Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Dupe

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2013
Posts
1,668
Reaction score
811
Wakati- Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akijisalimisha kwa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.

Juzi, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ilitoa amri kwa askofu huyo kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kashfa na matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Askofu Gwajima alitii amri hiyo na jana alifika kituoni hapo saa 8.15 mchana kwa ajili ya kutoa maelezo.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kwenda kutoa maelezo, Askofu Gwajima alisema Baraza la Maaskofu Tanzania, lilikubaliana kupinga Mahakama ya Kadhi lakini Askofu Pengo akawageuka..

"Tulikubaliana kwa pamoja kwamba hatutaki na viongozi wote tulisaini makubaliano hayo akiwamo Kardinali Pengo lakini tunashangaa alitugeuka," alisema na kuongeza:

"Mimi kama kiongozi wa kiroho nilimkemea kiongozi mwenzangu wa kiroho."

Alisema katika maneno aliyotoa hakuna neno lolote ambalo ni la kashfa..."yale yote ambayo nimeongea ni maneno kutoka kwenye Biblia. Kwa hiyo leo (jana) nimeshangaa kuitwa na polisi. Nilitarajia kama kuitwa angeitwa yeye (Kardinali Pengo)," alisema Askofu Gwajima na kuongeza kuwa, aliitikia wito huo ili kufahamu ni kwa nini ameitwa. Mapema wiki hii, mitandao mbalimbali ya kijamii, ilisambaza sauti ya Askofu Gwajima akitoa maneno makali ya kumkashifu Kardinali Pengo.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema: "Taratibu za mahojiano zimeanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa- atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu na rafiki yake wa karibu anayemwamini au wakili wake."

Akizungumzia kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima, Kova alisema ni pamoja na kumkashifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo.

Kuitwa kwa DC Kinondoni

Katika hatua nyingine, Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. "Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini.

Chanzo:
Mwananchi
 
Pbagu kabisa huyu dogo hivi hajui nguvu ya waumini nini? Akae pembeni tu huyu dogo asijifanye yeye kuwa ni mkatoliki sana
 
Huyu gwajima kwanza ameharibu ndoa ya kijana mwenzetu Mbasha alafu bado anajiita mchungaji,tunaomba serikali itusaidie kudeal na mamluki was hivi kwenye jamii yetu ...this guy deserves to be tasked on how to keep manners
 
Sasa wewe DC kiherehere na kujishebedua mpaka huku jamani! Ungekuwa Regional Commissioner au Minister c ndo ingekuwa balaa! Ndo mana mm nlishajua tu kwmb hicho cheo ulichopewa ni kama umepandikizwa kwa maslahi ya akina flani flani tu. Idiot kabisa!
 
Wakati- Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akijisalimisha kwa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.

Juzi, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ilitoa amri kwa askofu huyo kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kashfa na matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Askofu Gwajima alitii amri hiyo na jana alifika kituoni hapo saa 8.15 mchana kwa ajili ya kutoa maelezo.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kwenda kutoa maelezo, Askofu Gwajima alisema Baraza la Maaskofu Tanzania, lilikubaliana kupinga Mahakama ya Kadhi lakini Askofu Pengo akawageuka..

“Tulikubaliana kwa pamoja kwamba hatutaki na viongozi wote tulisaini makubaliano hayo akiwamo Kardinali Pengo lakini tunashangaa alitugeuka,” alisema na kuongeza:

“Mimi kama kiongozi wa kiroho nilimkemea kiongozi mwenzangu wa kiroho.”

Alisema katika maneno aliyotoa hakuna neno lolote ambalo ni la kashfa...“yale yote ambayo nimeongea ni maneno kutoka kwenye Biblia. Kwa hiyo leo (jana) nimeshangaa kuitwa na polisi. Nilitarajia kama kuitwa angeitwa yeye (Kardinali Pengo),” alisema Askofu Gwajima na kuongeza kuwa, aliitikia wito huo ili kufahamu ni kwa nini ameitwa. Mapema wiki hii, mitandao mbalimbali ya kijamii, ilisambaza sauti ya Askofu Gwajima akitoa maneno makali ya kumkashifu Kardinali Pengo.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema: “Taratibu za mahojiano zimeanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa- atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu na rafiki yake wa karibu anayemwamini au wakili wake.”

Akizungumzia kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima, Kova alisema ni pamoja na kumkashifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo.

Kuitwa kwa DC Kinondoni

Katika hatua nyingine, Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. “Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini.

Chanzo:
Mwananchi

sio kashfa kumwambia kiongozi mkuu wa dini kuwa amevaa pampasi !!!
 
Hizi ndizo kazi za Mkuu wa Wilaya??

Mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani kwenye wilaya yake.Matamshi ya Gwajima yaweza letelea vurugu katika wilaya yake ya kinondoni kati ya wakatoliki wanaomheshimu Pengo na wafuasi wa Gwajima waliokuwa wakishangilia wakati Pengo akiporomoshewa matusi ya nguoni.

HIVYO KUMWITA NI SAWA
 
usinikumbushe haya. kama alithubutu kumpiga wazir mstafu na hakuna aliyemuita kumhoji zaidi ya kupewa mkuu wa wilaya.
 
hivi paul makonda naye ameshafikia level hiyo ya kumwita gwajima afike ofisini? naomba gwajima avumilie manake kwa ninavyomjua, makonda anaweza kupata za uso kuliko pengo muda si mrefu. hata hivyo ccm mwaka huu watapambana sana na gwajima, najua atawatandika sana.
 
usinikumbushe haya. kama alithubutu kumpiga wazir mstafu na hakuna aliyemuita kumhoji zaidi ya kupewa mkuu wa wilaya.
anatumia kifungu gani cha sheria ambacho kama hataenda atakuwa amekaidi amri ya mkuu wa wilaya?hicho ndio cha muhimu, otherwise unaweza kumwita asije, utamfanya nini?
 
Dah!

"...the picture drop down without because..."

Hii inaitwa chizi kapewa rungu.

Hivi mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya ana mamlaka hayo? Au ndo mwendelezo wa kusaka kiki tu kama Gwajima mwenyewe?
 
Back
Top Bottom