Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,700
Reaction score
3,921
Mara ya mwisho nilifanya hivi ilikua mwaka jana na wengi niliwasaidia bure tu, lakini hawakushukuru au wengine kuleta mrejesho.

Naam wakili nipo likizo toka hapa kijijini nilipo so naimani naweza kutoa msaada walau ata robo tu tokana na maarifa machache ya sheria niliyo bahatika kuya soma.

Pro bono ya hapa na pale 😀, yasiwe yakuumiza kichwa saanaa wala kufikirisha sanaa, ni hivi vya hapa na pale tu.
 
Master plan ya mji ni nini? au planning area ni nini? Juzi nilikwenda kuangalia kiwanja changu nilichonunua kwa mtu (shamba la mtu) kina status gani katika mipango miji.

Nikakuta kipo kwenye barabara kama tatu na open space. Fate yangu ikoje hapo? Nijenge au nisijenge? Nitalipwa na nifanyeje ili nilipwe ninunue pengne. Thanks.
 
Retired,
Master planning ni mpango wa muda mrefu wa eneo husika kwa miaka mingi ijayo, unapo nunua eneo/ardhi yoyote kisheria tunashauri mnunuzi afanye official search kwenye mamlaka za ardhi na hii itamsaidia kujua status ya eneo husika, kiwanja chako icho ndio basi tena hakuna hela utakayo lipwa hapo kama fidia labda tu mipango hio iwe ni mipya na imewakuteni kwenye eneo husika. Buyer be aware.
 
kuna jamaa namdai..

in fact kuna issue alitakiwa aniunganishe kupitiaa nafasi yake,hata hivyo hakuweza au alishindwa kutekeleza

na pesa INA mwaka na nusu,na kama amenilipa/rejesha ni robo tu nimeambulia..

hii imekaaje ndugu wakili msomi.!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna taasisi ya fedha nilikopa,nimeshindwa kulipa baadhi ya marejesho.Nimeambiwa natumiwa majembe.Hao majembe watanibeba mzimamzima au wataninyanganya vitu nilivyonavyo?
 
Hii ngumu kupata back up ya kisheria unless uyo mliaidiana nae kukupa mchongo ni mmiliki wa hio kampuni/ofice ambae aliku ahidi atakuunganishia mchongo, mkataba ili uwe mkataba lazima kuwepo na nia halali ya kisheria ya watu kuingia ktk mkataba huo na consideration kwa maana ya mabadilishano yenye thamani ya vitu,

kukuahidi atakuunganishia mchongo ni kitu ambacho ungeweza kutizama kwa mbele tu kua kinaweza kua au kisiwe tegemea na position aliyopo huyo jamaa. Endelea kumdai hivi hivi kikawaida tu.
 
Kuna taasisi ya fedha nilikopa,nimeshindwa kulipa baadhi ya marejesho.Nimeambiwa natumiwa majembe.Hao majembe watanibeba mzimamzima au wataninyanganya vitu nilivyonavyo?
Watakunyanganya vitu ulivyo navyo, jaji mlyambina aliwai kusema "mahakama sio chaka la wakopaji kuja kukimbilia kujificha, dawa ya deni ni kulipa."
 
Habari wakili. Naomba kujua kama kesi ya kusafirisha mkaa magunia 20 inastahili kuwa ya uhujumu uchumi. Natanguliza shukrani.
 
Habari wakili. Naomba kujua kama kesi ya kusafirisha mkaa magunia 20 inastahili kuwa ya uhujumu uchumi. Natanguliza shukrani.
Ndio, inaweza kua ya uhujumu uchumi pia, ila tu kupewa kesi ya uhujumu uchumi haimaanishi kwamba ndio tayari mtu kashakutwa na hatia au ni makosa mazito sanaa, hapana ni tuhuma tu kama tuhuma zingine.
 
Et Mwajiri anaweza kumuachisha kazi mtumishi ambaye alishitakiwa polisi kwa kosa la wizi lkn baada ya uchunguzi wa jeshi la polisi mtumishi alionekana hana kosa. Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara ya mwisho nilifanya hivi ilikua mwaka jana na wengi niliwasaidia bure tu, lakini hawakushukuru au wengine kuleta mrejesho.

Naam wakili nipo likizo toka hapa kijijini nilipo so naimani naweza kutoa msaada walau ata robo tu tokana na maarifa machache ya sheria niliyo bahatika kuya soma.

pro bono ya hapa na pale 😀,,, yasiwe yakuumiza kichwa saanaa wala kufikirisha sanaa, ni hivi vya hapa na pale tu.

Habari wakili.
He ninaweza kuishitaki vodacom badala ya wakala aliyeingia mitini na fedha zangu?
 
Et Mwajiri anaweza kumuachisha kazi mtumishi ambaye alishitakiwa polisi kwa kosa la wizi lkn baada ya uchunguzi wa jeshi la polisi mtumishi alionekana hana kosa. Msaada tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana hana uwezo huo, kama ilitokea basi unfair termination, kimsingi mtu yoyote anaweza kutuhumiwa tu mpaka mahakama itakavyo kuta ni tofauti, so haki za huyu mtu hua ziko pale pale kama ilivyokua kabla ya tuhuma au ukamatwaji wa polisi.
 
Yupo bwana alikamatwa na gari ya wizi, huyo bwana nina ugomvi nae wa kibiashara, sasa jamaa alipoulizwa gari kaitoa wapi akasema mimi ndio nimempa.

Polisi wakatukamata sote wakatuweka ndani then tukafikishwa mahakamani.
Kule mahakamani jamaa akakiri kosa ile siku ya kwanza tuliyopelekwa na akahukumiwa miaka 9 gerezani, mimi nilikataa. Mwaka mmoja baadae jamaa akakata rufaa, mahakama kuu ikaamua ashitakiwe upya. Aliposhitakiwa upya akakataa mashitaka na akakana kuwa si mimi niliyempa hiyo gari.

PP hakumuuliza alipewa na nani. Wote tupo nje kwa dhamana.
Swali. Kesi ikiisha naweza kumfungulia kesi ya kumdai fidia huyu bwana kwa kunizalilisha, gharama za kesi na kunipotezea muda?
 
Ahsante sana,nikimuwekea dhamana mtuhumiwa harafu akatoroka Mimi nifanyaje niepuke adhabu au mkono wa sheria?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikawaida ukimuwekea mtu dhamana na akatoroka basi wewe mdhamini hua unapaswa kufika mahakamani na kutoa taarifa mara moja juu ya tukio ilo, mahakama itakupa order ya wewe kumtafuta hadi kumpata ila ukishirikiana na jeshi la polisi, endapo itaonekana kabisaa jamaa hajapatikanika basi mahakama hua inachukua bond uliyoiweka kwa muda mpaka siku atakapo patikanika au inakutozesha fine ulipe na wewe ufanye maombi ya kujitoa kama mdhamini kwa mtu huyo, kwa busara muda mwingine mahakama hua zinawaacha tu huru wadhamini hao na inaendelea na utaratibu wa usikilizwaji in absentia angali mtuhumiwa hayupo, hakuna mtu anaeweza kufungwa kwa kosa la mtu mwingine kisa alimdhamini.
 
Back
Top Bottom