Zakumi,
Unachozungumzia ni Ethics au miiko ya uongozi katika Azimio la Arusha. Miiko ya uongozi ni sehemu tu ya Azimio la Arusha
..
Exactly!.. Azimio la Arusha lilikuwa na mabaya yake ambayo ndiyo yalitakiwa kurekebishwa na Azimio la Zanzibar lakini badala yake kilichobadilishwa ni Ethics za Uongozi.. Kumbuka kwamba tuliacha Siasa za Ujamaa July 1984 siku mwalimu alipotangaza kushindwa kwa Ujamaa hivyo kuacha milango wazi ya Biashara..
Toka siku hiyo policy ya open market ilikutumika na mabaya tuliyoyajua sisi ndio ulikuwa mwisho wake...Mwaka 1992 - miaka minane baadaye (kama sikosei) ndipo Mwinyi alipotangaza Azimio la Zanzibar hiyo - RUKSA..na hakuna jambo lolote lililokuwa geni ktk Uchumi isipokuwa nafasi ya viongozi wetu kujihusisha na biashara. Kwa hiyo Azimio la Zanzibar lilikuja kuvunja miiko ya Uongozi. Uongozi wa Mwinyi unatia Kichefuchefu kiuchumi toka hilo Azimio lilipotangazwa, machafu yote utayakuta baada ya Azimio hilo..
Hivyo mkuu, unapolipigia debe Azimio la Zanzibar ni sawa na kupingana na maneno ya mwalimu uliyoyaandika hapo juu..Hakuna kati yetu anayesema Azimio la Arusdha lilikuwa bomba kichizi isipokuwa pale tunapogusia swala la Uongozi bora na ndilo tatizo kubwa la Tanzania. Mara nyingi tumeshindwa kutafuta kiini cha matatizo yetu badala yake tuna laumu watu na sio policy iliyoshinikiza.
Ukitazama ukumbi wa siasa utaona karibu mada zote zinahusiana na
Uongozi bora na kwa bahati mbaya tumeshindwa kuelewa kwamba yote haya yametokana na kuvunjika kwa hiyo miiko ya Uongozi. Ni hilo Azimio la Zanzibar lilompa uwezo Mkapa, Mramba, Yona, Karume, na wengine wote kufanya waliyoyafanya kwa sababu ilikuwa ruksa kufanya biashara ama kwa lugha inayoendana na Uongozi nitasema KUJITAJIRISHA...
Hakuna ethics za Uongozi ambazo zinaambatana na sheria zinazowapa uhuru Viongozi kufanya biashara. Ni sawa na Padre unayemruhusu kufunga ndoa lakini anakatazwa kutongoza mwanamke au mwanafunzi wake... unafikiri huyo mke atampata vipi?..
Ethics za Uongozi ni lazima ziambatane na sheria zinazokataza hata kukaribia kufanya maovu, Wala Takribun - waarabu wanasema..Hata katika mashirika ya kawaida huwezi kumwona CEO wa shirika moja la Simu akiruhusiwa kufungua kampuni yake ndogo ya simu na ukategemea hataifanya kazi ya shirika hilo vizuri..Acha hilo huku Ulaya kuna mashirika hata ndugu yako huruhusiwi kuwajiri ukisha kuwa na wadhifa fulani...
Ukimwacha Lowassa anunue hisa ya kumiliki Celtel unategemea atafanya nini zaidi ya kuhakikisha anaua Ushindani, anaweka masharti rahisi na pengine kodi ndogo ktk shirika hilo..
Hata ukitazama matatizo ya nyumba na viwanda.. Kinachotuumiza wengi sio ununuzi wa viwanda hivyo ama fedha njugu walizolipa isipokuwa ni ile ruksa ya hao viongozi kujipanga na kuzichukua.. hakuna mtu ambaye atajipangia bei kubwa ama masharti magumu lakini kama hawa viongozi wangekuwa hawaruhusiwi ungeona tofauti ya bei na tender za Ukweli zikitumika..UWAZI ungekuwepo kwani hakuna mtu angetaka kuonekana kauza kitu kwa hasara...Mkapa kaichukua Kiwira kwa sababu alikuwa rais hakuna sababu nyingine..Ni hivyo hivyo kwa viongozi wote wamegawana mali zetu chini ya uhuru waliopewa na sasa hivi tumeganda hatujui la kufanya.. Kisheria walilipa thamani ya viwanda hivyo hata kama ilichorwa, lakini walilipa hawakuiba wala kunyang'anya, hivyo sio wao waliovunja sheria isipokuwa sheria zenyewe ndizo zilikuwa mbovu.. tazama maswala ya madini hata Waziri mkuu wa Canada alishangaa kusikia tumefungiwa kanyaboya na Barricks kiasi kile, na kashidnwa kutusaidia kwa sababu tuliingia mkataba kisheria.. Mkapa kaondoka na asilimia zake 10 ambazo huweiz kuziona zinaingia direct ktk sahani lake...