Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Uswahilini siku hizi hasa kipindi cha sikukuu wanapendelea kununua Bata kwani ni mkubwa kiasi cha kutosha familia nzima
 
Umeshanza ufugaji
 
Vipi hujaanza kufuga tu bata nataka sehemu ya kuwa na nunua mayai ya bata kwa ajili ya kutotoresha ila awe Dsm tuwasiliane kupitia 0766559496/0656320899
 
Nilikua cjui
 
Binafsi nina bata 76 ila sifahamu kama kama ninawafuga au wanajifuga kwani kazi yangu ni kuwafungulia asubuhi wanaenda kujichunga wenyewe na jioni kuwafungia.nadhani hata mimi hapa nitanufaika ngoja tusubiri wataalamu.
Hahahahahaha
 
Nilikua nauliza namna/ jinsi ya kuzuia vifo vya viranga wa bata.. Ni chanjo gani inafaa? Nilikua na vifaranga 39 nimebakiwa na 8 tu.. Na budo siko sure kama wata survive hawa walio bakia help please
 
Bata hawaitaji sana chanjo, hawana magonjwa kama kuku. Mimi nawafuga hao viumbe kikubwa wakishatotolewa hakikisha unatenganisha na Bata dume, wanatabia ya kuwadonoa na kuwaua vifaranga. Situmii chanjo yoyote na vifaranga vinakua fresh.
 
Jibu zuri @Ramea,pia hakikisha dume moja likipanda Mara mbili uza au chinja maana yake wanatakiwa wasije kupandana damu moja,maana ikiwa wamepandana koo moja lazima kaugonjwa kakiwapitia either kutokana na bacteria au viruses lazima watakufa karibu wote
 
Nashukuru Kwa majibu hayo, sema sijajua tatizo in nini au Kwa sababu naaoza kufuga,,,!! cha kushangaza hawa bata nilisha watenganisha walikua wanakaa kwenye mabanda maalumu na mama zao!!

Mmoja alikua na vifaranga 16 wote wamekufa, na mungine alikuna na 18 wamebakia 8 tu,,

Vitu ambavyo nahisi vimesababisha, usafi ni banda,

Pili nilikua nalaza kiroba nawawekea pumba then nahis wamekula kinyesi chao,

Tatu nahisi baridi Kwa sababu sikuwaongezea joto lolote usiku kwenye hii winter..

Mfa maji haishi kutapatapa.!!
 
safisha vyombo vya chakula na maji , usiwape pumba ya mahindi yenye uozo (ukungu), wasipandane uzao mmoja, tenganisha madume na bats wanaoatamia au wenye vifaranga.

Sent from my itel it1556 using JamiiForums mobile app
 
Bata akiwa hawezi kutembea anajivuta na mabawa ....ni nini sababu? Ugonjwa au kang'atwa na mdudu???
 
Nilikua nauliza namna/ jinsi ya kuzuia vifo vya viranga wa bata.. Ni chanjo gani inafaa? Nilikua na vifaranga 39 nimebakiwa na 8 tu.. Na budo siko sure kama wata survive hawa walio bakia help please
Nina miaka lukuki sijamla bata kama navyowala madada wa mujini
 
Duh kumbe ufugaji wa Bata ni mgumu fulani ivi
 
Waungwana, kwenye ufugaji wa kuku nimekumbana na changamoto nyingi sana. Sasa nimeamua niuze waliobaki nianze ufugaji wa bata. Kuna mambo sijajua vizuri.
1. Soko lake likoje?
2. Kuna changamoto zipi?
Kuna jamaa mmoja nilikutana naye nanenane last year alikuwa na bata wengi sana, ila hakuwa na mda wa kutoa maelekezo kwa sababu wanunuzi walikuwa wengi hivyo mda mwingi alirudi shambani Ukerewe kufuata mzigo.
Naomba alowahi kufanya biashara hii asaidie maelekezo hapa, kwa faida ya kwangu na wasomaji wengine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…