Pascal Mayalla tafadhali Jumamosi tuletee wataalamu wa sheria tujadili "Uhalali" wa ubunge wa Cecil Mwambe na Nimrod Mkono

Pascal Mayalla tafadhali Jumamosi tuletee wataalamu wa sheria tujadili "Uhalali" wa ubunge wa Cecil Mwambe na Nimrod Mkono

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Naelewa kuwa wewe Pascal na mwenzio Dotto ni members humu na mmekuwa mkilipa umuhimu wa juu hili jukwaa katika kipindi chenu cha Jicho letu ndani ya habari.
Nakumbuka hata juzi ulimuuliza waziri wa habari mh Mwakyembe juu ya misukosuko ya kimahakama anayokumbana nayo mkurugenzi wa Jf mh Max.

Nikuombe tu kama kuna uwezekano kipindi kijacho tuletee ama wanasheria wabobezi au wanasiasa /wanahabari nguli watudadavulie hii sintofahamu ya ubunge wa Cecil Mwambe na ikiwezekana hata uhalali wa mbunge Nimrod Mkono ambaye hajaonekana bungeni kwa muda mrefu sana.

Mungu awabariki sana

Maendeleo hayana vyama!
 
Mimi kama hawa waandishi wangeweza kuomba kuonana na Rais wa nchi kufanya naye mazungumzo kulieleza taifa nini sababu ya yeye kuwa nje ya makazi Rasmi kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu?
Nimejaribu kupitia na ninaendelea kufahamu kama yupo mwingine duniani amewahi kufanya hivyo na sababu ni nini ya kufanya hivyo.
Waandishi kuomba kuzungumza na Rais sio jambo baya wala la ajabu.
Ni bora waombe wetu, wakishindwa tutawaomba wa BBC International, DW au Aljazera waombe wao. Na kwa kawaida wao wakikataliwa nayo ni habari pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Trump kakimbia mkutano na waandishi... Nadhani huyo unayemsema anaweza kuwatia ndani waandishi wote watakaohudhuria mkutano...
 
Awe mwanasheria mbobezi asiyefungamana na upande wowote. Japokuwa mimi naunga mkono maamuzi ya spika. Maana kama kulikuwa hakuna formal writen statement kuwa Mwambe amejiudhuru basi spika yuko sawa.
Mwambe ndio tatizo kwa sababu amepungukiwa uadilifu.

Ndugai hana tatizo lolote na amemwambia kabisa Cecil Mwambe kama kweli amehamia CCM aandike barua ya kujiuzulu ubunge, Mwambe amesita!
 
Back
Top Bottom