Nukta5
JF-Expert Member
- Jun 7, 2014
- 1,182
- 1,288
Pastor Myamba na Mkewe Praxceda wakionyesha pete zao za ndoa
Sio muvi wala maigizo bali ukweli ni kwamba Mwigizaji machachari wa Bongo Movie anayezitendea haki scene za uchungaji, Pastor Myamba ameaga rasmi maisha ya ubachela baada ya kufunga pingu za maisha na mchumba wake wa kipindi kirefu aitwae Praxceda hapo jana.Akionekana kuwa mwenye furaha isyo na kifani, Myamba aliweza kushea baadhi ya picha za ndoa yake kwenye ukurasa wake wa Facebook ikiwemo zawadi baab kubwa ya kitita cha pesa zilizokuwa zimewekwa kwenye kitololi walizozawadiwa na wanakamati.
Mr na Mrs Myamba wakitoka nje ya kanisa baada ya tendo la kufunga ndoa kumalizika
MR & MRS Myamba wakiwa ufukweni katika picha ya pamoja na wapambe wao
Nikuite nani Pesa???? Mr & Mrs Myamba wakionyesha minoti waliozawadiwa na kamati ya harusi
Pastor Myamba na Praxceda siku ya send off
Chanzo: LaryBway Blogu