Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Pascal Mayalla ni mtu makini sana. Vijana wa kileo tungelijifunza namna bwana huyu anavyoshauri bila kwa ujasiri bila hofu. Tanzania ingelikuwa mbali katika nyanja nyingi.

Mzee huyu sio mnafiki, nyeusi anaita nyeusi haijalishi kasimama mbele ya nani.

Huyu ni mtu muhimu kwa watawala kuwa nae karibu kwa ajili ya kuwashauri.

Hana uchawa, huyu angelimsaidia sana Mhe. Rais kumueleza tabia za wateule kabla Rais hajaingia aibu ya kuteuwa asubuhi na kutengua jioni.

Mzee huyu ni wakwenda nae vitani, huwa namfananisha na Kapt. George Mkuchika namna asivyochuja.
 
Nilianza kumuona miaka ile na kipindi chake cha Kitimoto.

Nikaja kukutane nae UDSM akisoma LLB na mimi nikisoma kozi ngumu kuliko zote pale chuoni, namkumbuka akinesanesa na pikipiki lake viunga ya UDSM au Mabibo Hostel nilipokuwa naishi.

Mwaka 2005 Au 2006 NIlikuwa napata lunch Hill Park, tukajikuta tuko meza moja, ila kwa vile alikuwa star sikumshobokea, Kama ilivyo desturi yangu ya kuwakaushia mastaa so hanijui, simjui.

Kwa bahati mbaya wote tulidisco chuo,Mimi nilidisco sababu ya ugumu wa masomo ila mwenzangu nasikia ilikuwa ni figisu figisu tu za prof mmoja sio sababu ya uwezo mdogo.
Baada ya kudisco nikakimbia nchi tena kwa mara ya pili. Sikuwahi kumuona tena zaidi ya kumsoma JF na mimi siangalii TV sijui yuko TV gani siku hizi.

Kupitia JF Nimekuwa nikifuatilia maandishi yake, nara kadhaa, niseme tu maandishi yake yana unabii ndani yake, orodha ni ndefu sana nikiweka hapa hapatoshi, vitu vingine huchukua miaka hata mitano kutokea, hakuna mwana JF anayemfikia kwa hilo.

Kama hana pepo wa utambuzi basi ana roho mtakatifu. Nafahamu yeye ni mkatoliki Mzuri ila afungue tu kanisa atapata wafuasi. Nafahamu pia anapenda siasa, madhabahuni pia ni sehemu sahihi ya kupiga siasa kama akina Mama Rwakatale, Kakobe, Gwajima, Pengo, Mtikila, Sheikh Ponda, Alhad Musa wote hao wanapiga siasa kwenye mimbari.

Atumie hilo pepo la utambuzi au roho mtakatifu aliyenae kuwafikia wengi.

Maana kila utawala unamsukumia kambo utadhani hana kitu kichwani na kwa umri wake sitegemei kuona akipata teuzi,

Ni ushauri tu.
Pascal Mayalla wewe ni mtabiri, mbashiri, nabii au trend reading analyst?
 
hivi kwanini kila mtu hapa bongo huwa anahusishwa na ushushushu. hamna kitu kingine cha kumfananishia mtu mpaka huo ushushushu. na huwa mnawajuaje hao mashushushu...? kama sio wenzenu...?
Habari nyeti hawezi pata mtu back,unaweza kuwa unatumiwa na system Kwa kujua au kutojua Kwa kutumia hiyo hiyo career Yako Kwa sababu maalumu
 
Toa upuuzi,Siri za Serikali ziko mtamdaoni?
Ndio...tatizo unajifungia ndani...Kuna majukwaa ukienda hizo Siri unakutana nazo au zinakufuata zenyewe. Jitahidi walau siku Moja Moja uwe unapenda kunywa maji ya kunywa pale Mamboz...chai unywe orchid, na chakula Cha mchana update pale epido. Hazitokua Siri 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom