Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
RC MAKONDA ACHUKUWA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KIGAMBONI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 15 amechukuwa Fomu ya kuomba ridhaa ya Kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi CCM.
Jimbo hilo lilikuwa chini ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amechukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kigamboni, kitendo hicho kinaweza kuibua upya madai yake ya kughushi vyeti vya elimu na nyaraka zingine.
Kuna tuhuma kuwa Paul Makonda alitumia vyeti vya Daud Albert Bashite. Siasa ni mchezo mchafu, inaweza kupelekea kuwekewa pingamizi kwenye Tume ya Uchaguzi au ushindi wake kuja kupingwa mahakamani.
Mwaka 1995 Ramadhan Ali Kihiyo alishinda ubunge jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, baadae NCCR Mageuzi ilienda Mahakamani kupinga kuwa Kihiyo alitumia vyeti visivyo vyake kuwania ubunge. Wakati kesi ikiwa inaendelea Mahakama kuu Kihiyo alijiuzulu ubunge.