Paul Kagame: Nashangaa Afrika mashariki tunalima pamba na kuuza Nje ila tunaagiza nguo za mitumba kutoka nje

Huyo mshamba wako alikuwa na maono gani, kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato? Yule alikuwa mshamba katili, Na huyo lofa skeleton maono yake ni kuua wakongomani na kuwaibia madini yao? We kwl ni bwege
Punguza kisirani!!
 
Huyo mshamba wako alikuwa na maono gani, kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Chato? Yule alikuwa mshamba katili, Na huyo lofa skeleton maono yake ni kuua wakongomani na kuwaibia madini yao? We kwl ni bwege
Umekula lakini?
 
Pamba tuna viwanda kibao vinatengeneza Bidhaa humu humu, yeye ana viwanda vingapi?

Tanzania tunatumia Pamba yetu kwa kiasi kikubwa humu humu Ndani kuanzia Kanga, Vitenge, Uniform za Jeshi, Mashuka mbalimbali kuanzia ya shule hadi yanayotumika majumbani, mablanket etc.

Bidhaa za Cotton si za bei rahisi, ni ghali, either utumie Nyuzi chache kama vile Kanga ama ukubali kuuziwa bei kubwa.

Mfano kwenye Mashuka ya Cotton ya kulalia anatengeneza Hapa Tanzania na kiwanda kama Nida ila still bei sio competitive, Shuka la ndani la cotton 35,000 wakati Mchina ukubwa huo huo kwa material ya Polyester anauza 16,000.

So tatizo letu sio mtumba bali bidhaa za bei rahisi za Polyester ambazo watu wengi wanakimbilia.
 
Sisi tuna mtengenezea Marekani Nguo, Levis na brand nyengine kama Wrangler za Marekani zinatengenezwa Tanzania hapo Ubungo, tatizo si Viwanda bali bei, Cotton ni Gharama, Upo Tayari kununua jeans Laki? Ama utatafuta mtumba ama low Quality mchina?


View: https://youtu.be/JBfRl5UCyRs?si=maIhk7Lco19qqls9
Video ikionesha kiwanda cha Levis.
 
Serikali yetu haijaweka kipaumbele tu kwenye viwanda vya nguo.
 
Serikali yetu haijaweka kipaumbele tu kwenye viwanda vya nguo.
Serikali walishabinafsisha hivyo viwanda, watu Binafsi ndio wanamiliki kama Vile Metl (MO Dewji), na uzalishaji ni mkubwa, Huu uzi wa Zamani ila una data wa Viwanda vya MO tu.

Mita milioni 120 za Fabric, na Revenue $100M kwenye viwanda vyake vya Textiles mwaka 2014

Na hizi data 21st century toka kwa Metl wenyewe


Tanzania tuna zalisha tani 280,000 kwa mwaka za Pamba, 21st century cha Morogoro pekee kinatumia Tani 45,000 ambazo ni zaidi ya Asilimia 15 ya uzalishaji.

Bado kuna Kile cha Musoma, Kuna Cha Arusha wale wa mashuka, KUNA Nida hapa Dar etc

So tuna viwanda vingi mno vinavyotumia Pamba za ndani kuanzia Mabatiki, Shirt, Kanga, Vitenge, Mashuka, Mablanket etc ni made in Tanzania.
 
Shuka la pamba kufua utata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…