Paul Makonda aipasua CCM, kigogo ndani ya chama atishia kujiuzulu

Paul Makonda aipasua CCM, kigogo ndani ya chama atishia kujiuzulu

HALI NDANI YA CCM siyo shwari baada ya Paul Makonda kuteuliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM katika kikao ambacho kilijaa masikitiko na lawama nyingi sana kwa nini na sababu zipi zinafanya apewe hiyo nafasi. Wajumbe wengi wa NEC wametafsiri kuwa ubabe ukitumika kumsimika kwenye nafasi hiyo na wakidai hana sifa za kuwa Mwenezi wa CCM kuna ambao walidiriki kusema bora angeridishwa Polepole au Shaka lakini siyo Makonda.

Chanzo chetu toka ndani ya kikao cha NEC zinasema wa kwanza kabisa kupinga uteuzi wa Makonda alikuwa ni waziri mkuu mstaafu Mzee Mizingo Pinda ambaye alisema " kijana huyu katukana wastaafu wote na kafanya kila aina ya makosa na uovu lakini leo anafaaje kuwa na cheo kikubwa kiasi hiki ndani ya chama" Pinda aliendelea kusema kama kuna ulazima sana wa kurudishwa kwenye serikali au kupewa madaraka basi atafutiwe cheo kingine lakini siyo kuwa mwenezi wa chama kwa sababu ana historia chafu na ya hovyo sana ndani ya chama na nje ya chama na kwa watanzania CCM haitaeleweka kuteua mtu mhalifu kiasi kile kuwa kiongozi tena wa nafasi ya mwenezi.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale wajumbe wengi walipoonekana kutoridhishwa na kuletwa jina la Makonda na wengine mpaka wakaonya kwa nini kunakuwa na mabadiliko ya nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama mara tatu ndani ya miaka 2 tu? Kuna mjumbe alihoji kuwa "mwenyekiti ulituletea Shaka ulipoingia,baada ya muda ukamtoa ukamleta Mjema na sasa unamtoa unamleta Makonda shida ni nini"

Baada ya kuona majibizano ni makali sana na wajumbe hawataki kabisa jina la Mkonda tunataarifiwa kuwa Mwenyekiti akaamua kura ipigwe kwa majina mawili aliyopendekeza ambayo yalikuwa nai jina la CHALAMILA na MAKONDA na baada ya kupigwa kura Makonda akamzidi CHAKAMILA kwa kura moja na akawa mwenezi kama ulivyotangwazwa.

Baada ya kikao cha NEC tunaarifiwa Kinana na JK na kundi la vjana wao wanaojiita wamekulia kwenye chama walikubaliana kukutana Dar Es Salaam nyumbani kwa Kinana na kikao kilifanyanyika na moja ya mambo waliyoazimia ni kuwa MAKONDA PAUL hafai kuwa Mwenezi wa CCM na watahakikisha kazi yake inakuwa ngumu sana na wameshaanza chini kwa chini kupeleka sumu mikoani na wilayani kuwashawishi wana CCM kutompa ushirikiano atakapoanza kuzunguka mikoani na mawilayani kwa ajili ya kukitangaza chama.

Suala la pili ni kuwa wamempa jukumu Chenge kuhakikisha kanda ya ziwa CCM inakataliwa kwa kiasi kikubwa na dalili zianze kuonekana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 ili mwaka 2025 kwa pamoja wamtake mwenyekiti wao apishe mtu mwingine asimame kwenye urais kwa kuwa chama kimemkataa na kimepasuka kwa sababu ya maamuzi yake.

Kinana kapewa jukumu la kujiuzulu umakamu uenyekiti kabla ya mwezi December 2023 na aweke wazi kuwa hakubaliani na mwenyekiti kwenye maamuzi mengi na hasa ya kumteua Makonda kuwa Katibu Mwenezi na kuwa hakumshirikisha na hivyo bora akae pembeni kulinda heshima yake na heshima ya chama.

Kwa hiyo muda wowote kuanzia sasa Kinana ataomba kujiuzulu umakamu mwenyekiti wa chama na kukaa pembeni sasa kuratibu mipango ya kumuondoa Rais 2025 akishirikiana na akina Chenge na JK na January Makamba yeye kapewa jukumu la kukusanya fedha za kukamilisha mipango hiyo na anashirikiana na Luhanga Mpina sasa kuoroshesha na kuzunguka majimbo yote ya kanda ya Ziwa ambayo CCM ni lazima ishindwe ili kuwe na sababu ya kumtaka mwenyekiti wao asiwe mgombea 2025 na kwa kifupi wanajipanga kufanya mapinduzi na hawataki Rais Samia awe mgombea 2025.

Sasa wenye kusikia wasikie na wenye kukaa kimya wakae kimya lakini HABARI NDIYO HIYO..

#KigogoMedia

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya kikao cha NEC tunaarifiwa Kinana na JK na kundi la vjana wao wanaojiita wamekulia kwenye chama walikubaliana kukutana Dar Es Salaam nyumbani kwa Kinana na kikao kilifanyanyika na moja ya mambo waliyoazimia ni kuwa MAKONDA PAUL hafai kuwa Mwenezi wa CCM na watahakikisha kazi yake inakuwa ngumu sana na wameshaanza chini kwa chini kupeleka sumu mikoani na wilayani kuwashawishi wana CCM kutompa ushirikiano atakapoanza kuzunguka mikoani na mawilayani kwa ajili ya kukitangaza chama
 
Kinana hajawahi kuua mtu. Hakuna uchafu unaoweza kupita ule wa kutoa roho ya binadamu mwenzio

Makonda ameua akina Ben Sanane, Azory na kumshambulia Lissu
Zote hizo ni hadithi za kutunga. Unalo hata tone la ushahidi la kuthibitisha makonda kumuua mtu yeyote? Acha maneno ya vijiwe vya kahawa
 
Rais Samia amechanganyikiwa kwenye hili. Repercussions zake ni mbaya sana. Kuna methali inasema "adui mwombee njaa"

Hapa naona maadui wa Samia wamefanikiwa kumuombea NJAA. Makonda hakufaa kurudi kwenye utumishi wa chama wala Serikali bali alipaswa kuwa gerezani tu. Hii ni DHIHAKA kubwa kwa Watanzania

Ila iko siku Paul Makonda ataingia tu gerezani na kutumikia kifungo kwa maovu yake
Kweli tupu mkuu,👍,Samia is out of her senses.Kwa hili wenye akili na wasio wachumia tumbo,CCM bye bye,"kwanza si mama yangu," Mwalimu Nyerere alisema,
 
Kweli tupu mkuu,👍,Samia is out of her senses.Kwa hili wenye akili na wasio wachumia tumbo,CCM bye bye,"kwanza si mama yangu," Mwalimu Nyerere alisema,
Jumba bovu ndiyo limeanza kupata nyufa, 2025 linadondoka na waliokuwamo wanakufa nalo
 
Mimi ni mwana CCM, nasema bila unafikia kwamba katika teuzi za hovyo Samia amefanya huu wa Makonda umetia fora!
Makonda hana hadhi, uadilifu wala ueweledi wa kuwa Mwenezi wa CCM Taifa.
Ila waswahili wana msemo wao wa " Ndege wafananao huruka pamoja"!
CCM inalazimishwa kuwa Chama Cha Mazuzu !
Kwa zama na nyakati kama hizi Makonda anahitajika,mtu asietabirika asieogooa yeyote ndio anaweza okoa chama!

Hao unaowaona wanafaa huku wakifumbia hjinga macho kwa neno haki hawafai kwa sasa !tunataka haki na wajibu.ndani ya chama na serikali!
 
Makonda ukipewa mic tena usiache kutupa ya kukujadili wiki mbili mfululizo au iwe kwa mwezi mzima kabisa.. Hii ya juzi ilikuwa safi sana. Tunajadili nyuzi zaidi ya kumi, kisa mtu mmoja wewe tu.
 
Kwa zama na nyakati kama hizi Makonda anahitajika,mtu asietabirika asieogooa yeyote ndio anaweza okoa chama!

Hao unaowaona wanafaa huku wakifumbia hjinga macho kwa neno haki hawafai kwa sasa !tunataka haki na wajibu.ndani ya chama na serikali!
Kwa majibu haya,CCM kweli ni chama cha mazuzu.
 
Zote hizo ni hadithi za kutunga. Unalo hata tone la ushahidi la kuthibitisha makonda kumuua mtu yeyote? Acha maneno ya vijiwe vya kahawa
Ushahidi upo sana. Ni suala la muda tu. Subiri Rais Samia atakapotoka madarakani. Huyo shoga lazima akaliwe msambwanda wake mkubwa jela
 
Hisia dhidi ya uhalisia.
Wengi wenu mnahisi vitu ambavyo si halisi.
Maana hamna siku ambayo umeletwa ushahidi zaidi ya nadharia.
Wewe nani ukatae ushahidi? Kwani wewe ndiyo Makonda? Utakataaje watu wanasema wana ushahidi Subiri atakapotoka Samia madarakani, huyu Nyamitako lazima atapanda kizimbani tu. Labda afe mapema
 
Back
Top Bottom