Pato la kila Mkoa: Dar es Salaam yazidi kuongoza ikifuatiwa na Mwanza, Njombe na Katavi zashika mkia

Pato la kila Mkoa: Dar es Salaam yazidi kuongoza ikifuatiwa na Mwanza, Njombe na Katavi zashika mkia

Tungesema kila mtu ajenge kwao, sijui hii pwani na dar pangekuwa na hali gani.....kwa kufunga ubuyu wa mia mia na kukaanga vitumbua tungeshuhudia nyumba za makuti zimetapakaa kila mahali.....
Hivi hujui bandari peke yake inaweza kuendesha uchumi wa nchi nzima?
 
**** watu roho inawauma sana tena nataka niwaambie mimi niko dar! Bila bandari Dar kwa mwanza wanapambana tu! Maana ukiangalia nyumba mitaani za makazi mtaa mingi ya mwanza ina nyumba kali kuzidi dar! Maana makazi mengi dar ni ya zamani isipokuwa mitaa ya kinyerezi mbezi,tegeta na kigamboni,
MNAJUA mnakosea mnapojenga hoja jengeni kiuchumi si kwa kulinganisha majengo.angalieni vitu vinavyochangia kukua kwa uchumi kwa maana ya factors of economy.ukisema majengo yameshamiri bukoba ina majengo ya kutisha lkn iko hoi kiuchumi pia ruvuma wala haina majengo ya kutisha lkn kiuchumi iko katika top ten.
 
Ofisi ya taifa ya takwimu imetoa pato la kila mkoa nchini Tanzania, mkoa wa Dar es salaam wazidi kuongoza ukifuatiwa na Mwanza.

Mikoa ya Katavi na Njombe imeshika mkia kwa kua na pato dogo sana ukilinganisha na mikoa mingine.

Kwenye kumi bora kanda ya ziwa imeingiza mikoa 3, Mwanza, Shinyanga na Geita kwa jumla ya Trilioni 25 sawa na mkoa wa Dar es Salaam.

Kanda ya kaskazini, pato la mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ndio inafikia pato la mkoa wa Mwanza. Utajiri wa Arusha, Kilimanjaro na Tanga ni sawa na utajiri wa Mwanza na Shinyanga.

Kwa Takwimu za NBS, ukitoa Dar, kanda inayofuatia kwa utajiri ni anda ya ziwa, ikifuatiwa na Kaskazini huku Kusini kwa Lindi, Mtwara na jirani yao Pwani wakishika mkia.

Kanda ya nyanda za Juu kusini Mbeya inawabeba ila imezungukwa na mikoa choka mbaya kama Katavi na Njombe hivyo kuchangia kanda hiyo kuonekana ni choka mbaya mbavu za mbwa.

Watu wa Mara tukomae tuiondoe kilimanjaro ama Ruvuma hapo juu tuingie top 10.

====

Utajiri wa mikoa kwa kuangalia pato la mkoa husika.
1. Dar es Salaam Trilion 25.2
2. Mwanza Trilioni 10.95
3. Mbeya Trilioni 8.3
4. Shinyanga Trilioni 7.5
5. Morogoro Trilioni 7.1
6. Tanga Trilioni 6.96
7. Arusha T6.94
8. Geita T6.66
9. Kilimanjaro T6.62
10. Ruvuma Trilioni 5.6
View attachment 1969823
Njombe inakuwaje ya mwisho wakati kuna parachichi kule
 
Nimeishi Mbeya pia miaka minne,naijua vizuri sana Mwanza,usilinganishe Mbeya (kichuguu) na Mwanza (Mlima)
Ukiona mtu anatumia nguvu nyingi kutaka kutambulika ujue Hali yake ni mbaya..

Umekalia ooh nimeishi lini uliishi? Miaka uliyoishi Ndio sawa na Sasa? Hali ya Halisi ya Mwanza ni hii hapa 👇

Screenshot_20211018-114259.png


Screenshot_20211018-120105.png
 
Hizi data hazitoi picha kamili. Dar ina watu milioni sita. Mwanza ina watu milioni mbili. Ukigawa kwa mtu mmoja mmoja, Dar inaweza kuwa na masikini wengi kuliko Njombe na Katavi.
===========
NB: Nimefanya kwick maths. Dar inascore 4 point something wakati Katavi inascore 2.8.
By average, an average Dar resident is 1.5 richer than Katavi resident.
No please. Mkoa wa Mwanza una watu karibia milioni sita, wewe inaonekana ukisikia Mwanza akili yote iko kwenye jiji la Mwanza tu.

Mwanza ni zaidi ya Nyamagana na Ilemera. Halafu kumbuka jamii ya wasukuma ndio inaongoza kwa kuzaana sana ktk Afrika Mashariki.
 
Njombe inakuwaje ya mwisho wakati kuna parachichi kule
Ya mwisho kuchangia GDP kwa sababu ni Mkoa mpya na ndio unajijenga saizi..

Kuwa wa mwisho kuchangia GDP haimaanishi ni WA Mwisho kwenye maendeleo,Hali halisi ni hii hapa 👇

Screenshot_20211012-195233.png


Screenshot_20211018-120105.png
 
Takwimu hizo zinatafsiriwa kwa namna nyingi. Ukitaka kujua hali halisi pima kwa per capita. Population ya mkoa lazima izingatiwe sio tu namba zilizo andikwa hapo. Jaribuni kugawa hiyo thamani ya utajiri wa idadi ya watu wake utapata sura tofauti kabisa.
GDP Per Capita sio kipimo sahihi cha kupima usitawi wa watu kiuchumi labda bara, nchi, mkoa au wilaya.

Ukichukulia Annual GDP ya nchi kama China utakuta ni ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Marekani lakini sasa rudi kwenye GDP Income Per Capita yao utakuta wanazidiwa na nchi nyingi tu.

Hivyo hicho sicho kipimo sahihi sana sana kinatumika kukibeba zaidi taifa huku wananchi walio wengi wakiwa hawanufaiki nacho.

It's a yardstick used mainly in political economy.
 
Umewaona wahaya tu[emoji12][emoji12]
Kuna wakati palifanyika ujanja/kosa/upotoshaji kwamba eti Dodoma ilikuwa inaongoza kimapato. Watu wengi walihoji usahihi wa taarifa ile. Kama sasa inakuja taarifa kwamba Dar Es Salaam bado iko juu kimapato , naona wameamua ukweli ufanye kazi kuliko porojo za makusudi
 
Kuna wakati palifanyika ujanja/kosa/upotoshaji kwamba eti Dodoma ilikuwa inaongoza kimapato. Watu wengi walihoji usahihi wa taarifa ile. Kama sasa inakuja taarifa kwamba Dar Es Salaam bado iko juu kimapato , naona wameamua ukweli ufanye kazi kuliko porojo za makusudi
Takwimu za chatto ndo zlikua znafanya kazi
 
Hayo majumba mazuri vijijini uhayani yanachangia pato la taifa kiasi gani ishu ni GDP sio makazi bora hao wasukuma ni wachuuzi miamala wanayofanya kwa siku tu ni mikubwa huko kwenye machimbo ya dhahabu mfano mji wa bukoba umejengeka kuliko kahama lakini pato la mji wa kahama na mzunguko wa fedha kahama inazidi bukoba japokuwa bukoba imejengeka kuliko kahama ndio ujue majengo hayaongezi pato la taifa halafu hata hayo majengo huko bukoba vijijini hamjauza ndizi ndio mkajenga ni pesa mmepata dar na mikoa mingine mkajenga nyumbani sehemu yenu ya kuzikiwa ili msije kuchekwa ila msukuma akifa anazikwa popote sio lazima kupelekwa kwao
Yaani kwa akili yako unataka kutuaminisha Bukoba imejengeka kuliko kahama? Kahama mpaka kijijini majumba mazuri!
 
Acha kudanganya kahama Kijiji gani kunanyumba nzuri nyumba ziko mjini tu na kwa mazingira yenye mvuto na muonekano wa mji bukoba kuilinganisha na kahama ni kuikosea adabu bukoba linganisha na moshi pamoja na iringa kahama uzuri wake ni mzunguko wa fedha ila sio kwa muonekano wa mji
 
Mpaka atakapostaafu yule mama wa kichaga ndio nitaanza kuamini takwimu za hii bureau of statistics.
Wakati wa mwendakuzimu alikua anatoa data kumfurahisha mteuaji
 
Acha kudanganya kahama Kijiji gani kunanyumba nzuri nyumba ziko mjini tu na kwa mazingira yenye mvuto na muonekano wa mji bukoba kuilinganisha na kahama ni kuikosea adabu bukoba linganisha na moshi pamoja na iringa kahama uzuri wake ni mzunguko wa fedha ila sio kwa muonekano wa mji
Acha kudanganya watu wewe. Tumezunguka hii nchi. Huwezi kamwe kuishushia Moshi heshima kwa kuilinganisha na Bukoba. Nina wasiwasi hujafika Moshi.
Naongelea Moshi iliyoko Kilimanjaro. LABDA wewe unaongelea Moshi nyingine huko usweken kwenu.
 
Kanda ya ziwa inabebwa ma migodi.
zaidi ipo imepakana na karibu nchi tajiri EA......na pia jirani mnoo na Nparks zenye hela...tatu watu wake ni hapa kazikazi tu..wana mifugo weeengi.ngombe mbuzi.kondoo punda nk. Ziwa mwanana kwa lishe!
usafiri wa aina zooote upo pale...reli.barabara nzuri.anga ndo usiseme.mikokoteni ya punda farasi.barafu vipo....ungo nk!

Ndo mkoa pekee ulio ruhusu nyungo za kichawi kufanya biashara za kubeba abiria wawahi kazini kuzalisha mali ...siri kubwa iko hapo....wkt nyie mnaabudu yesu mzungu wasukuma walishaiona hiyo kuwa ni changa la macho....so wakakomaa na yao ya kienyeji...ndo leo wako ivo tulieni....wakaenda mbali zaidi siku hizi hawatumii ungo tena... bali unga wa kijani ukifumba na kufumbua uko kazini kwako unafanya kazi kula ni huko huko!! Mazao wanauziana mkileta porojo miiing ngoma inahama wanauza nchi jirani..kwa pesa za kigeni kwa usafiri wa ungo wamebeba tani nyingi sana.....ngoma inaenda mpaka Somalia hiyo. Km mkiweza nawashauri hamieni Mwnza wote. Kikubwa mtunze siri hii.
 
Kuna mikoa takriban 10 ambazo uwepo wao ni wa kisiasa tu na ni mzigo kwa taifa. Kimsingi hii nchi haina sababu ya kuwa na mikoa mingi kiasi hicho.

Mikoa hiyo ilianzishwa kwa sababu za kisiasa huku ccm wakifikiri ingefanya wapate sifa kutoka kwa wananchi ambao wengi wao hawajui hasara ya nchi maskini kama hii kuwa na mikoa/wilaya nyingi na hawajui kwamba ni mzigo kwao.

Katika utaratibu huu unakuta mikoa miwili tu pato lao ni theluthi moja ya pato lote la nchi huku mikoa mingi tu ikiwa ni wasindikizaji na misalaba kwa mingine.
 
Tunataka mapato ya per Capita income,GDP haitakusaidia Sana mkuu ni kujifariji.

GDP yenyewe ya huko Kanda ya Ziwa ni madini ya dhahabu amvayo huishia Kwenye makampuni, serikali na kiduchu ndio huenda kwa watu wachache..

Huko Njombe ambako unadai WA Mwisho ukileta GDP Per Capita income inashindana na Dar tuu.

Mwisho Takwimu za Shinyanga na Mwanza zinahusisha Mkoa was Simiyu kiasi kwamba Kama Mbeya isingegawanywa kuunda Songwe basi ingekuwa no.2 nyuma ya Dar na huko hakuna Migodi huko ndiko Kuna watu waliostawi Sasa.

Tunataka Takwimu independent za Simiyu,tuone aibu ya baadhi ya mikoa hapa.
Mkoa wa simiyu umechukua sehemu ndogo sana Mwanza, sehemu hiyo ndogo haina impact kwa Mwanza
 
Back
Top Bottom