matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
- Thread starter
- #21
Kwani kuna mcha Mungu hatafuti pesa?Naunga mkono hoja....
Duniani ni PESAAAA .... hii ni dunia sio PARADISO jamanii, lazima tuelewe, lazima tutafautishe kati ya DUNIA na PARADISO.....
Dunia inataka PESAA ndio hivyo..... yaani imekaa hivyo.
Shida Pesa inakuja kama kipaumbele kipya cha kiroho wakati wacha Mungu wamewahi kumiliki mapesa mengi sana miaka zIdi ya 4000 iliyopita tena bila nguvu nyingi.
Mfano Ibrahim alikuwa Bilionea tena sio kwa kukomaa , alipewa huko Misri hizo mali bado huwezi kumsikia anazisisitiza zaidi ya kutumia muda mwingi kusisitiza imani na usafi na biblia inasema hata Yeye alikuwa anautazamia mji mpya na nchi mpya.
Waebrania 11:10
Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
Tunakoelekea sio kuzuri kuna haja sasa waumini tuanze kuwafundisha na kuwaombea wachungaji.