Paukwa... Pakawa!

Paukwa... Pakawa!

FMES,
Kuwa mwanafunzi wa mtu haina maana kuwa utaiga au kufuata aliyokufundisha. Binadamu ndivyo tulivyo. Mwinyi alijiita kichuguu kwa kulinganishwa na Mwalimu lakini akawa wa kwanza kulizika azimio la Arusha na kutuletea azimio la Zanzibar. Na juzi tu katwambia kuwa azimio la Arusha lilikuwa ndoto. Huyu wa sasa anasema ukizungumzia azimio la arusha leo watakuona chizi. Ni kweli kulikuwepo na rushwa wakati wa utawala wa Mwalimu lakini kulikuwa pia na hofu ya kuogopa kugunduliwa na authorities na subsequent consequences. Lakini wakati wa Mwinyi lilikuwa jambo la fahari kuonekana unakula na wakubwa, wafanyibiashara etc. etc. Na huyu wa awamu ya tatu ndiyo kabisa akatumbukia kwenye limbwi la uozo wa rushwa na matokeo yake ndiyo hayo ya akina Zombe, Mahita na kukumbatiwa kwa mafisadi.

Jasusi:

Nostalgia zingine itabidi tuziache. Azimio la Arusha lilikuwa katika misingi ya chama kimoja na kwenye dira za kijamaa. Hile ni miongozo ya wanaTanu na baadaye CCM.

Sasa hivi nchi hiko katika mfumo wa vyama vingi. Kila chama kina siasa zake. Hivyo kama kuna hoja za ethics za uongozi basi hoja hizo zilenge mazingira tuliyo nayo.

Kama kuna mfanyabiashara anayetaka kuleta mafanikio yake katika endeshaji wa serikali kwanini asipewe ruhusa kuwa kiongozi?

Sioni mtu wa CHADEMA alidai kuwa ni mfuata wa siasa za mlengo wa kulia kukumbatia Azimio la Arusha.
 
hatuna haja ya maelezo marefu, mfano mshaonyeshwa huko thailand.....!!
 
Zakumi,
Mkuu Azimio la Arusha lilikuwa kweli chini ya chama kimoja lakini hata hilo la Zanzibar.. maamuzi ya Azimio hilo yamependekezwa na kupitishwa na viongozi wale wale wa chama kimoja kabla hatujaunda vyama vingi..Kumbuka kuwa Miwnyi ndiye alikuwa rais wakati linapitishwa.

Pili, Azimio la Zanzibar halipotoshi ama kupingana na Azimio la Arusha kulingana na maelezo ya mwinyi, kama unakumbuka Mwinyi alisema haya alipokuwa akiliwakilisha isipokuwa ni MAREKEBISHO toka Azimio la Arusha ktk kipengele cha viongozi. Ni sawa na Agano jpya la Yesu kutopingana na lile la kale isipokuwa ni marekebisho ya baadhi ya Aya na nyongeza za yale yaliyokuwa yamekosekana mwanzoni ili waumini wapate kufanya ibada kwa ufasaha zaidi.

Mkuu ni muhimu sana uelewe tunapozungumzia viongozi ujue ni viongozi wapi tunaowasema...Hawa ni wale waliochaguliwa kushika madaraka ktk serikali inayoongoza - Toka rais mwenyewe hadi watu wote atakao WATEUA kushika nyadhifa ndani ya serikali yake, ndio watu wasioruhusiwa kuwa na biashara pembeni kwani majukumu waliyopewa yanawahitaji muda wote 24/7...
Azimio la Zanzibar liliwapa uhuru watu hawa kufanya biashara hivyo kuleta conflict of interest... na matokeo yake ndio haya ya kina Yona na Mramba, bado unatetea wafanyabiashara kuwa viongozi mkuu!

Hii ni Principal ya uongozi ktk serikali zote iwe ya Kibepari au ya Kisoshalist!... kwa hiyo usije danganyika kuwa Azimio la Zanzibar ni muhimu ktk kuendesha serikali ndani ya Ubepari..
Na ndio maana Kikwete ameondoa Azimio hilo ktk Uongozi wa awamu yake.. Ni moja ya sifa kubwa ninazompa hadi sasa hivi ingawa bado uetekelezaji wake haujakaa sawa.
 
Sikuwa na nia ya kulitetea Azimio la Zanzibar. Lakini wakati Azimio hilo linapita. Mkapa alikuwa na Nyumba Ukonga. Na wakati anagombea urais bado alikuwa ana nyumba hiyo hiyo ya Ukonga na Account yenye Shilling million 5 kama sikosehi.

Kwa mujibu wa Azimio la Zanzibar angeweza kupangisha nyumba yake ya mbavu za mbwa iliyopo Ukonga na kwenda kuishi Ikulu. Kwa kuipangisha nyumba yake angeweza kumsaidia mtanzania mwenzake. Hilo ndilo Azimio la Zanzibar.

Al Gore akiwa makamu wa rais aliishi kwenye Maskani ya makamu wa rais na nyumba yake ya DC alipangisha. Na mtu aliyepangishwa alikuwa hata kodi hataki kulipa.

Azimio la Zanzibar alikuruhusu mtu kuingia Ikulu na kutoka kama mfanya biashara mwenye kumiliki mgodi wa mawe kwa kweli huyo sio mfanyabiashara ni mwivi.
 
Kwa mujibu wa Azimio la Zanzibar angeweza kupangisha nyumba yake ya mbavu za mbwa iliyopo Ukonga na kwenda kuishi Ikulu. Kwa kuipangisha nyumba yake angeweza kumsaidia mtanzania mwenzake. Hilo ndilo Azimio la Zanzibar.

Hata Azimio la Arusha liliruhusu viongozi kuwa na hisa japo kwa makampuni mawili, hivyo kumiliki mali kwa kiasi na si ulafi ilikuwa ni ruksa.

Sasa Azimio la Zanzibar likasema nyumba moja ya kupanga haitoshi, shurti Kiongozi awe na nyumba 7 kama za babu yake Nyani (Yohana wa Makopo)! Ndipo ulafi, uroho na umelo ukaanza!
 
Rev Kishoka:

Azimio la Zanzibar alikufanya watu wawe walafi. Kwa namna moja au nyingine limefanya watanzania wenye fani mbalimbali kujiunga na siasa na kuweza kutumikia taifa lao.

Ni miaka ya hivi karibuni tumeona waProfessor na wataalamu wengi wanajingiza kwenye siasa.

Miaka ya zamani siasa ilikuwa ni ya waalimu au maafisa elimu tu.

Suala linalokuja hapa ni ethics au miiko ya uongozi. Na ethics tunazo-miss hapa sio za uongozi tu bali ethics za kazi.
 
Rev.Kishoka said:
Hata Azimio la Arusha liliruhusu viongozi kuwa na hisa japo kwa makampuni mawili, hivyo kumiliki mali kwa kiasi na si ulafi ilikuwa ni ruksa.

Kishoka,

..Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili, na kuwa na hisa ktk makampuni ya kibepari.

..kuna watumishi wa serikali walifunga miradi yao ya kufuga kuku wa biashara ili kuzingatia miiko ya uongozi ya Azimio la Arusha.

..cha msingi hapa ni kuiboresha sheria ya maadili ya viongozi na watumishi wa serikali. hata sheria zetu za makosa ya jinai zinatosha kukabiliana na uhalifu uliotokea na unaoendelea.

NB:

..Azimio la Arusha na siasa za Ujamaa lilisababisha nidhamu ya kazi na productivity kushuka kwa kiwango cha kutisha.
 
There we go. Rafiki yangu Kishoka analizungumza Azimio bila kulisoma. Sheria zetu za sasa ambazo zinampeleka mwizi wa kuku jela kwanini hazitumiki kumpeleka mwizi wa pesa kwenye benki ndani?
 
Kishoka,

..Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili, na kuwa na hisa ktk makampuni ya kibepari.

..kuna watumishi wa serikali walifunga miradi yao ya kufuga kuku wa biashara ili kuzingatia miiko ya uongozi ya Azimio la Arusha.

..cha msingi hapa ni kuiboresha sheria ya maadili ya viongozi na watumishi wa serikali. hata sheria zetu za makosa ya jinai zinatosha kukabiliana na uhalifu uliotokea na unaoendelea.

NB:

..Azimio la Arusha na siasa za Ujamaa lilisababisha nidhamu ya kazi na productivity kushuka kwa kiwango cha kutisha.

Nakiri nilinukuu vibaya Azimio. Viongozi ndiyo waliopewa miiko na si wananchi wa kawaida. Sababu ya Viongozi kuwekewa masharti magumu ilikuw ani ili kuondokana na Viongozi kutumia vibaya madaraka yao na kujipatia ziada kwa misuli ya vyeo vyao.

Azimio la Zanzibar, badala ya kuweka japo vipingamizi fulani ili kuratibu huu mwanya wa kujipatia, limefungulia mlango na kila mtu sasa anakuwa nyang'au na kula kupita kiasi!
 
Tatizo la manyang'au ni pale mzoga unapokwisha, wanaanza kutafunana wao kwa wao. Naona ndio wameanza na huyo ole wake atakayepona, tunamsubiri - sisi wananchi tuliochoka na ulafi wao - kwa ari na shauku. Twendeleze libeneke.
 
Kuna kauli moja aliwahi kuitoa Rais Mwinyi a.k.a Ruksa, katika hotuba aliyoitoa Tanga nafikiri, nilikuwa mdogo nikisikiliza kwenye radio, alisema "hata hatua elfu moja zilianza na hatua moja!"
Nakubaliana na wewe Rev. Kishoka lakini nawasihi watanzainia katika hili tusiongozwe na jazba, kwani haya yanayofanyika sasahivi ni ushindi mkubwa kwa wavuja jasho (hata kama ni kiini macho), na inaashiria kulegea kwa kuta za ukiritimba na ufisadi uliojengeka kwa miaka mingi sana.
Akiongea na baba Maaskofu wa Tanzani kuhusu ujio wa vyama vingi mjini dodoma(ilikuwa baada ya maaskofu kusignishwa na Askofu Mtikila document fulani huko dodoma), Mwalimu Nyerere alitoa mfano "Nisawa na kukata mti mkubwa sana ambao utaangukia barabarani, wakati hujafanya maandalizi ya kuutoa hapo ukishaanguka"
Mimi nadhani huu ni mwanzo haiwezani kutoka zero mpaka kumshitaki rais, wakati hapo nyuma hata kumchora rais kwenye gazeti ilikuwa issue, waacheni tu watoane kafara kwanza. Wakimaliza moja tutadai lapili hapo nadhani tunafika hatua elfu moja.
Hakuna mtu alitegemea kuwa Kikwete angeweza kuwa na kifua cha kuyakabili haya anayopambana nayo sasa, wengi tulijuwa angeendelea kuwa 'BOYZ11MEN' lakini..........Nilipokuwa safarini kwenda Mwanza via Nairobi, niliwahi kuona maandishi makubwa ukutani " KUNA NURU GIZANI"
nb. hizo nukuu siyo rasmi nimejaribu kuzikumbuka kutoka kichwani, aliyenazo arekebishe.
 
Nakiri nilinukuu vibaya Azimio. Viongozi ndiyo waliopewa miiko na si wananchi wa kawaida. Sababu ya Viongozi kuwekewa masharti magumu ilikuw ani ili kuondokana na Viongozi kutumia vibaya madaraka yao na kujipatia ziada kwa misuli ya vyeo vyao.

Azimio la Zanzibar, badala ya kuweka japo vipingamizi fulani ili kuratibu huu mwanya wa kujipatia, limefungulia mlango na kila mtu sasa anakuwa nyang'au na kula kupita kiasi!

Rev Kishoka:

Kwani sheria za nchi zinaruhusu wizi. Azimio la Zanzibar alipo juu ya sheria za nchi.
 
Tatizo la manyang'au ni pale mzoga unapokwisha, wanaanza kutafunana wao kwa wao. Naona ndio wameanza na huyo ole wake atakayepona, tunamsubiri - sisi wananchi tuliochoka na ulafi wao - kwa ari na shauku. Twendeleze libeneke.

Na Ukweli huu ni historical. Sio mara ya kwanza au ya mwisho kwa kanuni hii kujitokeza na kuonekana wazi hadharani.

Ungetegemea Mafisadi na wala nyma za watu wajifuze kuwa finaly it goes back on feeding on themselves....hainaga mwisho!!

Ambayo hii inatoa mwanya mzuri kwa waliooenewa na kunyanyaswa muda mrefu kutake Charge.

We should therefore be in startegic postion na kuwamalizia mbali!
 
Zakumi,
Mkuu ebu kasisikilize upya Hotuba ya Mwinyi...naona kama unapotosha!
Ni kweli Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili na bado mimi naunga mkono kabisa jambo hilo.. Kununua hisa ktk mashirika yaliyopo ktk soko letu hiyo ruksa kwa sababu hawana control ya market lakini sio hisa Vodaphone ama mishahara nje ya kazi aliyopewa unless mnayo tafsiri tofauti ya mshahara, ambayo nielewavyo mimi ni malipo ya mwezi kwa kazi uliyoifanya...
Halafu swala la Kupangisha nyumba ni bomu kabisa..haiwezekani kila mtu apangishe nyumba lazia kuwepo na utaratibu wa kupangisha ili kodi za mapato ya kupangishwa ziweze kukusanywa... Serikali inatakiwa kuweka maazimio yenye manufaa kwa Taifa na sio kutazama mtu mmoja mmoja, hapa nikiwa na maana kuwa unaporuhusu kupangisha nyumba lengo lkake linakuwa kutunisha mfuko wa serikali ktk pato la kodi za upangishaji, hivyo ni lazima iwekwe taratibu ambazo zitahakikisha kwamba wapangishaji wanafuata masharti ya kupangisha, sio swala la kumsaidia mtu mahala pa kuishi..
Kifupi mkuu wangu Azimio la Zanzibar ni bomu, viongozi hawatakiwi kabisa kujihusisha na biashara wala nyumba za kupangisha kutokana na madaraka waliyopewa..Ni ktk kutumia madaraka hayo ndio tunaona wakijenga hoja za mji mpya Kigamboni ambako wao wenyewe kwa kutumia madaraka yao hupewa nafasi ya kwanza kuchukua viwanja hivyo kujenga hizo nyumba za kupangisha...
Kisha hata siku moja tusifikirie kwamba kiongozi anaweza kuvua joho lake la uongozi kufuata utaratibu ambao unamweka yeye sawa na raia wa kawaida.. Hata siku moja hawezi kupanga msitari kupanda daladala mkuu wangu usijechanganya vitu hivi na ukweli unasimama peke yake...
Tunawalipa kodi zetu, mishahara mikubwa, magari majumba na kadhalika kuliko hata viongozi wa nchi za Ulaya tena hata baada ya kustaafu bado wanapokea ruzuku kubwa kuliko daktari wa Muhimbili, hivyo hakuna sababu kabisa ya viongozi hawa kujihusisha na biashara...
 
Zakumi,
Mkuu ebu kasisikilize upya Hotuba ya Mwinyi...naona kama unapotosha!
Ni kweli Azimio la Arusha lilikataza viongozi kuwa na mishahara miwili na bado mimi naunga mkono kabisa jambo hilo.. Hisa ktk mashirika ruksa lakini sio mishahara unless mnayo tafsiri tofauti ya mshahara, ambayo nielewavyo mimi ni malipo ya mwezi kwa kazi uliyoifanya...
Halafu swala la Kupangisha nyumba ni bomu kabisa..haiwezekani kila mtu apangishe nyumba lazia kuwepo na utaratibu wa kupangisha ili kodi za mapato ya kupangishwa ziweze kukusanywa... Serikali inatakiwa kuweka maazimio yenye manufaa kwa Taifa na sio kutazama mtu mmoja mmoja, hapa nikiwa na maana kuwa unaporuhusu kupangisha nyumba lengo lkake linakuwa kutunisha mfuko wa serikali ktk pato la kodi za upangishaji, hivyo ni lazima iwekwe taratibu ambazo zitahakikisha kwamba wapangishaji wanafuata masharti ya kupangisha, sio swala la kumsaidia mtu mahala pa kuishi..
Kifupi mkuu wangu Azimioa la zanzibar ni bomu, viongozi hawatakiwi kabisa kujihusisha na biashara wala nyumba za kupangisha kutokana na madaraka waliyopewa..Ni ktk kutumia madaraka hayo ndio tunaona wakijenga hoja za mji mpya Kigamboni ambako wao wenyewe kwa kutumia madaraka yao hupewa nafasi ya kwanza kuchukua viwanja hivyo kujenga hizo nyumba za kupangisha...
Kisha hata siku moja tusifikirie kwamba kiongozi anaweza kuvua joho lake la uongozi kufuata utaratibu ambao unamweka yeye sawa na raia wa kawaida.. Hata siku moja hawezi kupanga msitari kupanda daladala mkuu wangu usijechanganya vitu hivi na ukweli unasimama peke yake...
Tunawalipa kodi zetu, mishahara mikubwa, magari majumba na kadhalika kuliko hata viongozi wa nchi za Ulaya tena hata baada ya kustaafu bado wanapokea ruzuku kubwa kuliko daktari wa Muhimbili, hivyo hakuna sababu kabisa ya viongozi hawa kujihusisha na biashara...

Mkandara:

Unachozungumzia ni Ethics au miiko ya uongozi katika Azimio la Arusha. Miiko ya uongozi ni sehemu tu ya Azimio la Arusha.

Hata Nyerere mwenyewe alisema kuwa kulitupa Azimio la Arusha sio mbaya kwake. Lakini kutupa Ethics za uongozi kulikuwa kunamsumbua kwani hata nchi za kibepari zina ethics za uongozi.

Ni lazima tulinganisha mapera kwa mapera. Na mafenesi kwa mafenesi.

Hapa watu wanavunja sheria za nchi. Na hatua zinaweza kuchukuliwa kama vile mwizi wa kuku anavyochukuliwa hatua.

Mwanawasa aliweza kufanya vitu vyake bila kuwa na Azimio la Arusha. Alitumia sheria tu.
 
Zakumi,
Unachozungumzia ni Ethics au miiko ya uongozi katika Azimio la Arusha. Miiko ya uongozi ni sehemu tu ya Azimio la Arusha
..
Exactly!.. Azimio la Arusha lilikuwa na mabaya yake ambayo ndiyo yalitakiwa kurekebishwa na Azimio la Zanzibar lakini badala yake kilichobadilishwa ni Ethics za Uongozi.. Kumbuka kwamba tuliacha Siasa za Ujamaa July 1984 siku mwalimu alipotangaza kushindwa kwa Ujamaa hivyo kuacha milango wazi ya Biashara..
Toka siku hiyo policy ya open market ilikutumika na mabaya tuliyoyajua sisi ndio ulikuwa mwisho wake...Mwaka 1992 - miaka minane baadaye (kama sikosei) ndipo Mwinyi alipotangaza Azimio la Zanzibar hiyo - RUKSA..na hakuna jambo lolote lililokuwa geni ktk Uchumi isipokuwa nafasi ya viongozi wetu kujihusisha na biashara. Kwa hiyo Azimio la Zanzibar lilikuja kuvunja miiko ya Uongozi. Uongozi wa Mwinyi unatia Kichefuchefu kiuchumi toka hilo Azimio lilipotangazwa, machafu yote utayakuta baada ya Azimio hilo..
Hivyo mkuu, unapolipigia debe Azimio la Zanzibar ni sawa na kupingana na maneno ya mwalimu uliyoyaandika hapo juu..Hakuna kati yetu anayesema Azimio la Arusdha lilikuwa bomba kichizi isipokuwa pale tunapogusia swala la Uongozi bora na ndilo tatizo kubwa la Tanzania. Mara nyingi tumeshindwa kutafuta kiini cha matatizo yetu badala yake tuna laumu watu na sio policy iliyoshinikiza.
Ukitazama ukumbi wa siasa utaona karibu mada zote zinahusiana na Uongozi bora na kwa bahati mbaya tumeshindwa kuelewa kwamba yote haya yametokana na kuvunjika kwa hiyo miiko ya Uongozi. Ni hilo Azimio la Zanzibar lilompa uwezo Mkapa, Mramba, Yona, Karume, na wengine wote kufanya waliyoyafanya kwa sababu ilikuwa ruksa kufanya biashara ama kwa lugha inayoendana na Uongozi nitasema KUJITAJIRISHA...

Hakuna ethics za Uongozi ambazo zinaambatana na sheria zinazowapa uhuru Viongozi kufanya biashara. Ni sawa na Padre unayemruhusu kufunga ndoa lakini anakatazwa kutongoza mwanamke au mwanafunzi wake... unafikiri huyo mke atampata vipi?..

Ethics za Uongozi ni lazima ziambatane na sheria zinazokataza hata kukaribia kufanya maovu, Wala Takribun - waarabu wanasema..Hata katika mashirika ya kawaida huwezi kumwona CEO wa shirika moja la Simu akiruhusiwa kufungua kampuni yake ndogo ya simu na ukategemea hataifanya kazi ya shirika hilo vizuri..Acha hilo huku Ulaya kuna mashirika hata ndugu yako huruhusiwi kuwajiri ukisha kuwa na wadhifa fulani...
Ukimwacha Lowassa anunue hisa ya kumiliki Celtel unategemea atafanya nini zaidi ya kuhakikisha anaua Ushindani, anaweka masharti rahisi na pengine kodi ndogo ktk shirika hilo..
Hata ukitazama matatizo ya nyumba na viwanda.. Kinachotuumiza wengi sio ununuzi wa viwanda hivyo ama fedha njugu walizolipa isipokuwa ni ile ruksa ya hao viongozi kujipanga na kuzichukua.. hakuna mtu ambaye atajipangia bei kubwa ama masharti magumu lakini kama hawa viongozi wangekuwa hawaruhusiwi ungeona tofauti ya bei na tender za Ukweli zikitumika..UWAZI ungekuwepo kwani hakuna mtu angetaka kuonekana kauza kitu kwa hasara...Mkapa kaichukua Kiwira kwa sababu alikuwa rais hakuna sababu nyingine..Ni hivyo hivyo kwa viongozi wote wamegawana mali zetu chini ya uhuru waliopewa na sasa hivi tumeganda hatujui la kufanya.. Kisheria walilipa thamani ya viwanda hivyo hata kama ilichorwa, lakini walilipa hawakuiba wala kunyang'anya, hivyo sio wao waliovunja sheria isipokuwa sheria zenyewe ndizo zilikuwa mbovu.. tazama maswala ya madini hata Waziri mkuu wa Canada alishangaa kusikia tumefungiwa kanyaboya na Barricks kiasi kile, na kashidnwa kutusaidia kwa sababu tuliingia mkataba kisheria.. Mkapa kaondoka na asilimia zake 10 ambazo huweiz kuziona zinaingia direct ktk sahani lake...
 
Halafu swala la Kupangisha nyumba ni bomu kabisa..haiwezekani kila mtu apangishe nyumba lazia kuwepo na utaratibu wa kupangisha ili kodi za mapato ya kupangishwa ziweze kukusanywa... Serikali inatakiwa kuweka maazimio yenye manufaa kwa Taifa na sio kutazama mtu mmoja mmoja, hapa nikiwa na maana kuwa unaporuhusu kupangisha nyumba lengo lkake linakuwa kutunisha mfuko wa serikali ktk pato la kodi za upangishaji, hivyo ni lazima iwekwe taratibu ambazo zitahakikisha kwamba wapangishaji wanafuata masharti ya kupangisha, sio swala la kumsaidia mtu mahala pa kuishi.....

Mkandara,

Dr. Hussein Mwinyi ana nyumba zake kadhaa na moja iko pale Mlalakua kapangisha watu wa VETA na anakusanya si chini ya $4000.00 kwa mwezi!Jiulize mshahara wake kwa mwezi ni kiasi gani na tunaambiwa ana nyumba nne kapangisha wazungu na ma-TX?
 
Back
Top Bottom