Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 12,835
- 23,584
Baada ya Kifo cha John Magufuli Africa ya mashariki kiongozi imara na mwenye maono aliyebaki ni Paul Kagame Rais wa Rwanda.
Akihojiwa na mwandishi wa habari Mario Nawfal hivi karibuni kagame amesikitishwa na kitendo cha Afrika mashariki kuendelea kuingiza nguo zilizotumika maarufu kama mitumba kutoka nchi za nje wakati nchi hizo zinalima pamba na kuuza Nje.
Anasema walikaa kikao kama viongozi wa Afrika mashariki na wakakubaliana kusitisha biashara ya kuagiza nguo chakavu kutoka nje na kuanzisha pamoja na kuendeleza viwanda vya nguo katika ukanda wa mashariki ya afrika. Anasema marekani ilipopata habari hizo walitoa taarifa kwa nchi za afrika mashariki ni marufuku kuzuia uagizaji wa nguo chakavu kutoka marekani. Viongozi wetu baada ya kuelezwa hayo walinywea na kukubaliana na masharti ya Marekani.
Viongozi wetu wakishindwa kufanya maamuzi magumu tutaendelea kutawaliwa na mataifa haya yenye nguvu hata kufikia kutwezwa utu wetu kwa mambo ambayo tunayaweza sisi wenyewe.