Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Mkuu ebu naomba ushauri wako kwenye hili suala πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Wakuu poleni na majukumu, naombeni msaada wenu mawakili wasomi, na wadau wengine Kwenye jukwaa hili. niende moja kwa moja kwenye mada...
Mkuu pole sanaa na maswaibu hayo uliyo yapata.

Mosi unapaswa kujua kua swala lako limegawanyika ktk sehemu mbili, moja ni ishu ya kimkataba na pili ni ishu ya kikampuni kwa maana ya shares.

1. Ili kesi ya madai ifike mahakamani ni lazima kuwe na kitu kimoja kinachoitwa cause of action, kisababishi/msingi wa madai,,, sasa hapa ni lazima uwe makini nako je msingi wa madai yako unataka uweje ni wale jamaa kukuvunjia makubaliano kinyemela na kukutimua bila malipo ya aina yoyote au ni wewe kunyimwa shares zako bila mpango sahihi anuai.

Lakini ni lazima kwanza kabla haujajibu moja hapo juu wewe uandae mazingira rafiki na wezeshi ya madai yako kwa maana kama kuna memorandum ya makubaliano, jumbe za email, barua, makubaliana nk nk.

Taratibu zingine utashauriwa hapa hapa tu, ila jua kwanza juu ya haya machache hapa juu na useme ulichokua unataka pia, ni izo milion 30, shares au fidia? Je pakuwabania ni wapi? Cause of action yako ulitaka iwe ipi?
 
Mkuu pole sanaa na maswaibu hayo uliyo yapata.

Mosi unapaswa kujua kua swala lako limegawanyika ktk sehemu mbili, moja ni ishu ya kimkataba na pili ni ishu ya kikampuni kwa maana ya shares...

Asante mkuu kwa reply yako..kitu hasa ninachotaka kwa hawa jamaa ni fidia, maana hata hyo 30M sikuwa nimekubaliana nayo ndio maana unaona nimesema aliyekuwa ana-negotiate hyo 30M siyo mimi. 30M kwangu nilikuwa naona kama ni tusi maana kazi niliyokuwa nimewafanyia hao jamaa tangia tunakutana na sehemu ambao niliwapeleka wakaweza kuwekeza hailingani kabisa na hyo 30M.

Kimsingi hapa ni kuwa tulikuwa na makubaliano ambayo nilisisitiza yawekwe kwenye maandishi na jamaa hawakuandaa yale maandishi kwa wakati muafaka. Baadae mimi nikaandaa yale makubaliano na wakati tunajadiliana vipengele vya yale makubaliano ndo yakatokea yalitokea.

Ninazo mails nyingi tu ambazo tulikuwa tunabadilishana nyingine za kazi na nyingine za kuhusu yale makubaliano ambayo niliandaa na kuyatuma kwao. Na kuna email kabisa wanakiri kuwa tuna makubaliano,

Nadhani pa kuwabania ni hapo walipovunja makubaliano kinyemela maana kama kuna wizi nilifanya nadhani hii ilitakiwa ithibitiswe na mahakama na sio wao kunihukumu na kuchukua hatua.
 
Asante mkuu kwa reply yako..kitu hasa ninachotaka kwa hawa jamaa ni fidia, maana hata hyo 30M sikuwa nimekubaliana nayo ndio maana unaona nimesema aliyekuwa ana-negotiate hyo 30M siyo mimi. 30M kwangu nilikuwa naona kama ni tusi maana kazi niliyokuwa nimewafanyia hao jamaa tangia tunakutana na sehemu ambao niliwapeleka wakaweza kuwekeza hailingani kabisa na hyo 30M...
well, nimepitia maelezo yako kwa umakini kabisaa na nimeona ni ukweli una madai ya msingi ni kiasi cha wewe tu sasa kuhamua kuwapeleka hao jamaa mahakamani, ukiangalia maelezo yako yalikua ni mchanganyiko wa ishu za shares kwa maana ya commercial case na ishu ya kimkataba kwa maana ya contractual case,

lakini ukiangalia hapo ni wazi unaweza dili na hii ishu ya ukiukwaji wa makubaliano kwa kufungua kesi ya madai dhidi ya hao jamaa,

sasa kwa kuanza ni unatakiwa uwatumie demand letter hao jamaa, hii ni hua ni kama barua ya ukumbusho wa deni unalowadai na hatua unazofikiria kuzichukua dhidi yao kama hawatakulipa hela yako kwa wakati huo utakao usema humo ndani.

Ishu ya pili sasa ni kufungua kesi mahakamani, ambapo hapa nazani unaweza kutafuta wakili akakusaidia sana na ukashinda haki yako.
 
Kuna jamaa tulimpa fedha mimi na wife ili atutengenezee kazi flani, nina mpango wa kumfungulia kesi ya utapeli kwa sababu ni mwaka sasa, back up ya malipo ilikua ni kwa simu na hatuna ushahidi, je tutashinda? vipi na gharama za kufuatilia tunaweza kumuwekea azilipe?
 
Ndio inawezekana, hii ishu ya maandishi yako wapi? Ushaidi huko wapi? Hua inatumiwa na watu kama kujidefend sanaa, kumbe hata hua haisaidii, ushaidi ni unaweza kutengenezwa pale pale wakati wa usikilizwaji wa kesi na mdaiwa akashindwa vibaya vibaya na hoja zake za ushaidi huko wapi?

Mnaweza kumfungulia mashtaka huyo bwana mkadai fidia na hasara sababishi,,, cha kufanya tengenezeni mazingira ya ushaidi tu mfano kumpigia na kumrekodi kwenye simu, jumbe mbali mbali za sms mkijafanya kumuulizia kuhusiana na kazi yenu na kama hela haikutosha mumuongeze aje afanye kazi na sio kukimbia tu, ata respond back na hapa mnakusanya ushaidi ambao unaonesha kweli kulikua na hilo tukio na mdaiwa analijua vizuri sanaa.
 
Nimenunua eneo sehemu,muuzaji tukaandikishana kwa mwanasheria vzr kabisa lakini nilipo peleka kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa akasema hilo eneo lilisha uzwa kaa mtu mwingine.nilipo mfuata muuzaji akakili kweli eneo limeuzwa na akaamua kunipatia eneo lingine.

Baadae nakuja kugundua hilo eneo limekopewa bank na hati zipo bank na bank wameamua kuuza hayo maeneo na pia nakuja kugundua aliyeniuzia na kuandikishana mkataba kumbe ni dalali tu na si mmoja wa wamiliki kwa hiyo kampuni.

Kwahiyo mkataba wangu unasomeka mm na huyo dalali na si mmiliki halali wa eneo ingawa mwenye eneo tulikua tunawasilina na anajua kua nimeuziwa mm hilo eneo.

Je hili limekaaje!?
 
well, nimepitia maelezo yako kwa umakini kabisaa na nimeona ni ukweli una madai ya msingi ni kiasi cha wewe tu sasa kuhamua kuwapeleka hao jamaa mahakamani, ukiangalia maelezo yako yalikua ni mchanganyiko wa ishu za shares kwa maana ya commercial case na ishu ya kimkataba kwa maana ya contractual case, lakini ukiangalia hapo ni wazi unaweza dili na hii ishu ya ukiukwaji wa makubaliano kwa kufungua kesi ya madai dhidi ya hao jamaa, sasa kwa kuanza ni unatakiwa uwatumie demand letter hao jamaa, hii ni hua ni kama barua ya ukumbusho wa deni unalowadai na hatua unazofikiria kuzichukua dhidi yao kama hawatakulipa hela yako kwa wakati huo utakao usema humo ndani.

Ishu ya pili sasa ni kufungua kesi mahakamani, ambapo hapa nazani unaweza kutafuta wakili akakusaidia sana na ukashinda haki yako.

Asante sana mkuu..unajua kuna watu eti walikuwa wananiambia kwa vile sikuwa na mkataba (legal contract) na hao Jamaa eti sina cha kuwadai. Nikawa nashangaa tu ila mimi nilijua tu kuwa nina strong case against them.

Sasa mkuu ebu nishauri hapa hili shauri langu endapo nitawaandikia Jamaa barua ya demand na wakakaid kutekeleza natakiwa nikafungue Mahakama Gani??? Mahakama ya wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi (mkoa)??
 
Ndio inawezekana, hii ishu ya maandishi yako wapi? Ushaidi huko wapi? Hua inatumiwa na watu kama kujidefend sanaa, kumbe hata hua haisaidii, ushaidi ni unaweza kutengenezwa pale pale wakati wa usikilizwaji wa kesi na mdaiwa akashindwa vibaya vibaya na hoja zake za ushaidi huko wapi? Mnaweza kumfungulia mashtaka huyo bwana mkadai fidia na hasara sababishi,,, cha kufanya tengenezeni mazingira ya ushaidi tu mfano kumpigia na kumrekodi kwenye simu, jumbe mbali mbali za sms mkijafanya kumuulizia kuhusiana na kazi yenu na kama hela haikutosha mumuongeze aje afanye kazi na sio kukimbia tu, ata respond back na hapa mnakusanya ushaidi ambao unaonesha kweli kulikua na hilo tukio na mdaiwa analijua vizuri sanaa.
Shukran mkuu
 
Nimenunua eneo sehemu,muuzaji tukaandikishana kwa mwanasheria vzr kabisa lakini nilipo peleka kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa akasema hilo eneo lilisha uzwa kaa mtu mwingine.nilipo mfuata muuzaji akakili kweli eneo limeuzwa na akaamua kunipatia eneo lingine.

Baadae nakuja kugundua hilo eneo limekopewa bank na hati zipo bank na bank wameamua kuuza hayo maeneo na pia nakuja kugundua aliyeniuzia na kuandikishana mkataba kumbe ni dalali tu na si mmoja wa wamiliki kwa hiyo kampuni.

Kwahiyo mkataba wangu unasomeka mm na huyo dalali na si mmiliki halali wa eneo ingawa mwenye eneo tulikua tunawasilina na anajua kua nimeuziwa mm hilo eneo.

Je hili limekaaje!?
Mkuu pole na majanga yaliokupata, kisheria tunasema hakuna uuzwaji wa ardhi ambao hautopitia sheria ya ardhi namba 4 au namba 5 ya 1999, na marejeo yake, sasa sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 inasema bayana kua uuzwaji wa ardhi lazima ufuate misingi iliyowekwa ktk vifungu vya 37, 38, 39 na 40 ambavyo vyote vinagusia swala la kumtaarifu kamishina wa ardhi, ubadilishwaji wa umiliki tokwa mtu mmoja kwenda kwa mwimgine nk.

Lakini pia tunasema uuzwaji wa ardhi lazima uwe umepitia official search na mnunuzi akajiridhisha juu ya umiliki wa eneo husika, kitu ambacho wewe haukufanya,,, walau mngeenda hata kwa mwenyekiti hapo mnepata taarifa,,, na unasema ardhi hio imewekwa kama mkopo na bank imeshachukua which means ardhi izo zilikua tayari zimesha sajiliwa.

Sasa nafasi uliyo nayo wewe sio kupata tena hio ardhi, hapana ni kufungua kesi ya utapeli dhidi ya huyo dalali na mwenye eneo wote kwa ujumla, na kwa bahati nzuri ushaidi na mashaidi unao, so cha msingi pigania hela yako irudi tu na sio ardhi tena.
 
Asante sana mkuu..unajua kuna watu eti walikuwa wananiambia kwa vile sikuwa na mkataba (legal contract) na hao Jamaa eti sina cha kuwadai. Nikawa nashangaa tu ila mimi nilijua tu kuwa nina strong case against them.

Sasa mkuu ebu nishauri hapa hili shauri langu endapo nitawaandikia Jamaa barua ya demand na wakakaid kutekeleza natakiwa nikafungue Mahakama Gani??? Mahakama ya wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi (mkoa)??
Mara nyingi demand letter hua hazijibiwi au zikijibiwa majibu hua ni negative tu, sasa lengo lake ni kwamba ndugu mdai kuna effort ulizifanya kabla na hata wakati wa ulipwaji gharama za kesi nakala ya barua hii hua inasaidia sanaa.

Baada ya majibu ya demand letter, wewe utapaswa kujua ni hatua ipi inafuata ambayo ni mahakamani, then utapiga hesabu unataka kulipwa kiasi gani kwa sababu gani madai yako yawe ni kiasi icho na hapa ndio utapata mahakama sahii ya kwenda, mfano kuanzia milion 251 na kuendelea itakulazimu uipeleke mahakama kuu, ila ikiwa madai yako ni chini ya milion 250 kushuka mpaka milion 50 itakulazimu kuipeleka mahakama ya wilaya au hakimu mkazi,,, gharama hizi hua sio fidia unayotaka upewe(yaan general damage) hapana ila ni hasara ambayo umesababishiwa na kiasi iko ndio ilikua haki yako wewe kukipata(specific damage).

Unaweza kumtafta wakili hapo ulipo na akakusaidia ktk hili zaidi.
 
Nilikua mshauri wa taasisi moja ya kutoa mikopo kwa wateja. Mkataba ulikua instructions zipite kwangu Mkurugenzi. Meneja mmoja wa taasisi hiyo akatoa instructions kwa mtu mwingine ambae alifoji taarifa zangu sahihi na mihuri na kuwasilisha zikatumika bila kunijulisha kuchukua mkopo wa 1.6 billion. Je naweza dai fidia mahakamani kwa taasisi hii kukiuka na kujinufaisha kwa forged documents.
 
Walikufanyia impersonation, ambalo ni kosa la jinai, ambapo hauwezi kulipwa fidia,,, ila unaweza kufungua kesi ya madai ukionesha ni namna gani impersonation ile ilivyokuathiri na hasara uliyoipata, mfano imekuletea usumbufu usio na sababu, mamlaka za mapato zimekudai baadhi ya kodi, utatakiwa kuwajibila mahala flani, imekuletea magonjwa ya kisaikolojia 'irrepelable loss', itakuletea matatizo ya utakatishaji fedha, nk nk.
 
666 chata,

Nashukuru kwa Mara nyingine mkuu...naomba unijibu hili pia kama hutojali.

Baada ya kuwaandikia demand letter na kuahinisha kiasi cha madai yangu na lengo langu la Kutafuta haki yangu kwingine kama hawatatoa ushirikiano (kunilipa ninachodai) Je natakiwa kuchukua muda gani kwa Mimi kwenda mahakamani baada ya ule muda nilioweka Kwenye demand letter kuisha na wao kutokuonyesha ushirikiano..
 
Kikawaida demand letter hua inawapaga wadaiwa siku 14 tu, kwamba ndani ya siku 14 msipo nilipa kiasi ikii na ikii then ntachukua zinazofuata ambazo ni mahakamani.
 
Kikawaida demand letter hua inawapaga wadaiwa siku 14 tu, kwamba ndani ya siku 14 msipo nilipa kiasi ikii na ikii then ntachukua zinazofuata ambazo ni mahakamani.

Asante mkuu...Msingi wa swali langu ulikuwa...Je naweza kuwaandikia demand letter ya hzo siku 14 let's say January 2020 halafu kesi nikaja kufungua January 2021??? Hyo inakubalika kisheria???

Maana kuna sehemu ulisema Mwisho wa kesi ya madai ni miaka 6...tangia madai yatokee kama nilielewa vzuri.
 
Mimi siyo mwanasheria lakini ngoja nikwambie kitu, kwenye kupitia Pitia Sheria ya Civil procedure code cap 33 sijawahi kuona kifungu kinachosema kwamba kesi ya madai ni Lazima kuwe na 'demand notice ' bali sheria hiyo ya CiviL procedure code imesema kuwa kesi yoyote itafunguliwa kwa njia ya 'plaint ' hivyo basi unaweza kufungua kesi moja kwa moja bila ya kuanza na demand notice,
Except kwenye kesi za madai dhidi ya serikali, 'suit against government ' ambapo Unatakiwa kutuma notice kwa mwanasheria mkuu wa serikali,kama inavyotakiwa na sheria ya Government Proceedings Act
 
Asate mkuu wewe sio mwanasheria ila michango yako inaeleweka sana na nachelea kusema upo njema kwa kweli.
 
Mimi siyo mwanasheria lakini ngoja nikwambie kitu, kwenye kupitia Pitia Sheria ya Civil procedure code cap 33 sijawahi kuona kifungu kinachosema kwamba kesi ya madai ni Lazima kuwe na 'demand notice ' bali sheria hiyo ya CiviL procedure code imesema kuwa kesi yoyote itafunguliwa kwa njia ya 'plaint ' hivyo basi unaweza kufungua kesi moja kwa moja bila ya kuanza na demand notice,
Except kwenye kesi za madai dhidi ya serikali, 'suit against government ' ambapo Unatakiwa kutuma notice kwa mwanasheria mkuu wa serikali,kama inavyotakiwa na sheria ya Government Proceedings Act

Mkuu unaweza nitumia PDF ya hiyo Sheria ya madai mkuu Wangu na Mimi niipitie kidogo...maana nimeitafuta google siipati..
 
Back
Top Bottom