Pastor Tony: Kwenda mbinguni sio kipaumbele cha mkristo, Pesa ndio kipaumbele

Naunga mkono hoja....

Duniani ni PESAAAA .... hii ni dunia sio PARADISO jamanii, lazima tuelewe, lazima tutafautishe kati ya DUNIA na PARADISO.....

Dunia inataka PESAA ndio hivyo..... yaani imekaa hivyo.
Kwani kuna mcha Mungu hatafuti pesa?
Shida Pesa inakuja kama kipaumbele kipya cha kiroho wakati wacha Mungu wamewahi kumiliki mapesa mengi sana miaka zIdi ya 4000 iliyopita tena bila nguvu nyingi.

Mfano Ibrahim alikuwa Bilionea tena sio kwa kukomaa , alipewa huko Misri hizo mali bado huwezi kumsikia anazisisitiza zaidi ya kutumia muda mwingi kusisitiza imani na usafi na biblia inasema hata Yeye alikuwa anautazamia mji mpya na nchi mpya.
Waebrania 11:10
Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.


Tunakoelekea sio kuzuri kuna haja sasa waumini tuanze kuwafundisha na kuwaombea wachungaji.
 

Huyu hata hapigi round 3 tutazijua rangi zake zote
 
Na pia kama ishu ni mpangilio. Kitqbu cha kwanza kuandikwa sio mwanzo ni Ayubu.

Sababu ile ni dhaifu sana. Na kitabu cha ufunuo kinatabiri wanaotanguliza besa na wafanyabiashara kuna wakati utafika watazitupa na hazita kuwa na msaada wowote kwa yoyote.

Mcha Mungu kumiliki pesa ni suala la kikanuni sio motivation
 
Reactions: I M
Mithali 30:7-9
[7]Mambo haya mawili nimekuomba;
Usininyime [matatu] kabla sijafa.
[8]Uniondolee ubatili na uongo;
Usinipe umaskini wala utajiri;
Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.
[9]Nisije nikashiba nikakukana,
Nikasema, BWANA ni nani?
Wala nisiwe maskini sana nikaiba,
Na kulitaja bure jina la Mungu wangu
 
Ukweli ni kwamba tutafute pesa . Katoa ushauri tuukubali na ndio ukweli halisi huo
 
Imeandikwa kuwa moja ya ishara ya siku za mwisho ni watu kupenda pesa kuliko kumpenda Mungu.
 

Changamoto wa krito tulio wengi HATUSOMI MAANDIKO na pili HATUTAKI UKARIBU NA MUNGU. Tunatafuta ufahari zaidi

Na hii ni kutokana na saikolojia ya mwanadamu yakutaka kuonekana YEYE NI WAMUHIMU

Kwamana hiyo haya makanisa yashajua pakupigilia ni wapi.

Huwana natamanigi kuona siku ata mchungaji anasimama na kusema katika mtaa wetu huu kanisa letu lichange pesa lijenge kuwanda na ajira zote zitaanzia na waumini.
 
Leo nimekutana na dada mmoja anafanya biashara ya fedha mtandaoni.Muamala ulipokamilika zile sarafu nikasema ntazitoa sadaka kanisani akasema hazitoshi nami nikamuuliza kwani Mungu wa siku hizi anajua hela?Kifupi waumini wamekuwa watumwa wa makanisa: yaani wao ni mawakala wa kutafuta pesa na watumishi wa Mungu ni kuzipiga.
 
Japo maisha siyo kutesa Kila la ila pesa ndiyo Kila kitu...


Cc: Mahondaw
Ukimpata mungu umepata maarifa ukiwa na maarifa ata upewe hizo fedha itakuwa rahisi kuziendesha.

Kupata pesa ni elimu namba moja

Kutunza pesa ni elimu ya pili

Kukuza pesa ni elimu ya tatu.

Ukikosa haya marifa yote we basi ata tukupe buku mbili
 

Unajiandaaje mbinguni kama huna pesa
 
Unajiandaaje mbinguni kama huna pesa
Sijaona andiko lolote linalosema kielelezo cha kwenda mbinguni ni kuwa na pesa.

Pesa ni maarifa
Pesa ni Roho
Pesa ni kama umeme
Pesa ni kama maji

Pesa inamfumo.

Soma Mithali 8:18.... Ukimtafuta mungu umepata utajiri na yote.

Mungu ni nani?
Ni roho
Ni mwanzo na mwisho wa marifa yote

Yohana 4:24
Mithali 1:7

Mwombe Mungu akusaidie upate mwanga ukisoma neno lake.

Akusaidie uwenende kiroho na sio kidini.
 
Kwamba hela zitafutwe ndio Mungu atumikiwe. Mbona ni kinyume kabisa na maandiko.

Ila sio Jambo la kushangaza maana ilishaandikwa Pia kuhusu manabii wa uongo.
 
Huo ni upotoshaji.
Hapo tayari kupenda Fedha kumejaza moyo wa mtoa hayo maneno, hivyo nafasi ya Mungu inapotea.
 
Watu wengi wanatamani waishi maisha marefu wakati huohuo wanazungukwa na madeni hadi yanayaitwa kausha damu, kumbe uwezo wao wa kipata umezidiwa na kiwango cha marejesho, unamuomba Mungu uishi maisha marefu wakati huna pesa, tafuta pesa ili uweze kutimiza malengo ambayo Mungu alikuumba uyatimize vinginevyo bora ufe mapema usitaabike ama kusumbua watu wengine kwa mizinga
 
Biblia imesema tutafute kwqnza ufalme wa Mungu na hayo mengine tutazidishiwa. Pesa tunatakiwa kuzidishiwa huku tunatafuta ufalme wa Mungu sio kipaumbele. Wanatupeleka kasi sana hawa watumishi wa Bwana.
Acha aendelee kudanganya mang'ombe yake ya maziwa. Yesu alikuja kutupa habari za ufalme wa mbinguni hapa duniani, yeye sijui anaongea habari gani?!
 
Atakuwa mjenzi huru(Free mason) yuko huru kujenga hoja zake na kuzitetea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…