Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Nadhani Gwajima hatakwenda na wala hatamjibu chochote huyu Makonda.
Maana akitii na kwenda ofisini basi Makonda atapata Kiburi zaidi, na akimjibu atampa umaarufu wa bure. Shortly apige kimya.
 
Mkuu wa Wilaya at work!!!!!!

Tiba
 
Wakati- Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akijisalimisha kwa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.

Juzi, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ilitoa amri kwa askofu huyo kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kashfa na matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Askofu Gwajima alitii amri hiyo na jana alifika kituoni hapo saa 8.15 mchana kwa ajili ya kutoa maelezo.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kwenda kutoa maelezo, Askofu Gwajima alisema Baraza la Maaskofu Tanzania, lilikubaliana kupinga Mahakama ya Kadhi lakini Askofu Pengo akawageuka..

“Tulikubaliana kwa pamoja kwamba hatutaki na viongozi wote tulisaini makubaliano hayo akiwamo Kardinali Pengo lakini tunashangaa alitugeuka,” alisema na kuongeza:

“Mimi kama kiongozi wa kiroho nilimkemea kiongozi mwenzangu wa kiroho.”

Alisema katika maneno aliyotoa hakuna neno lolote ambalo ni la kashfa...“yale yote ambayo nimeongea ni maneno kutoka kwenye Biblia. Kwa hiyo leo (jana) nimeshangaa kuitwa na polisi. Nilitarajia kama kuitwa angeitwa yeye (Kardinali Pengo),” alisema Askofu Gwajima na kuongeza kuwa, aliitikia wito huo ili kufahamu ni kwa nini ameitwa. Mapema wiki hii, mitandao mbalimbali ya kijamii, ilisambaza sauti ya Askofu Gwajima akitoa maneno makali ya kumkashifu Kardinali Pengo.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema: “Taratibu za mahojiano zimeanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa- atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu na rafiki yake wa karibu anayemwamini au wakili wake.”

Akizungumzia kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima, Kova alisema ni pamoja na kumkashifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo.

Kuitwa kwa DC Kinondoni

Katika hatua nyingine, Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. “Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini.


Chanzo:
Mwananchi
DC kijana mwenye makeke tunataka vijana kama hao ila busara ndio Zero cc Paul Makonda
 
Last edited by a moderator:
kuliko kuwa mwingi wa maneno bora kuwa kilema au kipofu ipo siku makonda atajutia mdomo wake kukosa breack:ballchain:
 
Hizi ndizo kazi za Mkuu wa Wilaya??

Ndio...kuhakikisha amani inatamalaki wilayani kwake.Gwajima ni hatari kwa usalama wa taifa.lazima uelewe kuna kundi kubwa hapo kiongozi wao wa juu ametukanwa
 
Dc Makonda anahitaji ushauri nasaha kwa kudandia treni kwa mbele.
Ofisi ya Dc na ofisi ya Kova ni nani yuko juu zaidi ?!
 
Muvi inaendelea wakuu,

Wakati Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amejisalimisha kwenye Jeshi la Polisi kwa mahojiano hali iliyopelekea Askofu huyo kupoteza fahamu; naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka Askofu huyo aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.


Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. "Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini."

11081016_360745177443838_2390948105818373976_n.jpg



 
----- huyu, hana uwezo wa kisheria kumwita mtu ofisini kwake, labda awe ni mfanyakazi wa ofisi yake
 
Gwajima ni Firauni mkubwa....mzinifu, ma.laya sana...kampiga miti sana Flora...leo hii anatoa maneno hata ktk uchungaji wa uchawi na nguvu za giza hayapo...maneno ya ushenzi na uhayawani...amini mchungaji huyo anatumia ushetani ktk kuendesha ktk lake...na ni mfanya biashara tu...wala sio mcha Mungu...!!!
Acha kutukana viongozi wa Kikristo.Najua hizo ni Hasira za kuikataa Mahakama ya Kadhi.Unachotakiwa uelewe ni kwamba Mahakama ya Kadhi haiwezekani Tanzania sio kwa Utawala wa CCM tu hata Upinzani wakishika Nchi.Kama kuna mtu anataka kulipa fadhila kwa mgongo wa Mahakama ya Kadhi jua hataweza kufanya hivyo.
 
Nasema KWELI TUPU kwamba Laana aliyotangaza baba ask.Gwajima itawatafuna wengi aliyelaaniwa kama mtini na wadandiaji !
 
Last edited by a moderator:
Tunataka viongozi wa namna hii safi sana makonda dc kijana mchapa kazi.
 
Back
Top Bottom