisha JPM kubadili katiba, sasa la katiba halimo kwenye ilani ya Samia, hivyo kumshiza au kumlazimisha Samia kukamilisha mchakato wa katiba mpya ni kumuonea!. Tunaweza kubadili baadhi ya sheria kandamizi na kuvibadili baadhi ya vipengele kandamizi vya katiba iliyopo, kuwezesha uchaguzi wa 2025, kuwa ni uchaguzi huru na wa haki, halafu mchakato wa katiba mpya ukaendelea, Kwa nafasi baada ya 2025.

Paskali
 
teuzi zilimkosa hadi jamaa kaenda ahera....aendelee kubeti beti itaweza jibu
 
Ujinga

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
sasa ulisifia nini Pascal? CCM hawawezi kuachia nchi kwa uchaguzi..........nilijua na nimetoa harsh comment kwako maana kwa level yako unajua fika kuwa ccm haiwezi kuleta tume huru maana wanajua ikiwepo wanaondoka....
Tatizo la Tume yetu ya uchaguzi ni tume huru ila ilikuwa sio shirikishi!, kwenye muswada huu bado sijauona huo ushirikishi, hivyo huu ni mvinyo ule ule wa zamani ila kwenye chupa mpya!.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…