Wanajamii ,
Kama kuna mtu anautaalamu wowote wa ufugaji wa bata kibiashara naomba anijuze.Hii ikiwa ni pamoja na soko lake na management yake kwa ujumla.Mimi ni mwajiriwa na nipo hapa Dare salaaam nipo interested sana na ufugaji.Nawasilisha.
Bata ni kama walivyo jamii nyingine ya ndege yaani poultry mfano kuku,kanga,Bata mzinga,njiwa,kwereakwerea, nk,.Mahihitaji yao yanafanana kabisa na yale ya jamii nyingine ya ndege.Chakula ambacho kuku anakula hata bata anakula. Bata wakilishwa vyakula vya kuku wa kisasa wanakua haraka na uzito wao huu mkubwa kwa muda mfupi .
Ufagaji wa bata utakuwa mzuri kama utakuwa aidha na bwawa au mto uliopitishwa shambani kwani Bata anahitaji maji kwa asilimia 90.
Magonjwa yote anayopata kuku au jamii nyingine ya ndege pia bata hupata.Lakini ugonjwa unaowasumbua zaidi ni Mafua na kipindupindu.Bata ni wastahimilivu wa kupata magonjwa lakini wakipata ugonjwa uwezo wa kustahimili kwao huwa ni mdogo sana ,mara nyingi huwa wanakufa hovyo hivyo umakini unahitajika.
Masoko ya Bata yako ya kutosha hasa kwenye mahoteli makubwa ya mijini.Wageni wengi sana wanahitaji nyama ya bata,na kutokana uzalishaji wake kuwa mdogo ndio maana unakuta bei ya bata haikamatiki.
Ukijuhusisha na ufugaji wa bata,ndani ya muda mfupi,uwezekano wa kuwa tajiri ni mkubwa sana.Hebu tazama Tanzania sijasikia kampuni yoyote inayojihusisha na utotoreshaji na uuzaji wa vifaranga wa bata.Asikudanganye mtu nyama ya bata ni tamu sana.Tatizo letu watanzania ni mazoea mazoea.Tumezoea zaidi nyama ya Ng'ombe,mbuzi na kuku.Lakini nyama ya Kondoo,bata na kanga si maarufu sana.Kama mtu ukaaanzisha miradi ya ufugaji wa wnyama kama kondoo,bata na kanga wakapewa promo nadhani biashara itafanyika.Ebu fikiria hoteli zinaagiza bata kutoka magereza bwawani,na unakuta mahitaji yanakuwa makubwa kuliko uzalishaji.