Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Patrick Nyembera ni mmoja kati ya wachambuzi wa michezo nchini ambaye anafanya kazi hiyo Azam Media. Na mara zote amekuwa ni Commentator wa masumbwi ambayo kwa Azam wanaita Vitasa. Katika mapambano mengi huwa wanakuwa na watu wengine kwenye kuelezea michezo hiyo na kuwapa radha watazamaji.
Mmoja wa watu ambao hivi karibuni wamekuwa wakijikita zaidi kwenye uchambuzi wa ndondi ni Aidan Mlimila, ambaye naye yupo Azam na mara zote amekuwa akielezea ndondi kwa namna ambavyo ndondi inapaswa kuwa. Yaani Aidan ni dizaini ya Kashasha alivyokuwa kwenye soka.
Katika pambano la Mei 31 ambapo Mwakinyo alikuwa main card kuna maneno ambayo Patrick aliyazungumza dhidi ya Aidan nikaona anachukia ufahamu wa Aidan kwenye ndondi. Kwa mliorekodi mapambano ya utangulizi ya siku hiyo, kaangalieni pambano la Kaoneka round ya nne, Patrick amemuita Aidan "Google".
Amemuita "Google" Kumaanisha kuwa Aidan anaisoma sana ngumi. Hata hivyo kwenye professionalism hauwezi kumuita mtu kwa jina lisilo lake. Jina lolote lisilo la mtu linamaanisha kuna kitu hakiko sawa kwa anayetumia jina hilo. Tena, jina hilo lilifuata baada ya kumlalamikia kuwa anasoma sana ngumi.
Nilisikia sauti ya Aidan ikiitikia kwa shida jina lile, na kujibu alichoulizwa ila kiukweli kitaaluma haiko sawa. Kwa wenzetu nje mtu akikutajia jina lake na ukaamua kumuita jina unalotaka wewe ni serious offence, ni disrespect kubwa inayostahili hatua za kinidhamu.
Nadhani Patrick hajazuiwa kuisoma ngumi, so badala ya kuchukia wanaoisoma ngumi, ni vyema na yeye asome. Pole sana Aidan kwa name callning uliyofanyiwa.
Nayeyuka huku nikiweweseka kiwendawazimu, langu jina ni Analogia Malenga.