Pato la kila Mkoa: Dar es Salaam yazidi kuongoza ikifuatiwa na Mwanza, Njombe na Katavi zashika mkia

Tungesema kila mtu ajenge kwao, sijui hii pwani na dar pangekuwa na hali gani.....kwa kufunga ubuyu wa mia mia na kukaanga vitumbua tungeshuhudia nyumba za makuti zimetapakaa kila mahali.....
Hivi hujui bandari peke yake inaweza kuendesha uchumi wa nchi nzima?
 
MNAJUA mnakosea mnapojenga hoja jengeni kiuchumi si kwa kulinganisha majengo.angalieni vitu vinavyochangia kukua kwa uchumi kwa maana ya factors of economy.ukisema majengo yameshamiri bukoba ina majengo ya kutisha lkn iko hoi kiuchumi pia ruvuma wala haina majengo ya kutisha lkn kiuchumi iko katika top ten.
 
Njombe inakuwaje ya mwisho wakati kuna parachichi kule
 
Nimeishi Mbeya pia miaka minne,naijua vizuri sana Mwanza,usilinganishe Mbeya (kichuguu) na Mwanza (Mlima)
Ukiona mtu anatumia nguvu nyingi kutaka kutambulika ujue Hali yake ni mbaya..

Umekalia ooh nimeishi lini uliishi? Miaka uliyoishi Ndio sawa na Sasa? Hali ya Halisi ya Mwanza ni hii hapa 👇



 
No please. Mkoa wa Mwanza una watu karibia milioni sita, wewe inaonekana ukisikia Mwanza akili yote iko kwenye jiji la Mwanza tu.

Mwanza ni zaidi ya Nyamagana na Ilemera. Halafu kumbuka jamii ya wasukuma ndio inaongoza kwa kuzaana sana ktk Afrika Mashariki.
 
Njombe inakuwaje ya mwisho wakati kuna parachichi kule
Ya mwisho kuchangia GDP kwa sababu ni Mkoa mpya na ndio unajijenga saizi..

Kuwa wa mwisho kuchangia GDP haimaanishi ni WA Mwisho kwenye maendeleo,Hali halisi ni hii hapa 👇



 
GDP Per Capita sio kipimo sahihi cha kupima usitawi wa watu kiuchumi labda bara, nchi, mkoa au wilaya.

Ukichukulia Annual GDP ya nchi kama China utakuta ni ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Marekani lakini sasa rudi kwenye GDP Income Per Capita yao utakuta wanazidiwa na nchi nyingi tu.

Hivyo hicho sicho kipimo sahihi sana sana kinatumika kukibeba zaidi taifa huku wananchi walio wengi wakiwa hawanufaiki nacho.

It's a yardstick used mainly in political economy.
 
Umewaona wahaya tu[emoji12][emoji12]
Kuna wakati palifanyika ujanja/kosa/upotoshaji kwamba eti Dodoma ilikuwa inaongoza kimapato. Watu wengi walihoji usahihi wa taarifa ile. Kama sasa inakuja taarifa kwamba Dar Es Salaam bado iko juu kimapato , naona wameamua ukweli ufanye kazi kuliko porojo za makusudi
 
Takwimu za chatto ndo zlikua znafanya kazi
 
Yaani kwa akili yako unataka kutuaminisha Bukoba imejengeka kuliko kahama? Kahama mpaka kijijini majumba mazuri!
 
Acha kudanganya kahama Kijiji gani kunanyumba nzuri nyumba ziko mjini tu na kwa mazingira yenye mvuto na muonekano wa mji bukoba kuilinganisha na kahama ni kuikosea adabu bukoba linganisha na moshi pamoja na iringa kahama uzuri wake ni mzunguko wa fedha ila sio kwa muonekano wa mji
 
Mpaka atakapostaafu yule mama wa kichaga ndio nitaanza kuamini takwimu za hii bureau of statistics.
Wakati wa mwendakuzimu alikua anatoa data kumfurahisha mteuaji
 
Acha kudanganya watu wewe. Tumezunguka hii nchi. Huwezi kamwe kuishushia Moshi heshima kwa kuilinganisha na Bukoba. Nina wasiwasi hujafika Moshi.
Naongelea Moshi iliyoko Kilimanjaro. LABDA wewe unaongelea Moshi nyingine huko usweken kwenu.
 
Kanda ya ziwa inabebwa ma migodi.
zaidi ipo imepakana na karibu nchi tajiri EA......na pia jirani mnoo na Nparks zenye hela...tatu watu wake ni hapa kazikazi tu..wana mifugo weeengi.ngombe mbuzi.kondoo punda nk. Ziwa mwanana kwa lishe!
usafiri wa aina zooote upo pale...reli.barabara nzuri.anga ndo usiseme.mikokoteni ya punda farasi.barafu vipo....ungo nk!

Ndo mkoa pekee ulio ruhusu nyungo za kichawi kufanya biashara za kubeba abiria wawahi kazini kuzalisha mali ...siri kubwa iko hapo....wkt nyie mnaabudu yesu mzungu wasukuma walishaiona hiyo kuwa ni changa la macho....so wakakomaa na yao ya kienyeji...ndo leo wako ivo tulieni....wakaenda mbali zaidi siku hizi hawatumii ungo tena... bali unga wa kijani ukifumba na kufumbua uko kazini kwako unafanya kazi kula ni huko huko!! Mazao wanauziana mkileta porojo miiing ngoma inahama wanauza nchi jirani..kwa pesa za kigeni kwa usafiri wa ungo wamebeba tani nyingi sana.....ngoma inaenda mpaka Somalia hiyo. Km mkiweza nawashauri hamieni Mwnza wote. Kikubwa mtunze siri hii.
 
Kuna mikoa takriban 10 ambazo uwepo wao ni wa kisiasa tu na ni mzigo kwa taifa. Kimsingi hii nchi haina sababu ya kuwa na mikoa mingi kiasi hicho.

Mikoa hiyo ilianzishwa kwa sababu za kisiasa huku ccm wakifikiri ingefanya wapate sifa kutoka kwa wananchi ambao wengi wao hawajui hasara ya nchi maskini kama hii kuwa na mikoa/wilaya nyingi na hawajui kwamba ni mzigo kwao.

Katika utaratibu huu unakuta mikoa miwili tu pato lao ni theluthi moja ya pato lote la nchi huku mikoa mingi tu ikiwa ni wasindikizaji na misalaba kwa mingine.
 
Mkoa wa simiyu umechukua sehemu ndogo sana Mwanza, sehemu hiyo ndogo haina impact kwa Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…