Patel sio Mtanzania, media za Tanzania acheni kupotosha umma

Acha waitangaze Tanzania; we unapata hasara gani?. Juzi tumewapa Utanzania wachezaji watatu wa kigeni; wakipata timu Ulaya; wanaitangaza Tanzania.
Huyo Jasusi kama Mama yake Mtanzania; huyo ni wetu kabisa.
Likipita kwake faili la TZ; lazima alipe kipaombele
 
Ukienda Hoyoyo wenyeji wanaona fahari kupatambulisha kuwa ni kwa baba yake Salma Kikwete.
Au kuna ile madalali wa viwanja wanakuambia eti ooh kiwanja kiko sehemu nzuri kimepakana na kiwanja cha Riziwani kikwete,unajiuliza who is Riziwani kwani akiwa jirani yangu ndo nini,atakua ananiletea ugali mezani?
Yani ni shobo za kipuuzi tu.
 
Mama wa Patel ni wagujarati kwa asili yake je Patel anakuwaje Mtanzania!??
 
Siku Muhoozi Kainerugaba akiukwaa urais naye tutasema ni mbongo maana kazaliwa DSM.
kainerugaba ndio nani wakati baba yake ni yoweri? Angeitwa tu muhozi yoweri kaguta museveni
 
Tunajipendekezajipendekeza, baadala ya kupambana na CCM ijenge mifumo itakayozarisha watu bora ndani ya Tanzania na kuijenga Tanzania tuko busy kupambana na asili za watu.

Hakuna Mhindi, Muarabu wala mburushi Mtanzania tuache kujidanganya.
 
"Haina mantiki ya msingi na sio afya njema kuona Mwaisa amekaa Tukuyu akicheza mpira na hakuna ukurasa wa TFF wowote umewahi kumuonesha ila akibadilisha uraia akaenda Australia na kukiwasha haswa, admin wa ukurasa wa TFF kule Facebook utaona anavyosifia kuhusu kiwango chake na kuelezea kuwa ni mtanzania."
 
Tunajipendekezajipendekeza, baadala ya kupambana na CCM ijenge mifumo itakayozarisha watu bora ndani ya Tanzania na kuijenga Tanzania tuko busy kupambana na asili za watu.

Hakuna Mhindi, Muarabu wala mburushi Mtanzania tuache kujidanganya.
Kabsa Mkuu!
 
Hapo ndo wakutane na kichaa sasa ๐Ÿ˜ƒ narudi home kimya kimya kama Ninja ๐Ÿฅท
Hata mimi aisee huwa sipendi unafki.
Kama kipindi kile Mwakinyo alivyoanza kung'aa baada ya kushinda pambano ulaya alivyokuwa anakwenda alikuwa yeye na kocha wake wa mtaani ila baada ya kushinda wakajifanya kuanza kumuongelea bungeni na wengine kuja kumpokea airport.
Kama ni mimi aisee nashukia Airport ya Kenya halafu napanda bus nakatiza Namanga narudi home kimyakimya nazima simu na kulala nawaacha wakeshe Airport bila mafanikio,Sitaki unafki hata kidogo
 
Kwani unadhani Wanaijeria wanajimwambafai na kina Leo Kokubo pamoja na Joel Chima Fujita, wale sasa hivi ni Wakorea sio Wanaijeria tena.
 
HUYO MAMA YAKE NI MBANTU AU NAYE ANA RANGI YA KIHINDI?TUANZIE HAPO
 
Utaitwa Mchochezi
 
Alielezq vizuri tu wakati wa uapisho wako, kuwa mama yake ni mtanzania, Baba ni mganda na yeye Alizaliwa marekani

Mama na baba yake walikutana masomoni India ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ณ, na namna baba na Mama yake walivyofika marekani wakitokea Uganda ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ

Itoshe kusema yeye mwenyewe anatambua asili yake kwa rangi na asili ya taifa ambalo wazazi wake wametokea ndio maana aliweza kuufahamisha ulimwengu na ukaelewa

Mihambo, ubalozi wa ujerumani Tanzania ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ulijivunia yeye na ukapost taarifa zake na kuungana na watanzania kusherekea mafanikio ya mihambo kwa pande zote mbili kwa kuwa Zina husika kwa namna moja au nyingine

Sunak kama sijakosea jina lake naye hivyo hivyo, wapo wengi sana na wanafurahia kuliko unavyochukizwa

Tunachofanya ni kufurahia kwa pamoja na kuwapa hamasa wengine waweze kukimbilia ndoto zao kwa kuwa Dunia ni uwanja mpana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ