Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Wa Igima,
Ni kesi ya kuua kwa kukusudia, kitendo cha kuwachukua watu wengine wa ziada ni alikua anajua analoenda kulifanya na alikusudia kutenda maovu na tukio lote alikua na idea nalo, mkewe ana husika ktk kupanga njama hio ya kufanya uovu huo.
 
mpimamstaafu,
Doooh 🤣🤣 hakuna mtu anaeweza kumnyanganya mtu mwingine kiwanja isipokua rais/serikali tu na kukiwa na fidia kwa mnyanganywaji. Na hakuna mtu mwingine anaeweza kumilikishwa kiwanja ambacho mwenye nacho hajataka kimilikiwe na mtu mwingine, yaani hakuna madili ya juu kwa juu.
 
Ukimlipa MTU deni harafu asisain settlement deed anaweza kunigeuka kuwa cjamlipa.
Hata akikugeuka kama ushahidi wa kutosha upo basi kusaini sio excuse ya mtu kusema et hakulipwa.
 
Kuna mtu nimemfungulia kesi ya jinai na anataka kuweka wakili hivyo itabidi kesi iamishwe je ntajuaje kesi kama
imeamishwa?
 
samahani wakili....
mimi nilikopa hela kwa mtu binafsi tukaandikishana nitamlipa riba...kwasababu nlikuwa na shida nkakubnali...miaka mitatu imeisha sijamlipa riba ila juzi nmemlipa laki tano na nusu alionikopa riba nimekataa....ameenda kunishtaki kwa mkuu wa wilaya..nkagoma pia wananiambia watakuja kuuza nyumba yangu,....hili likoje kisheria??naombamsaada wa haraka...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enguraruu,
Hahahahah hawawezi kuuza nyumba yako, sasa kwanini unataka kutumia mwanya wa sheria kutenda maovu? Dawa ya deni kulipa, ila kwa bahati iliyopo kwako ni kwamba, sheria inakataza watu wasiokua na leseni ya kukopesha kibiashara kufanya ivyo, so huyo hapaswi kudai riba wakati biashara anayoifanya haikua na leseni na wala hakulipa kodi za makato ya biashara hio ya ukopeshaji, usiofu.
 
Kuna mtu nimemfungulia kesi ya jinai na anataka kuweka wakili hivyo itabidi kesi iamishwe je ntajuaje kesi kama
imeamishwa?
Mahakama itawajulisheni wote kua sasa kesi imehamishwa.
 
Habari wakuu....Ninaomba kujuzwa kidogo juu ya suala la makato ya mshahara wa mfanyakazi. Je,inawezekana katika mazingira yoyote yale kukata mshahara wote wa mfanyakazi?
Asante
 
Habari wakuu....Ninaomba kujuzwa kidogo juu ya suala la makato ya mshahara wa mfanyakazi. Je,inawezekana katika mazingira yoyote yale kukata mshahara wote wa mfanyakazi?
Asante
Haiwezekani kwa mazingira yoyote yale, na ni makosa makubwa kwa muajiri.
 
Naomba kufahamu vipengele vinavyoweza kuunda "kosa la kukusudia kuiba" au kosa la kukusudia kuiba linaweza kuthibitishwa namna gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Attempt to theft? Hakuna kosa la hivi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa jinai, inakazia kwa kusema, "A person shall not be deemed to take a thing unless he moves the thing or causes it to move." Kwamba atleast alikiondoa icho kitu alicho taka kukuiba sehem moja kwenda sehem nyingine walau, lakin sio mawazo tu et alitaka kuiba huyu.
 
Mkuu kwema. Mm nimenunua kiwanja mkoa flani kanda ya ziwa na mm naishi mkoa mwingine. Sasa nililipa upimaji shirikishi laki na nusu. Ila wakati wanafanya upimaji sikuwepo hivo wapimaji waliunganisha kiwanja changu na cha jirani kikawa kimoja na wakaandika jina la jirani.

Sasa juzi nikaenda kuangalia utaratibu nilipie hati ndo nikagundua hilo. Nikamwambia jirani tuchange tulipie tupimiwe upya akagoma akasema yeye hana tatizo. Nikaona isiwe tabu nijilipue mwenyewe nilipe nipimiwe upya. Ila nilipoambiwa gharama nikaxhoka 1.5mil ambayo sikuwa nayo. Ninachotaka kujua ni gharama za kufanyiwa upimaji upya ni sh ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attempt to theft? Hakuna kosa la hivi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa jinai, inakazia kwa kusema, "A person shall not be deemed to take a thing unless he moves the thing or causes it to move." Kwamba atleast alikiondoa icho kitu alicho taka kukuiba sehem moja kwenda sehem nyingine walau, lakin sio mawazo tu et alitaka kuiba huyu.
Sawa nimekuelewa vzr sana mkuu! Lakini kama kitu kikikamatwa na polisi nje ya wilaya husika. Je huo ni wizi au kusudio la kuiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mku
Mkuu kwema. Mm nimenunua kiwanja mkoa flani kanda ya ziwa na mm naishi mkoa mwingine. Sasa nililipa upimaji shirikishi laki na nusu. Ila wakati wanafanya upimaji sikuwepo hivo wapimaji waliunganisha kiwanja changu na cha jirani kikawa kimoja na wakaandika jina la jirani. Sasa juzi nikaenda kuangalia utaratibu nilipie hati ndo nikagundua hilo. Nikamwambia jirani tuchange tulipie tupimiwe upya akagoma akasema yeye hana tatizo. Nikaona isiwe tabu nijilipue mwenyewe nilipe nipimiwe upya. Ila nilipoambiwa gharama nikaxhoka 1.5mil ambayo sikuwa nayo. Ninachotaka kujua ni gharama za kufanyiwa upimaji upya ni sh ngapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu gharama za upimiwaji viwanja/kiwanja haziwezi kuzidi laki na elf 50, na hii ilishushwa na wizara ya ardhi toka mwaka jana ambako kiasi kilikua ni 250,000. so hakuna anaetakiwa kuzidisha laki na elf 50 na waziri alionya sanaa, tafta haya makampuni huko ulipo yatakuwepo tu Visible Planners au Afro Max, wanafuata bei hio hio ya laki na 50.
 
Habari wakili msomi nimejaribu kukucheki dm naona umefunga naomba nicheki kama hutojali tafadhali
 
Mkuu,

Mimi mke wangu anafanyia kazi mamlaka fulani ya kiserikali kama mfanyakazi Wa muda.
Walijaza mkataba Wa kazi chini ya mwanasheria Wa mamlaka hiyo lakini

1:nakala ya mkataba wanayo wao kama mamlaka hats copy hawajampa.je ni sahihi?

2:mshahara wanalipwa lakini walikubaliana kwa mdomo tu,hata Kwenye mkataba wao hakuna kifungu cha malipo,je ni sahihi?

3:sheria inasemaje kuhusu mfanyakazi Wa ajira isiyo ya kudumu(ya muda) maana Kwenye mkataba hakuna ukomo Wa huo muda na sasa ni takribani miezi 18
 
Back
Top Bottom