Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Nadhani Gwajima hatakwenda na wala hatamjibu chochote huyu Makonda.
Maana akitii na kwenda ofisini basi Makonda atapata Kiburi zaidi, na akimjibu atampa umaarufu wa bure. Shortly apige kimya.
 
Mkuu wa Wilaya at work!!!!!!

Tiba
 
DC kijana mwenye makeke tunataka vijana kama hao ila busara ndio Zero cc Paul Makonda
 
Last edited by a moderator:
kuliko kuwa mwingi wa maneno bora kuwa kilema au kipofu ipo siku makonda atajutia mdomo wake kukosa breack:ballchain:
 
Hizi ndizo kazi za Mkuu wa Wilaya??

Ndio...kuhakikisha amani inatamalaki wilayani kwake.Gwajima ni hatari kwa usalama wa taifa.lazima uelewe kuna kundi kubwa hapo kiongozi wao wa juu ametukanwa
 
Dc Makonda anahitaji ushauri nasaha kwa kudandia treni kwa mbele.
Ofisi ya Dc na ofisi ya Kova ni nani yuko juu zaidi ?!
 
Muvi inaendelea wakuu,

Wakati Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amejisalimisha kwenye Jeshi la Polisi kwa mahojiano hali iliyopelekea Askofu huyo kupoteza fahamu; naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka Askofu huyo aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.


Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. "Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini."




 
----- huyu, hana uwezo wa kisheria kumwita mtu ofisini kwake, labda awe ni mfanyakazi wa ofisi yake
 
Acha kutukana viongozi wa Kikristo.Najua hizo ni Hasira za kuikataa Mahakama ya Kadhi.Unachotakiwa uelewe ni kwamba Mahakama ya Kadhi haiwezekani Tanzania sio kwa Utawala wa CCM tu hata Upinzani wakishika Nchi.Kama kuna mtu anataka kulipa fadhila kwa mgongo wa Mahakama ya Kadhi jua hataweza kufanya hivyo.
 
Nasema KWELI TUPU kwamba Laana aliyotangaza baba ask.Gwajima itawatafuna wengi aliyelaaniwa kama mtini na wadandiaji !
 
Last edited by a moderator:
Tunataka viongozi wa namna hii safi sana makonda dc kijana mchapa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…