Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Mtu unaweza kufungwa kwa kufanya makosa Kwenye kazi yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi,hata kama kipengele hakipo Kwenye mkataba?
 
Mkuu naomba kupata ufafanuzi katika hili,

kuna tofauti gani kati ya kesi ya 'wizi wa uaminifu' na 'Stealing by agent'. Kati ya hizo ipi ni mbaya na yenye adhabu kubwa zaidi na niadhabu zipi hizo.

Pia huwa nini kinatokea pale PP anapokucharge kwenye kifungu flani ambacho hakina adhabu ya kukuhukumu.

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba kupata ufafanuzi katika hili,

kuna tofauti gani kati ya kesi ya 'wizi wa uaminifu' na 'Stealing by agent'. Kati ya hizo ipi ni mbaya na yenye adhabu kubwa zaidi na niadhabu zipi hizo.

Pia huwa nini kinatokea pale PP anapokucharge kwenye kifungu flani ambacho hakina adhabu ya kukuhukumu.Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Centia2,
Mkuu hakuna tofauti yoyote kati ya term izo mbili, ukisoma kifungu cha 273 (B) kinasemea juu ya wizi wa kuaminiwa kwa mtu ambae amepewa kitu, kaachiwa kitu kwa kuaminiwa alaf yeye akaondoka nacho kwa madhumuni ya kuiba, basi kosa ilo kitaalam ni stealing by agent ambayo ndio huo huo wizi wa kuaminiwa....

kama kosa litakua charged kwenye charge alaf hakuna kifungu kinachotoa adhabu moja kwa moja kwenye kosa ilo, basi jua hua kuna makosa generally ambayo hua yanatoa adhabu kwa makosa yanayofungamana na kosa husika, mfano ukiangalia kifungu namba 265 cha penal code kinatoa adhabu generally kwa makosa ya wizi just in case baadhi ya vifungu vikiwa silent kwenye adhabu inayoendana na wizi.
 
Mtu unaweza kufungwa kwa kufanya makosa Kwenye kazi yanayoweza kuhatarisha usalama wa nchi,hata kama kipengele hakipo Kwenye mkataba?
Katiba ni sheria mama, sheria ndogo ndogo ndio zinazotoa adhabu na kuya hainisha makosa, hakuna kosa ambalo halipo kwenye sheria, kama lipo basi ni asilimia 1 katika 100.
 
D Metakelfin,
1. Wao kubakia na copy sio hoja kwamba haki ya mtu inawezwa kuvunjwa, incase likitokea la kutokea ataenda kuwaomba copy.

2. Ni sahii mkataba/makubaliano yanaweza kua kwa njia ya maandishi au mdomo.

3. Mikataba ya chini ya miaka 5 hua inaitwa Contract Fixed term, inaweza kua hata kwa miaka mitatu mitatu na mpaka miaka minne, ila ni marufuku mikataba ya namna hio iwe chini ya mwaka mmoja, ajira yake inaweza isiwe ya kudumu kwa kua anafanya nao kazi labda kwa miaka mitatu mitatu, kama hawakuandika miaka basi uyo aliemuajiri yupo kwenye matatizo makubwa sanaaa.
 
666 chata,
Hawajataja kikomo cha muda Wa ajira. tena ni mamlaka ya serikali na viongozi wakubwa tu huwa wanaenda pale lakini mkataba wao ni wa kibabaishaji je afanyaje kuweka mambo sawa bila kuathiri hiyo ajira?
 
Mku

Mkuu gharama za upimiwaji viwanja/kiwanja haziwezi kuzidi laki na elf 50, na hii ilishushwa na wizara ya ardhi toka mwaka jana ambako kiasi kilikua ni 250,000. so hakuna anaetakiwa kuzidisha laki na elf 50 na waziri alionya sanaa, tafta haya makampuni huko ulipo yatakuwepo tu Visible Planners au Afro Max, wanafuata bei hio hio ya laki na 50.
Kuna mtu ananidai million 4 na mpango wangu ni kumdhulumu kabisa! Na nimemkopa tena mdogo wake yani nampango wa kudhulumu familia nzima je wakinifungulia kesi ya wizi wa uaminifu mahakamani watanishinda?
Kwa kosa hilo hakupati, kosa hilo ni pale ambapo kitu kimewekezwa au kuhifadhiwa kwako. Kilichopo hapo ni makubaliano /mkataba wa kukopeshana pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakili naomba unisaidie kuna ndugu yangu alifunguliwa kesi ya kufoji na kujipatia nyumba kwa njia ya kugushi ingawa alikuwa na haki bahati mbaya akashindwa kesi lakini baadae akapata uthibitisho kuwa wale waliomshinda vielelezo vyao vilikuwa vya kufoji ila muda ulikuwa umepita.

Je< anaweza kufungua tena mahakamani kutengua maamuzi yalitoa haki kwa yule aliyemshinda.Ushahidi wote anao.
 
Nikitaka kufungua kesi mahakamani nafanyeje?

Sent using Jamii Forums mobile app
inategemeana, kama ni mahakama ya mwanzo ukifika unapeleka malalamiko yako masijala zao then wanakupa fomu unazijaza, au unapeleka malalamiko yako kwa njia ya maandishi tu, kama ni mahakama za wilaya hadi mahakama kuu kuna documents zakutengenezwa ambapo unaomba msaada wa mawakili.
 
wakili naomba unisaidie kuna ndugu yangu alifunguliwa kesi ya kufoji na kujipatia nyumba kwa njia ya kugushi ingawa alikuwa na haki bahati mbaya akashindwa kesi lakini baadae akapata uthibitisho kuwa wale waliomshinda vielelezo vyao vilikuwa vya kufoji ila muda ulikuwa umepita .Je anaweza kufungua tena mahakamani kutengua maamuzi yalitoa haki kwa yule aliyemshinda.Ushahidi wote anao.
ndio anaweza kuikatia rufaa hukumu hio, japokua yuko nje ya muda, basi atafanya maombi maalumu katika mahakama ya juu tofauti na ile aliyo hukumiwa nayo, maombi haya itakua ni juu ya kuomba kuongezewa muda wa kukata rufaa kwa sababu hizo na hizo na hizo atakazo zitaja, baada ya kupewa ruhusa ya kuleta maombi yake ya rufaa, then atakatia rufaa.
 
Habari wakili, baba yangu alinunua kiwanja mwaka 89 kwa thaman ya ng'ombe mmoja. Huyo aliyemuuzia akafariki, watoto wake pamoja na wajukuu wakaja juu wakidai pesa aliyonunua mji baba kwa baba yao ni ndogo.

Baba akakataa hapo ukatokea mtafaruku pande zote mbl kugombea mji serkal ikainglia kat na kuchukua mji. Ili lipoje kisheria naweza kwenda mahakamn kufungua kesi ili kugomboa mji mikonon mwa serikal ikiwa baba yangu alikufa na nyaraka ninazo mimi.
 
Mkuu mimi nilimpatia pesa mtu aninunulie Korosho,. Kinyume chake akanisumbua hadi msimu ukaisha na pesa kala,.

Kilichofanyika tukaandikishiana kwamba atanilipa lakini sioni dalili Za kulipwa alichofanya ni kunipoza kidogo tu kiasi cha Ile fedha..

Nikienda mahakamani naweza kupata msaada kwenye hili?

Je? Nikienda mahakamani siwezi ingia matatani kwa ishu ya Kangomba?.



بندی ا
 
Habari wakili, baba yangu alinunua kiwanja mwaka 89 kwa thaman ya ng'ombe mmoja. Huyo aliyemuuzia akafariki, watoto wake pamoja na wajukuu wakaja juu wakidai pesa aliyonunua mji baba kwa baba yao n ndogo...baba akakataa hapo ukatokea mtafaruku pande zote mbl kugombea mji serkal ikainglia kat na kuchukua mji. Ili lipoje kisheria naweza kwenda mahakamn kufungua kesi ili kugomboa mji mikonon mwa serikal ikiwa baba yangu alikufa na nyaraka ninazo mimi
Mkuu kama una vielelezo vyote basi ningekushauri uende Baraza la Ardhi la Wilaya au la Kata (tegemea na thamani ya ilo eneo kwa sasa), kawafungulie mashtaka wote wawili yaani ile familia ya kwanza na hio serikali ya kijiji iliyochukua ilo eneo, maombi yako yakiwa ni kuliomba baraza lithibitishe wewe ndio mmiliki halali wa ile ardhi, itoe oda ya kuwaondoa watu wote walioko kwenye ilo eneo na itoe amri kwa serikali ya kijiji ikurudishie eneo.

Kisheria ilo eneo mzee wako alilinunua kihalali kwa wakati huo ambapo hata hakukua na masharti mengi ktk manunuzi ya ardhi, lakini pia kulikua kuna mabadilisho ya thamani kwa kila mmoja, eneo ilo lilifanikiwa kuhamishwa umiliki kwenda kwa mtu mwingine kihalali.
 
Mkuu mimi nilimpatia pesa mtu aninunulie Korosho,. Kinyume chake akanisumbua hadi msimu ukaisha na pesa kala,.

Kilichofanyika tukaandikishiana kwamba atanilipa lakini sioni dalili Za kulipwa alichofanya ni kunipoza kidogo tu kiasi cha Ile fedha.
Ndio ukienda Mahakamani unaweza pata msaada kwenye ilo.... hayo makubaliano yenu mlioyandikishana ndio hayo hayo unayoenda kuyadai, kwamba amekiuka deed of settlement/hati ya makubaliano, ivyo akulipe kama mlivyokubaliana na faida juu.... nenda mahakamani wala usiogope, wewe ni mdai ivyo hakuna kitakacho kugeukia.
 
Ahsante wakili, umenipatia mwanga na wapi pa Kuanzia
Mkuu kama una vielelezo vyote basi ningekushauri uende Baraza la Ardhi la Wilaya au la Kata (tegemea na thamani ya ilo eneo kwa sasa), kawafungulie mashtaka wote wawili yaani ile familia ya kwanza na hio serikali ya kijiji iliyochukua ilo eneo, maombi yako yakiwa ni kuliomba baraza lithibitishe wewe ndio mmiliki halali wa ile ardhi, itoe oda ya kuwaondoa watu wote walioko kwenye ilo eneo na itoe amri kwa serikali ya kijiji ikurudishie eneo.

Kisheria ilo eneo mzee wako alilinunua kihalali kwa wakati huo ambapo hata hakukua na masharti mengi ktk manunuzi ya ardhi, lakini pia kulikua kuna mabadilisho ya thamani kwa kila mmoja, eneo ilo lilifanikiwa kuhamishwa umiliki kwenda kwa mtu mwingine kihalali.
 
Back
Top Bottom