Pre GE2025 Paul Makonda ameagiza Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Pangani Haraka Sana

Pre GE2025 Paul Makonda ameagiza Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Pangani Haraka Sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mheshimiwa Makonda anafanya kazi kwa uzalendo na siyo kutafuta pesa maana kama pesa tayari anazo za kutosha.kumbuka amekuwa mjumbe katika bunge maalumu la katiba,DC,RC na Sasa katibu mwenezi wa CCM Taifa.kwa hiyi hana sababu ya kufanya kazi kwa ajili ya kutafuta pesa bali anafanya kazi kwa ajili ya kuwasaida watanzania wanyonge.
Akili za kitoto hizi nani aliyewahi kushiba na kuchoka pesa??
Donald Trump bado anatafuta pesa sembuse DAB??
Tumia akili kijana..
 
Mheshimiwa Makonda anafanya kazi kwa uzalendo na siyo kutafuta pesa maana kama pesa tayari anazo za kutosha.kumbuka amekuwa mjumbe katika bunge maalumu la katiba,DC,RC na Sasa katibu mwenezi wa CCM Taifa.kwa hiyi hana sababu ya kufanya kazi kwa ajili ya kutafuta pesa bali anafanya kazi kwa ajili ya kuwasaida watanzania wanyonge.
Akili za kitoto hizi nani aliyewahi kushiba na kuchoka pesa??
Donald Trump bado anatafuta pesa sembuse DAB??
Tumia akili kijana..
 
CCM haikupora uchaguzi bali ilipita kihalali kwa kura halali kabisa za wananchi.
Kupora uchaguzi sio kwamba nakuuliza bali naweka record sawa. Na sababu ya upuuzi ule, hakuna mtua anayejitambua tena atajitokeza kushiriki kwenye hizo chaguzi za tume zinazowajibika kwa mwenyekiti wa ccm.

Narudia tena, viongozi wote ni majizi ya kura ya ccm, iweje washindwe kutatua matatizo ya wananchi wa sehemu husika, hadi wamsubiri huyo muhalifu ndio ajifanye anatatua matatizo ya wananchi? Bado kunakuwaga na wajinga wa hivyo?
 
Chama ndicho kinampa maagizo waziri. Kumbuka na elewa ya kuwa CCM Ndio iliyounda serikali na siyo serikali iliyounda CCM. Ni CCM ndiyo itakayo kwenda kwa wananchi kuomba kura kwa hiyo ni lazima CCM iwakatae na kuwawajibisha kupitia serikali yake watendaji na viongozi wote wanaoonekana kuwa vikwazo katika kuwahudumia wananchi na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Unachanganya mambo,vikao na maamuzi ya Chama hupelekwa serikalini na si kiongozi 2a Chama kumkoromea mtumishi.Mtapigwa makofi hadharani
 
Sasa wewe jidanganye ufanye uzembe halafu ukutwe na kubainika .kwa hakika utakiona cha mtema kuni na kujuta kuzaliwa.

Hakuna lolote litafanyika, ni wangapi amewataja halafu hakuna kilichofanyika?
Wengine hadi kwenye report ya CAG wametajwa, nini kimefanyika?

Hakuna lolote , ni matamko ya kisiasa tu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda ametoa maagizo ya chama kwa waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa Pangani Haraka sana.

Hii ni baada ya kukutana na kero nyingi sana katika halmashauri hiyo zilizotolewa na wananchi pamoja na Wafanyabiashara mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa huduma kwa halmashauri lakini hawalipwi pesa zao ,na wanapodai haki zao za kulipwa madai yao wamekuwa wakipewa majibu yasiyoridhisha huku mkurugenzi akijifanya Mungu mtu.

Mheshimiwa Makonda pia ametoa maagizo kwa Mh waziri kuhakikisha kuwa anaunda timu na kuipeleka Pangani kwenda kufanya uchunguzi wa masuala mbalimbali ambayo yamekuwa ni kero na kulalamikiwa na wananchi . Pia amezungumzia suala la kukwama kwa miradi ya serikali na masuala mengine mengi sana yanayochochea chuki ya wananchi kwa serikali yao.

Katika hatua nyingine Ametoa pia kauli nzito sana iliyotetemesha na kuibua shangwe kwa wananchi baada ya kuagiza wakurugenzi wote nchini kushugulikia kero za wananchi ,na kwamba mahali ambapo itaonekana mkurugenzi ameshindwa kutatua kero basi chama hakitasita kutoa maagizo kwa serikali ya kusimamishwa kazi kwa mhusika. Lakini pia amewaagiza wenyeviti wote wa CCM nchini wilaya na mikoa kutoa taarifa juu ya wakuu wa mikoa,wilaya ,wakurugenzi na watendaji wengine wa serikali wanaoshindwa kufanya kazi na kutimiza majukumu yao vizuri ili wachukuliwe hatua.

Ndugu zangu Watanzania kupitia jukwaa hili niliwatahadhalisha sana na kuwasihi sana viongozi wote wa serikali mikoani na wilayani kuwa waanze kufanya kazi na kwenda kwa wananchi kuwasikiliza kero zao.niliwaambia ya kuwa ziara za Mheshimiwa Makonda zitakuwa za moto sana tena sana na zitasomba wengi sana hasa wale wazembe na wanaofanya kazi kwa mazoea na kujifanya miungu watu hawatasalimika wala kuachwa salama katika ziara za Mheshimiwa Makonda. Kwa sababu kila mtu anafahamu ya kuwa Mheshimiwa Makonda hanaga huruma wala subira wala uvumilivu kwa wazembe kazini.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Taarifa mpya ya hivi punde.

Ni kuwa Tayari muda huu mkurugenzi amesimamishwa kazi na waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa kama alivyoelekezwa na kuagizwa na chama. Amesimamishwa ili kupisha uchunguzi.
View attachment 2878884
hizo ni drama za ccm kama zile za kinana za kugawa tshirt za umoja ni ushindi
watumishi wa umma hawafukuzwi kazi na watu wenye akili ndogo kama makonda
kumfuatilia huyu bwana inahitaji uwe na tatizo la afya ya akili
 
hizo ni drama za ccm kama zile za kinana za kugawa tshirt za umoja ni ushindi
watumishi wa umma hawafukuzwi kazi na watu wenye akili ndogo kama makonda
kumfuatilia huyu bwana inahitaji uwe na tatizo la afya ya akili
Mheshimiwa Makonda ni akili kubwa na ndio maana amekuwa mbunifu sana na kiongozi mwenye kuleta matokeo makubwa na Chanya kila atakapopewa nafasi ya uongozi na kuongoza
 
Hii namba y simu ni ya nn? Au teuzi wakufikie kiwepesi.
 
Hakuna mvivu na mzembe kazini atakaye bakia salama wakati huu. Maana chama hakipo tayari kuchonganishwa na wananchi kwasababu ya uzembe wa watu wachache walioamua kufanya kazi kwa mazoea na kushindwa kubadilika.

Wanaona uchaguzi umekaribia wanaanza kuwalaghai wananchi
 
Back
Top Bottom