Patel sio Mtanzania, media za Tanzania acheni kupotosha umma

Patel sio Mtanzania, media za Tanzania acheni kupotosha umma

Mtanzania ateuliwa kuwa Mkuu wa Shirika la Ujasusi la FBI nchini Marekani. Hii ni hatua ya uundaji wa serikali wa utawala mpya wa Rais Trump.

Kash Patel amezaliwa Marekani lakini Baba yake ni Mganda na Mama yake ni Mtanzania walioamua kuhamia Marekani ambako huko ndiko Kash Patel alikozaliwa. Familia hii ina asili ya Uhindi (Gujarati).
View attachment 3245794

NB: Wahindi ukoo huchukua kwa Mama, kwahiyo Patel ni Mtanzania.

Kama kawaida yetu, kudandia treni kwa mbele, sijui ni nani alitupatia ugonjwa huu wa ujinga kiasi hiki? Wazee wa free rides! Je tunapata faida gani kuhubiria dunia kuwa watu wenye uraia wa nchi zingine waliofanikiwa ni watanzania?
View attachment 3245798

Kijana akicheza Ligi ya Ujerumani basi media zinafukuzana kuandika makala kuwa Yussuf Yurary Poulsen kuwa ni mtanzania? Ukiuliza sababu za kwanini ni Mtanzania utabaki kucheka tu, ukitazama vyema utaona Poulsen hana utanzania wowote.

Malaika Mihambo alivyokiwasha kwenye michezo ya Olympic tukaanza ngonjera zetu, kuwa Malaika Mihambo ni mtanzania ilihali yeye ni Mjerumani. Sasa hivi tumeanza kumzunguza Patel kama kijana wetu mzawa wakati kiuhalisia yeye ni Mhindi, Mgujarati mwenye asili sawa na kina Mahatma Gandhi, Dadabhai Naoroji, Azim Premji, Jamsetji Nusserwanji Tata, Diana Edulji, Sam Pitroda, Ajay Jadeja, Irfan Pathan, pamoja na Ravindra Jadeja.
View attachment 3245797

Tanzania hakuna uraia pacha na wengi wa hawa watu wanaopata mafanikio makubwa wanayapata wakiwa sio raia tena wa Tanzania.

Haina mantiki ya msingi na sio afya njema kuona Mwaisa amekaa Tukuyu akicheza mpira na hakuna ukurasa wa TFF wowote umewahi kumuonesha ila akibadilisha uraia akaenda Australia na kukiwasha haswa, admin wa ukurasa wa TFF kule Facebook utaona anavyosifia kuhusu kiwango chake na kuelezea kuwa ni mtanzania.
View attachment 3245796

Tuache hii tabia, hawa ambao tunawaona wanapata shavu basi tunaanza kutafiti kuhusu maeneo gani Tanzania wazazi wao walipita, sio jambo jema.

Abeba
pamoja na mumewe Cherenet wameingia kimagendo Tanzania wakitoka Ethiopia wakitamani kwenda Afrika ya Kusini, kwa bahati nzuri au mbaya wakafanikiwa kufika Mbeya na kukaa kwa muda wa miaka mitano na baadaye kupata nafasi ya kwenda Ufaransa.

Abeba bahati nzuri alikuwa mjamzito hivyo alijifungua mtoto wa kiume na kumpa jina la Dejen ama Daud ksa Kiswahili, Dejen anapenda michezo haswa kikapu na anafanikia kuingia Academy ya Riviera Basketball Academy ambapo anafanya mazoezi kwa bidii kubwa, akiwa na miaka 19 anapata nafasi ya kuonekana na scout wa timu ya Golden State Warriors na kupewa nafasi ya kucheza Pre Season.
View attachment 3245795

Halafu asubuhi unaamka unakutana na wachambuzi njaa wameshiba mihogo wakimzunguza kuwa Dejen ni mtanzania kwa kigezo kuwa aliishi Mbeya, wanasahau kabsa kuwa Abeba pamoja na Cherenet hawana uhusiano wowote na Tanzania, sio kabila bali hata asili yao.

Patel amezaliwa Marekani lakini asili yake ni Mgujarati sio Tanzania hana utanzania wowote, kina Yeriko na wengine acheni kupotosha umma, mtu akipita Tanzania sio kigezo cha yeye kuwa mtanzania, watoto wa mabalozi kutoka nchi nyingine wakizaliwa Tanzania haitoshi wao kuwa watanzania.
View attachment 3245794

Tufikie sehemu tuheshimu jitihada za nchi zao ambazo zimewatengeneza wakafikia hatua hizo. Msilete zile Ngonjera kuwa Obama amekuwa Rais wa Marekani basi Obama ni Mkenya, hakuna hicho kitu.
Acha waitangaze Tanzania; we unapata hasara gani?. Juzi tumewapa Utanzania wachezaji watatu wa kigeni; wakipata timu Ulaya; wanaitangaza Tanzania.
Huyo Jasusi kama Mama yake Mtanzania; huyo ni wetu kabisa.
Likipita kwake faili la TZ; lazima alipe kipaombele
 
Ukienda Hoyoyo wenyeji wanaona fahari kupatambulisha kuwa ni kwa baba yake Salma Kikwete.
Au kuna ile madalali wa viwanja wanakuambia eti ooh kiwanja kiko sehemu nzuri kimepakana na kiwanja cha Riziwani kikwete,unajiuliza who is Riziwani kwani akiwa jirani yangu ndo nini,atakua ananiletea ugali mezani?
Yani ni shobo za kipuuzi tu.
 
Mama wa Patel ni wagujarati kwa asili yake je Patel anakuwaje Mtanzania!??
 
Siku Muhoozi Kainerugaba akiukwaa urais naye tutasema ni mbongo maana kazaliwa DSM.
kainerugaba ndio nani wakati baba yake ni yoweri? Angeitwa tu muhozi yoweri kaguta museveni
 
Tunajipendekezajipendekeza, baadala ya kupambana na CCM ijenge mifumo itakayozarisha watu bora ndani ya Tanzania na kuijenga Tanzania tuko busy kupambana na asili za watu.

Hakuna Mhindi, Muarabu wala mburushi Mtanzania tuache kujidanganya.
 
"Haina mantiki ya msingi na sio afya njema kuona Mwaisa amekaa Tukuyu akicheza mpira na hakuna ukurasa wa TFF wowote umewahi kumuonesha ila akibadilisha uraia akaenda Australia na kukiwasha haswa, admin wa ukurasa wa TFF kule Facebook utaona anavyosifia kuhusu kiwango chake na kuelezea kuwa ni mtanzania."
 
Tunajipendekezajipendekeza, baadala ya kupambana na CCM ijenge mifumo itakayozarisha watu bora ndani ya Tanzania na kuijenga Tanzania tuko busy kupambana na asili za watu.

Hakuna Mhindi, Muarabu wala mburushi Mtanzania tuache kujidanganya.
Kabsa Mkuu!
 
Hapo ndo wakutane na kichaa sasa 😃 narudi home kimya kimya kama Ninja 🥷
Hata mimi aisee huwa sipendi unafki.
Kama kipindi kile Mwakinyo alivyoanza kung'aa baada ya kushinda pambano ulaya alivyokuwa anakwenda alikuwa yeye na kocha wake wa mtaani ila baada ya kushinda wakajifanya kuanza kumuongelea bungeni na wengine kuja kumpokea airport.
Kama ni mimi aisee nashukia Airport ya Kenya halafu napanda bus nakatiza Namanga narudi home kimyakimya nazima simu na kulala nawaacha wakeshe Airport bila mafanikio,Sitaki unafki hata kidogo
 
"Haina mantiki ya msingi na sio afya njema kuona Mwaisa amekaa Tukuyu akicheza mpira na hakuna ukurasa wa TFF wowote umewahi kumuonesha ila akibadilisha uraia akaenda Australia na kukiwasha haswa, admin wa ukurasa wa TFF kule Facebook utaona anavyosifia kuhusu kiwango chake na kuelezea kuwa ni mtanzania."
Kwani unadhani Wanaijeria wanajimwambafai na kina Leo Kokubo pamoja na Joel Chima Fujita, wale sasa hivi ni Wakorea sio Wanaijeria tena.
 
MAMBO MENGINE WALA HAYAHITAJI MSHINDI
HATA UKISHINDA KUWA SIO MTANZANIA ITAKUSAIDIA NINI?
MIMI NAFIKIRI WALIO ANDIKA NI MTANZANIA HATA KAMA NI WAKUUNGA UNGA WAMEFANYA KAZI YA KUITANGAZA NCHI
TUNAHITAJI WATALII/ TUTAHITAJI WAWEKEZAJI, KWA NAMNA YOYOTE AMBAYO HAINA MADHARA YA KUTUTAMBULISHA /KUTUTANGAZA HUKO ULAYA NA MAREKANI NAIUNGA MKONO....
KWANZA UMESHA SEMA MAMA YAKE NI MTANZANIA HIYO INATOSHA KUTUTANGAZA.....
MENGINE POTEZEA SIO KILA KITU UNATAKIWA USHINDE!!!
HUYO MAMA YAKE NI MBANTU AU NAYE ANA RANGI YA KIHINDI?TUANZIE HAPO
 
Hata mimi aisee huwa sipendi unafki.
Kama kipindi kile Mwakinyo alivyoanza kung'aa baada ya kushinda pambano ulaya alivyokuwa anakwenda alikuwa yeye na kocha wake wa mtaani ila baada ya kushinda wakajifanya kuanza kumuongelea bungeni na wengine kuja kumpokea airport.
Kama ni mimi aisee nashukia Airport ya Kenya halafu napanda bus nakatiza Namanga narudi home kimyakimya nazima simu na kulala nawaacha wakeshe Airport bila mafanikio,Sitaki unafki hata kidogo
Utaitwa Mchochezi
 
HUYO MAMA YAKE NI MBANTU AU NAYE ANA RANGI YA KIHINDI?TUANZIE HAPO
Tunanzie hapo! Huyu Bi Mkubwa ana utanzania upi!? Wakati ni Mgujarati mtupu!
images - 2025-02-23T095333.886.jpeg
 
Tanzania does not allow its nationals to hold dual nationality, except in the case of persons under the age of eighteen who had multiple nationality from birth. Multiple nationals automatically lose their Tanzanian citizenship at majority, unless they renounce all other nationality.
Alielezq vizuri tu wakati wa uapisho wako, kuwa mama yake ni mtanzania, Baba ni mganda na yeye Alizaliwa marekani

Mama na baba yake walikutana masomoni India 🇮🇳, na namna baba na Mama yake walivyofika marekani wakitokea Uganda 🇺🇬

Itoshe kusema yeye mwenyewe anatambua asili yake kwa rangi na asili ya taifa ambalo wazazi wake wametokea ndio maana aliweza kuufahamisha ulimwengu na ukaelewa

Mihambo, ubalozi wa ujerumani Tanzania 🇹🇿 ulijivunia yeye na ukapost taarifa zake na kuungana na watanzania kusherekea mafanikio ya mihambo kwa pande zote mbili kwa kuwa Zina husika kwa namna moja au nyingine

Sunak kama sijakosea jina lake naye hivyo hivyo, wapo wengi sana na wanafurahia kuliko unavyochukizwa

Tunachofanya ni kufurahia kwa pamoja na kuwapa hamasa wengine waweze kukimbilia ndoto zao kwa kuwa Dunia ni uwanja mpana
 
Back
Top Bottom