Mkuu umenena kitu kikubwa sana sema vijana sisi tuna tatizo moja ambalo limekua ni ugonjwa mkubwa sana tatizo lenyewe ni kukatishana tamaa bila kujaribu au kuangalia kuna watu wanauza vitafunwa kila siku ila hawasongi mbele. Siku moja nilifanya research ndogo sana kuhusu biashara ya mayai ya kuchemsha wanayotembeza hawa vijana mtaani.
STORY IPO HIVI.
Siku moja nilikua katika matembezi yangu nikakutana na kijana muuza mayai ya kuchemsha. Nikamsimamisha nikanunua mayai mawili kisha nikamuongezea elfu mbili ya bure kama yake. Akafurahi sana tukaanza stories mbili tatu kuhusu hii biashara akafunguka sana akanambia kuwa yeye ameajiriwa na analipwa elfu 30 kwa mwezi kama mshahara. Boss wake anampa chai asubuhi na chakula cha usiku that means mchana anajitegemea, pia kulala analala kwa boss wake na wameajiriwa vijana watano.
Kwa siku kila mmoja hupewa tray 3 za mayai ya kuchemsha ili wakatembeze ambapo yai moja ni mia 400. Kwa hesabu ya haraka haraka ni 400x90=36,000 kwa mtu mmoja. Bei ya kununulia mayai kwa tray ni 7000x3=21000. So kwa siku boss wake anaingiza kwa mtu mmoja elfu 15000 ambapo kwa watu watano jumla ni elfu 75000/day ambapo kwa mwezi ni 2,250,000. Kwa hesabu ya haraka haraka hawa vijana matumizi yao kuanzia chai ya asubuhi na chakula cha jioni hawawezi kumaliza milioni moja kwa mwezi. Hapo bado alikua analalamika kuwa boss wao anawanyanyasa sana ila wanafanya kwa kuwa hawana jinsi tu maisha yanawabana sana.
Nikajiuliza swali hili hivi nikiwachukua vijana kama hawa nikawapangia chumba nikawachukulia kama sehemu ya familia nikawapa milo mitatu kwa siku, nikawajali kwa kila hali. Wakafanya kazi yao bila mawazo huku wana uhakika wa chai asubuhi, chakula cha mchana na jioni, sehemu ya kulala na mshahara juu watashindwa kuwa waaminifu kwangu wakafanya kazi kwa furaha. Bahati mbaya yule kijana hakuwa na simu na nilimpa namba yangu nikamwambia anibeep tu kwa simu yoyote lakini mpaka leo sikufanikiwa kuwasiliana nae tena.
HITIMISHO
kila wazo linapokuja mbele yetu tusipuuze kabla ya kukaa chini na kulitazama kwa jicho la pili. Leo hii tunapinga hili la kuuza maandazi mtaani ila tukumbuke kila siku kuna maandazi yanauzwa madukani na tunanunua kila asubuhi. Asanteni sana