Passport kutolewa ndani ya siku 3

Passport kutolewa ndani ya siku 3

Mfumo umetengenezwa kuzuia wananchi wasipate pasipoti ndio maana wanataka barua ya kazi, mwaliko, shule nk ili upewe pasipoti.

Inashangaza sana kwa kweli
Hii ni sahihi kabisa, hakuna nchi unaruhusiwa kusafiri bila kuwa na sababu za maana.
 
Mwenye uwezo wakunisaidia kupata passport ndani ya wiki naomba aje pm.
Kama una tiketi ya kwamba unasafiri kwa haraka kwa hakika utaipata ndani ya simu 1 ama 2. Huduma za migration zimeboreshwa sana. Tusipumbazwe na maneno ya kuambiwa
 
Siku CCM iktoka madarakani ,huu upumbavu wa NIDA na Pale Uhamiaji utakwisha.

Urasimu mwingi sana.

Changamoto tulizonazo ni za kihistoria. Mifumo yetu ya vital records imekuwa sloppy tangu enzi za enzi. Serikali haina kumbukumbu za majority ya Wabongo waliozaliwa karne ya ishirini. Hata kwa zile ambazo zipo, nyingi sio real-time records za matukio.

It’s very hard to positively identify citizens when no real-time records vouch for the time, place, or manner of their births. Unalazimika kutumia multiple pieces of circumstantial evidence. Unaletewa barua ya mtendaji wa kata, ambaye yeye mwenyewe hakuzaliwa eneo hilo na wala hakuwepo kipindi ambacho huyo raia anadai kuzaliwa hapo. In fact, unakuta mtu mwingine alizaliwa Kilombero, lakini amechukua barua ya mtendaji wa kata ya Manzese. How reliable is this process?

Vizazi vijavyo vitapata unafuu mkubwa, kwa sababu Serikali sasa imechukua hatua mahususi kuboresha mifumo ya vital records!
 
hivi kuna mtu anaweza kwenda nchi nyingine bila sababu ya maana?
Na uhamiaji wanataka wajue unaenda kufanya nini ili iweje?
Hii ni sahihi kabisa, hakuna nchi unaruhusiwa kusafiri bila kuwa na sababu za maana.
 
Hii ni sahihi kabisa, hakuna nchi unaruhusiwa kusafiri bila kuwa na sababu za maana.

Passport isn’t a single-use document. Kwa sababu leo una sababu ya maana (iliyokusaidia kupata passport) haina maana kuwa siku zijazo utaendelea kuwa na sababu za maana za kwenda nje ya nchi. Hapo unasemaje? Ukirudi safari yako iliyokuwezesha kupewa passport urudishe hiyo passport Uhamiaji ili uje uombe tena utakapokuwa na sababu nyingine ya maana?

Whether sababu ni ya maana au siyo ya maana Uhamiaji haiwahusu. Ni swala la ubalozi wa nchi unakokwenda. Wakiridhika watakupa viza; otherwise, wanakunyima bila kupepesa macho!
 
warabu na wahindi waliozaliwa hapa wanatabu sana uhamiaji zinaletwa mafaili za mababu zao kuangalia waliingiaje tanzania kabla ya uhuru sasa anaeomba babu au mimi mbona hamuangalii wangoni waliingiaje kutoka sauth africa ndio asili yao au wasukuma waliingiaje kutoka ethiopia
 
warabu na wahindi waliozaliwa hapa wanatabu sana uhamiaji zinaletwa mafaili za mababu zao kuangalia waliingiaje tanzania kabla ya uhuru sasa anaeomba babu au mimi mbona hamuangalii wangoni waliingiaje kutoka sauth africa ndio asili yao au wasukuma waliingiaje kutoka ethiopia
Mkuu tuwe wakweli tu, waarabu na wahindi asili yao sio Tanzania. Hawa ni kwakua sisi ni wakarimu tu ndio maana nao wanajisikia kuwa wana haki ambayo kimsingi hawana kabisa. Kwa mfano mimi nikahamia India siwezi pewa ruhusa kumiliki ardhi au kuwa na pasi ya kusafiria ya India, ila kwa hapa wanapata kila kitu. Na bado wanatudharau wazawa, labda nahisi ni kwa ukarimu wetu uliopitiliza.
 
Huwezi kukata ticket bisa pass na visa.
Hata uwe navyo uhsmiaji wana uwezo wa kukataa vyote kwani ni waamuzi wa mwisho
Kama una ticket tayar na mwaliko wa huko uendako ukienda makao makuu unaipata ndani ya wiki.
Ila Kama hauna safari ya haraka kwa kawaida unaipata ndani ya wiki 3.
 
Back
Top Bottom