Passport ya Tanzania inaweza kukupeleka nchi 72 bila kulipia Visa. Iko nafasi ya 77 duniani kati ya nchi 195

Ni jambo jema
 
Utawala wa Mama Samia, kwa vigezo vyovyote vile, ni bora mara 100 ya utawala uliopita. Anaenda vizuri japo hatujafika tunapostahili.

Jambo pekee linalomchafua ni kesi ya kumbambikia Mbowe, kesi isiyo na kichwa wala miguu. Baada ya uamuzi wa mahakama, ni vema akichukua hatua dhidi ya Siro na wenzake waliotengeneza kesi, waliowatesa makomandoo wasio na hatia, na kisha kumwua kijana wetu komandoo Lijenje.

Damu ya Lijenje inamlilia Siro na kundi lake la wauaji.

Mama Samia, fanya kila uwezalo ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwenye:

1) Demokrasia
2) Uhuru wa watu na vyombo vya habari
3) Utawala wa sheria
4) Maisha ya ustaarabu na utu
5) Ukuuaji wa uwekezaji na uchumi

Achana na zile porojo za kusema demokrasia siyo soda!!
 

katika nchi zilizoongezeka kuna nchi yyte ya bara la ulaya?
 
Zitajwe hizo nchi Kama sio 55 za Afrika+ 17 za mashariki ya Kati yani Afughanstan,Korea kaskazini,Sirya, Lebanon na Iraq
Sasa wewe huoni rahaa kuzunguka Africa nzima bila kulipia Visa? Utumwa wa kifikra ni mzigo…
 
Elimu ni muhimu sana, kwa akili hizi sioni ajabu kwa nini watu wanazungushwa wakienda kufuatilia hati ya kusafiria ilhali imetajwa ni haki kwa kila mtanzania..

Hivi hapa Rais anayesifiwa ana uhusika gani na passport hizi..??
 
Tanzania kila Siku inazidi kung'aa tu,

Hongera sana mama Samia

Najivunia kuwa Mtanzania
Wenye passport Tanzania wangap? Wakati dunia inafungua visa free Tanzania Wana complicate upatikanaji passport ili iwe ngumu kuipata!! Hizo visa free hata dunia yote wangeachia kwa upatikanaji mgumu wa passport ni hopeless tu
 
Unajisifia kuwa wa 77?

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…