Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Habari familia yangu ya JF,
Katika hali ya kushangaza lakini yenye ukweli mkubwa kuna kundi kubwa sana la watu wanaamini katika nguvu za giza zaidi ya wanavyoamini uwepo wa Mungu, pamoja na ukuu na uwezo wake.
Jambo la kuvutia ni kwamba, watu hawa si wageni wa ibada. Wapo wanaohudhuria makanisa na misikiti mara kwa mara, lakini ukiangalia maisha yao halisi na maamuzi wanayofanya, utaona wazi kuwa imani yao kubwa iko kwenye nguvu za giza kuliko kwenye nuru.
Katika maisha ya kila siku, tukio lolote lisilo la kawaida linapotokea hasa lenye kuvuta hisia za watu huwa rahisi sana kulihusisha na nguvu za giza. Mfano, mtu akipata mafanikio makubwa kwa muda mfupi, watu wengi hawataanza kwa kuamini juhudi, nidhamu au baraka za Mungu, bali wataanza kusema: “Huyu lazima ana mkono wa giza.”
Hali hii inaonekana pia kwa watu wenye vipaji na karama za kipekee. Mtu anapofanya jambo la “extraordinary,” badala ya kuthamini kipaji chake, watu wengi huamini kuwa mafanikio hayo yametokana na nguvu zisizoonekana. Ndiyo maana utaona baadhi ya watu wanaamini zaidi katika makundi kama Freemason kuliko wanavyoamini katika nguvu ya Mungu.
Mfano mwingine uko wazi kwa watu mashuhuri. Baada ya vifo vya watu kama Bob Marley, Michael Jackson, Tupac Shakur, The Notorious B.I.G., Kobe Bryant, na Steven Kanumba, kumekuwa na imani kubwa kutoka kwa baadhi ya watu kwamba vifo vyao havikuwa vya kawaida, bali vilihusisha nguvu za giza au njama zisizoonekana.
Si hivyo tuu, kuna idadi kubwa ya watu wanaotafuta msaada kwa waganga wa jadi au nguvu zisizoeleweka, ilhali ni waudhuriaji wakubwa wa ibada za dini. Hii inaonesha mgawanyiko mkubwa kati ya kile wanachokiamini kwa maneno na kile wanachokiamini kwa vitendo.
Mfano halisi ni pale mtu anapopata matatizo ya kifedha, kiafya au kimahusiano badala ya kutafuta suluhisho kwa njia halali au kuamini katika Mungu, hukimbilia kwa waganga au kuamini kuwa kuna mtu “kamroga.”
Swali la msingi linabaki kuwa:
Kwa nini watu wengi wana haraka ya kuamini nguvu za giza kuliko kuamini nuru?
Je, ni hofu?
Je, ni ukosefu wa maarifa?
Au ni matokeo ya jamii inayopenda sana kuhusisha kila jambo lisiloeleweka na nguvu za giza?
Ni muhimu tujiulize haya maswali, kwa sababu imani zetu zinaathiri moja kwa moja maamuzi yetu, mitazamo yetu, na hatimaye maisha yetu kwa ujumla.