Mimi nadhani hii imefanywa kwa makusudi ili kuwaumiza gang fulani linaloonekana kutaka kumzuwia Mwenyekiti kwenye kinyang’anyiro cha 2025 ! Hii ni calculated move sio bahati mbaya !!
HALI NDANI YA CCM siyo shwari baada ya Paul Makonda kuteuliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM katika kikao ambacho kilijaa masikitiko na lawama nyingi sana kwa nini na sababu zipi zinafanya apewe hiyo nafasi. Wajumbe wengi wa NEC wametafsiri kuwa ubabe ukitumika kumsimika kwenye nafasi hiyo na wakidai hana sifa za kuwa Mwenezi wa CCM kuna ambao walidiriki kusema bora angeridishwa Polepole au Shaka lakini siyo Makonda.
Chanzo chetu toka ndani ya kikao cha NEC zinasema wa kwanza kabisa kupinga uteuzi wa Makonda alikuwa ni waziri mkuu mstaafu Mzee Mizingo Pinda ambaye alisema " kijana huyu katukana wastaafu wote na kafanya kila aina ya makosa na uovu lakini leo anafaaje kuwa na cheo kikubwa kiasi hiki ndani ya chama" Pinda aliendelea kusema kama kuna ulazima sana wa kurudishwa kwenye serikali au kupewa madaraka basi atafutiwe cheo kingine lakini siyo kuwa mwenezi wa chama kwa sababu ana historia chafu na ya hovyo sana ndani ya chama na nje ya chama na kwa watanzania CCM haitaeleweka kuteua mtu mhalifu kiasi kile kuwa kiongozi tena wa nafasi ya mwenezi.
Hali ilikuwa mbaya zaidi pale wajumbe wengi walipoonekana kutoridhishwa na kuletwa jina la Makonda na wengine mpaka wakaonya kwa nini kunakuwa na mabadiliko ya nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama mara tatu ndani ya miaka 2 tu? Kuna mjumbe alihoji kuwa "mwenyekiti ulituletea Shaka ulipoingia,baada ya muda ukamtoa ukamleta Mjema na sasa unamtoa unamleta Makonda shida ni nini"
Baada ya kuona majibizano ni makali sana na wajumbe hawataki kabisa jina la Mkonda tunataarifiwa kuwa Mwenyekiti akaamua kura ipigwe kwa majina mawili aliyopendekeza ambayo yalikuwa nai jina la CHALAMILA na MAKONDA na baada ya kupigwa kura Makonda akamzidi CHAKAMILA kwa kura moja na akawa mwenezi kama ulivyotangwazwa.
Baada ya kikao cha NEC tunaarifiwa Kinana na JK na kundi la vjana wao wanaojiita wamekulia kwenye chama walikubaliana kukutana Dar Es Salaam nyumbani kwa Kinana na kikao kilifanyanyika na moja ya mambo waliyoazimia ni kuwa MAKONDA PAUL hafai kuwa Mwenezi wa CCM na watahakikisha kazi yake inakuwa ngumu sana na wameshaanza chini kwa chini kupeleka sumu mikoani na wilayani kuwashawishi wana CCM kutompa ushirikiano atakapoanza kuzunguka mikoani na mawilayani kwa ajili ya kukitangaza chama.
Suala la pili ni kuwa wamempa jukumu Chenge kuhakikisha kanda ya ziwa CCM inakataliwa kwa kiasi kikubwa na dalili zianze kuonekana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 ili mwaka 2025 kwa pamoja wamtake mwenyekiti wao apishe mtu mwingine asimame kwenye urais kwa kuwa chama kimemkataa na kimepasuka kwa sababu ya maamuzi yake.
Kinana kapewa jukumu la kujiuzulu umakamu uenyekiti kabla ya mwezi December 2023 na aweke wazi kuwa hakubaliani na mwenyekiti kwenye maamuzi mengi na hasa ya kumteua Makonda kuwa Katibu Mwenezi na kuwa hakumshirikisha na hivyo bora akae pembeni kulinda heshima yake na heshima ya chama.
Kwa hiyo muda wowote kuanzia sasa Kinana ataomba kujiuzulu umakamu mwenyekiti wa chama na kukaa pembeni sasa kuratibu mipango ya kumuondoa Rais 2025 akishirikiana na akina Chenge na JK na January Makamba yeye kapewa jukumu la kukusanya fedha za kukamilisha mipango hiyo na anashirikiana na Luhanga Mpina sasa kuoroshesha na kuzunguka majimbo yote ya kanda ya Ziwa ambayo CCM ni lazima ishindwe ili kuwe na sababu ya kumtaka mwenyekiti wao asiwe mgombea 2025 na kwa kifupi wanajipanga kufanya mapinduzi na hawataki Rais Samia awe mgombea 2025.
Sasa wenye kusikia wasikie na wenye kukaa kimya wakae kimya lakini HABARI NDIYO HIYO..
#KigogoMedia
Sent using
Jamii Forums mobile app