Paternus Niyegira: Wananchi wanatakiwa kusimama bila uoga kuwajibisha Viongozi

Paternus Niyegira: Wananchi wanatakiwa kusimama bila uoga kuwajibisha Viongozi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mchambuzi wa masuala ya siasa, Paternus Niyegira, amesema kuwa wananchi ndio wenye mamlaka kuu ya kuwawajibisha viongozi kwa sababu wao ndio waliowapa mamlaka hayo kupitia mkataba wa kijamii na katiba. Akizungumza kwenye mahojiano na Crown Media Septemba 16, 2026, Niyegira amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kusimama kidete na kuzungumza kwa kauli moja isiyo na woga ili kulinda misingi mikuu ya haki, utu na amani waliyoijenga.

Aidha, Niyegira amebainisha kuwa tatizo kubwa kwa sasa linatokana na baadhi ya viongozi kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwatawala na kuwageuza wananchi kama wanavyotaka. Alieleza kuwa viongozi hao wanarejesha mfumo wa zamani wa kabla ya demokrasia, ambapo wenye nguvu na 'upanga' walitumia ubabe kuamua hatima ya maisha ya watu.

 
Back
Top Bottom