Pata msaada wa tatizo lolote la kompyuta hapa

Pata msaada wa tatizo lolote la kompyuta hapa

Dell N4010
mewasha lakin hali nihiyohiyo inajizima baada ya sek 5
nawewe jaribu ushauri huu kwanza ...toa adapter yaani huo waya wa chaja toa na betri isha bofya button ya kuwasha wa sekunde 30 vyote hivyo vikiwa havipo halafu weka adapter pekee yake kisha washa
 
Tatizo la pc kujizima kama imewaka vizuri na kukaa kwa muda kidogo mostly linatokana na pc kuwa overheated sasa hii hutokana na
1. pc kuwa na vumbi jingi kwenye feni na sink especially katikati ya feni na heat sink hivyo pc kushindwa kuondoa joto ndani
2. feni kutofanya kazi kabisa
3. heat sink compound kuisha wenye pc hii ni mara chache
Unaweza kufungua pc yako na kufuta vumbi lote ndani ya pc maeneo hayo kisha rudishia kama kawaida, kama feni haizungui kabisa hapo utahitaji utaalam zaidi...
kufungua pc just google how to disassemble.... hapo mbele uta-type model ya pc yako
Samahani mkuu. Je nitawezaje kuijua type model ya pc yangu? kuna sehemu yoyote niki press itanionyesha?.
 
Kompyuta yangu haipunguzi mwanga wa screen. Nabonyeza kitufe cha ku increase contrast inaongezeka namba tu
 
Samahani mkuu. Je nitawezaje kuijua type model ya pc yangu? kuna sehemu yoyote niki press itanionyesha?.
toa betri angalia hapo ilipokuwa betri utaona model au P/N namba zifuatao ndo model au washa pc, bofya start button, isha type system information halafu check model
 
Kompyuta yangu haipunguzi mwanga wa screen. Nabonyeza kitufe cha ku increase contrast inaongezeka namba tu
drivers zina-miss kwenye pc yako baada ya kubadilisha window...jaribu ku-update hiyo pc yako fully itaondoa hiyo shida lakini pia waweza ku-install driverpack kwa urahisi zaidi kama ipo
 
Habarini wakuu, nimebadirisha OS kwenye PC yangu toka win 10 kwenda Ubuntu 16.04
Shida ni kwamba sioni Disk drives zangu za NTFS
So naomba msaada

Pia nahitahi ku update drivers pia. Msaada
 
Habarini wakuu, nimebadirisha OS kwenye PC yangu toka win 10 kwenda Ubuntu 16.04
Shida ni kwamba sioni Disk drives zangu za NTFS
So naomba msaada

Pia nahitahi ku update drivers pia. Msaada
umeweka ubuntu alongside windows au uliondoa windows kabisa
 
Kutokana na uzoefu wa muda mrefu katika ufundi wa computers (software and hardware) hapa kariakoo nimeona niwasaidie wadau humu wanaosumbuliwa na matatizo ambayo pengine wana uwezo wa kuyamaliza hukohuko nyumbani kwa maelekezo kidogo lakini pia unaweza kuomba ushauri kama ulipeleka wa fundi na tatizo lako halikuisha maana wengi wanapatwa na hayo pia...majibu yangu mengi nitayatoa mida ya jioni na asubuhi sana kutokana na ubize nilionao

Karibuni
Hongera kwa msaada mkuu..
Natumai tatizo la PC yangu litapata suluhisho hapa..
Pc yangu mkuu button za keyboard hazifanyi kazi kabisa zinazofanya kazi hazizidi hata 3. tatizo ni nini mkuu..?
 
toa betri angalia hapo ilipokuwa betri utaona model au P/N namba zifuatao ndo model au washa pc, bofya start button, isha type system information halafu check model
Shukrani mkuu, nimeiona.
 
Mkuu hongera sanaa kwa hatua ulofikia ya kuon kuna umuhimu wa kutumi elimu ulonayo ya masuala ya computer kusaidia wenye matatizo.

Naomba msaada wako me natumia hp 250 g5 w10...
Nili update windows 10 baada ya hapo pc yangu imekuwa na ttzo la sound
Inaweza ikawa inaplay... Then suddenly sound inaanza kuscratch na badae inakata kabsa... Matokeo yake kama ni nyimbo inaplay bila sauti... Mpaka ni restart ndo tena inAtoa sauti...
 
Tatizo la computa yangu dell (latitude/E6400 inagoma kutumia bluetooth, na WiFi ata nikiinstall driver tofauti
NB
ata taa (indicator ) zake haziwaki,
pia inakataa kuinsataal baadhi ya program kama archcard
 
Huenda pc yako ikawa haina au ina defective Wireless/ Bluetooth card/ adopter. Maana kma icho kifaa kipo au kizima ikitakiwa ukiswitch on iyo switch basi Pilot indicator iwe on. So tafuta mtaalamu afanye troubleshooting

Na kuhusu ku install arch CAD, check requirements za Arch CAD eg. Inataka machine minimum iwe na processor yenye speed ipi? Iwe na RAM kiasi gani?? Iwe na GPU yenye Memory Kiasi gani Pia kioo kiwe na resolution ipi??? Pia Uwe ume install OS gani??? Na pia kwenye Arch CAD na AUTo CaD ni msingi kuzingatia Microsoft Dot NET Framework na unatakiwe iwe ni .NET Framework version ipi????

Ukiweza kujibu hayo maswali lazima utapata ufumbuzi kwa nn Arch CAD haiingii kwenye PC yako
Soooooo check requirements compatibility kati ya PC yako na Program yako

Regards....!
 
Tatizo la computa yangu dell (latitude/E6400 inagoma kutumia bluetooth, na WiFi ata nikiinstall driver tofauti
NB
ata taa (indicator ) zake haziwaki,
pia inakataa kuinsataal baadhi ya program kama archcard
Km upo dar. Ni-pm nikurekebishia tatizo lako.
Unatumia window gani?
 
mkuu computer yangu ina tatizo la kupenda site za porn kila niki fungua JF lazima inionyeshe dem mwenye SNURA
 
mkuu computer yangu ina tatizo la kupenda site za porn kila niki fungua JF lazima inionyeshe dem mwenye SNURA
Hayo ni matangazo yanayo pop up pindi ukiwa online. Tumia adgurd au slim jet browser hii ina ads blocker
 
TUPE NAMBA ZA SIMU, WHATSAP, EMAIL KWA MSAADA ZAIDI...WEWE NI MTU MWEMA SANA, NIMEKUSOMA.
 
Desktop ya Dell in a brink taa ya orange badala ya kijani niki switch on na monitor haiwaki kabisa.
 
Back
Top Bottom