Pre GE2025 Paul Makonda ameagiza Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Pangani Haraka Sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CHADEMA ninyi huwa hamjitambui na wala hamuelewi mnataka nini. Kwa ujinga wenu mmeanza kushindana na kanisa la KKKT. jambo ambalo kamwe hatafanikiwa zaidi ya kupata laana tu na kusambaratika kama kondoo.
Wewe una laana toka kwa Mama yako.
 
Kwa hiyo unaposema kesi ya mtu fulani ilitupwa je kwa akili yako ulitaka mlalamikaji apewe ushindi hata wakati kesi yake haina kichwa wala miguu?
Ni sawa kwa wakurugenzi kusimamia uchaguzi unaomhusisha boss aliyewateua(rais)?
Mahakamani kinachoshinda na hoja za kisheria na siyo blaa blaa
Mahakama zipi hizo ?
au kwenda kujazana mahakamani kama ambavyo huwa mnafanya ninyi CHADEMA
Kesi ya Mbowe sio tu kujazana watu walizuiwa hadi kuingia na simu ila mabalozi na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa na kesi tulikua tunapata update hapa jukwaani mashahidi wa kubumba wa serikali waliyokua wanaumbuka.
 
Ndio ni sawa tu kwa wakurugenzi kusimamia uchaguzi maana wanakula kiapo kabla ya kuanza kazi hiyo ya uafisa wa tume ya uchaguzi.ndio maana hao hao wakurugenzi ndio walikuwa wakiwatangaza akina Mbowe,Lissu,sugu,mnyika,lema n.k.kuwa ni washindi wa ubunge.
 
Hakuna kipya zaidi ya watu kuingiza per diem hata wewe akili yako inawaza the same.
Mheshimiwa Makonda anafanya kazi kwa uzalendo na siyo kutafuta pesa maana kama pesa tayari anazo za kutosha.kumbuka amekuwa mjumbe katika bunge maalumu la katiba,DC,RC na Sasa katibu mwenezi wa CCM Taifa.kwa hiyi hana sababu ya kufanya kazi kwa ajili ya kutafuta pesa bali anafanya kazi kwa ajili ya kuwasaida watanzania wanyonge.
 
Kwa mujibu wa katiba, PM atateuliwa kutoka Wabunge wa majimbo na si vinginevyo
Hiyo ni mipango ya uchaguzi ujao.wananchi wana kiu ya kutaka kuona Mheshimiwa Makonda anapewa nafasi nyeti serikalini.maana ameonyesha uthubutu na ujasiri wa hali ya juu sana katika kuwatetea wananchi wanyonge.
 
Ni mwanasiasa na si mamlaka ya uteuzi.Labda kwa hapo unieleweshe kati ya mamlaka ya uteuzi na msemaji wa chama cha siasa.
Kwa uelewa wako chama na serikali ni nani mkubwa? Nani anayetangulia kabla ya mweziye? Nani anayemuunda mwenziye? Nani anayekwenda kwa wananchi ambao ndio wenye nchi na mamlaka na nchi yao?
 
Kwa uelewa wako chama na serikali ni nani mkubwa?
Chama ni muunganiko wa watu wenye itikadi sawa.
Nani anayetangulia kabla ya mweziye? Nani anayemuunda mwenziye?
Hujui kuwa kuna nchi zina wagombea huru "independent candidate" asiyefungamana na upande wowote?

Na kwenye rasimu ya Warioba 2014 CCM mliyoifungia kabatini kipengele hiki kilikuwemo.
Nani anayekwenda kwa wananchi ambao ndio wenye nchi na mamlaka na nchi yao?
Je mgombea huru atawakilisha chama gani?

Anahitaji manifesto tu ndio blueprint yake sio chama au wapambe.

Kwahivyo tungetakiwa kuwa na mgombea huru sio lazima hivi vyama maana napo kuna matapeli.

Nimeamua nijibu haya maswali japo haikuwa quoted kwangu sababu una uwezo mdogo na ndio maana nimegundua machawa mnapendwa sababu mnatupiwa script mnabeba tu bila kuuliza.
 
Kwa uelewa wako chama na serikali ni nani mkubwa? Nani anayetangulia kabla ya mweziye? Nani anayemuunda mwenziye? Nani anayekwenda kwa wananchi ambao ndio wenye nchi na mamlaka na nchi yao

Kwa uelewa wako chama na serikali ni nani mkubwa? Nani anayetangulia kabla ya mweziye? Nani anayemuunda mwenziye? Nani anayekwenda kwa wananchi ambao ndio wenye nchi na mamlaka na nchi yao?
Kwahiyo chama kinaoverule katiba? Wanaoiweka serikali madarakani ni wananchi na siyo chama. Chama kinapewa tu dhamana. Na serikali ni mali ya wananchi na siyo chama. Mamlaka za uteuzi zilizopo ni kwa mujibu wa katiba ya nchi na si katiba ya chama. Mimi niliomba ufafanuzi ili nielewe sasa kama ukiniuliza swali bado nitabaki kwamba sijakuelewa
 
Hao wananchi wanauwezo serikali madarakani kupitia uchaguzi ,ambapo katika uchaguzi chama ndicho kinachokwenda kwa wananchi kuomba kura kwa kunadi sera zake kupitia ilani yake ambayo ndio mkataba wake rasmi na Wananchi. Kwa hiyo chama kina haki zote kufuatilia utekelezaji wa ilani yake ambayo ndio mkataba na wananchi .kwa kuwa kikienda tena kuomba kula itakibidi kieleze kimefanya nini kwa miaka mitano katika utekelezaji wa mkataba wake. Wananchi wanaiweka serikali madarakani kupitia chama cha Siasa.kumbuka huwezi ukawa diwani au mbunge au Rais bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa na kupewa baraka za kugombea uongozi.
 

Labda unipe tafsiri sahihi ya chama cha siasa na wananchi vs serikali ili tueleweshane zaidi.
 
Maccm mnajichanganya sana
Jana Nchimbi kakataza viongozi wa chama kuwakosoa wa serikali, makonda anafanya yake.
 
Maccm mnajichanganya sana
Jana Nchimbi kakataza viongozi wa chama kuwakosoa wa serikali, makonda anafanya yake.
Kwa hiyo unataka viongozi wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea wasichukuliwe hatua? Unataka uozo ufumbiwe macho? Unataka hatua zisichukuliwe kwa watu wanaoshindwa kutimiza vyema majukumu yao?

Pia naona hukuielewa vyema kauli ya katibu mkuu wetu. Na wala haikuwa na lengo kama unalotaka kulitafsiri wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…