Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni,imeahirisha kesi ya jinai namba 1/2022, dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda,hadi Februari 8.

Kuahirishwa kwa kesi hiyo kunatokana na mahakimu kuwa na majukumu mengine ya Kimahakama eneo la Segerea.

Hii ndio Taarifa iliyopatikana kwenye viunga vya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, ambako leo ilitarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza kesi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda .

Kesi hii imefunguliwa na Mbunge wa zamani wa Ubungo, Saed Kubenea.

Taarifa za Wakili wa Kubenea inasema kwamba Makonda hakupokea wito wa Mahakama kwa vile hapatikani , aweza kuwa kajificha au kakimbia nchi .

Kesi imeahirishwa hadi wiki ijayo ambapo Wito mpya wa Mahakama umetolewa ili atafutwe na kukabidhiwa .

====

MWANAHABARI mkongwe nchini Tanzania, Saed Kubenea, anakusudia kuiomba Mahakama ya Kinondoni, itoe wito mpya kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ili ahudhurie katika kesi aliyoifungua dhidi yake na Serikali.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 3 Februari 2022 na Wakili wa Kubenea, Hekima Mwasipu, akizungumza na wanahabari mahakamani hapo, baada ya kesi hiyo namba 1/2022, kuahirishwa hadi Jumanne ya tarehe 8 Februari mkwaka huu.

Katika kesi hiyo, Kubenea anaomba kibali cha mahakama kumshtaki Makonda, akidai Serikali kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na Mkurugenzi wa Makosa ya Upelelezi nchini (DCI).

Imeshindwa kutekeleza majukumu yake ya kumshtaki kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka yanayomkabili. Katika kesi hiyo, Kubenea anaishtaki Ofisi ya DPP, DCI na Makonda.

Wakili Mwasipu amedai kuwa, ombi hilo wataliwasilisha mahakamani hapo Jumanne ijayo, wakati kesi hiyo ikienda kutajwa mbele ya Hakimu Aron Lyamuya.

Amedai wanakusudia kuchukua hatua hiyo, baada ya jitihada zao za kumpata Makonda kugonga mwamba.

“Ni kweli kesi ilkuwa inakuja kwa ajili ya kutajwa lakini imeahirishwa hadi Jumanne na mjibu maombi namba tatu ambaye ni Makonda, hakuweza kufika mahakamani. Sababu tumemtafuta sana tumeshindwa kumpata tunakusudia kuiomba mahakama tupewe summons mpya,” amedai Wakili Mwasipu.

Wakili Mwasipu amedai kuwa, wito huo endapo utatolewa, wanatarajia kuutangaza katika magazeti na kwenye njia nyingine, ili taarifa zimfikie Makonda.

Tunakusudia kuiomba mahakama hiyo tupewe summons mpya kum-save, ikiwemo kuandika kwenye gazeti na sehemu nyingine yeyote tutakayoona inafaa. Ili aweze kupata taarifa kwamba kuna kesi iko mahakamani,” amedai Wakili Mwasipu.

Hii ni mara ya pili kwa Makonda kutohudhuria katika usikilizwaji wa kesi hiyo, ambapo mara ya kwanza alishindwa kuhudhuria tarehe 3 Desemba 2021 bila ya kutoa taarifa yeyote.

Aidha, Wakili Mwasipu amesema kesi hiyo iliyokuwa inatajwa leo, imeahirishwa baada ya Hakimu Lyamuya kuwa na udhuru.

“Sababu ya kesi kuahirishwa ni waheshimiwa mahakkimu wanakwenda Segerea kuna shughuli ya kimahakama,” amesema Wakili Mwasipu.

Katika kesi hiyo, Kubenea anamshtaki Makonda kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwemo tukio la uvamizi la ofisi za Kituo cha Televisheni cha Clouds Tv, jijini Dar es Salaam, lkililotokea Machi 2017

Chanzo: Mwanahalisi.

 
Kweli dunia duara, hujafa hujaumbika ndiyo huyu aliyekuwa anawaambia wabunge ambao si wakazi wa Dar es salaam marufuku kuwaona mjini, huyu aliyesema ukija mjini uwe umeoga, leo anaishi kama digidigi kwenye msitu wa simba wakali. Aiseee

Poa ila sisi wanaume tunaoendesha IST bado tunam-mind sana tu yaani.
 
Kweli dunia duara, hujafa hujaumbika.... ndiyo huyu aliyekuwa anawaambia wabunge ambao si wakazi wa Dar es salaam marufuku kuwaona mjini, huyu aliyesema ukija mjini uwe umeoga...leo anaishi kama digidigi kwenye msitu wa simba wakali...aiseee

poa ila sisi wanaume tunaoendesha IST bado tunam-mind sana tu yaani.
Uyu_Binadam_kama_angekuwa_Uwaziri_wa_Mambo_ya_ndani_au_Rais_Sijui_Tanzania_ingekuwaje_%3F_%F0%...jpg
 
Kweli dunia duara, hujafa hujaumbika.... ndiyo huyu aliyekuwa anawaambia wabunge ambao si wakazi wa Dar es salaam marufuku kuwaona mjini, huyu aliyesema ukija mjini uwe umeoga...leo anaishi kama digidigi kwenye msitu wa simba wakali...aiseee

poa ila sisi wanaume tunaoendesha IST bado tunam-mind sana tu yaani.
Huyu huyu aliyesema katika mkoa wake ni lazima wanaume wote wapimwe tezi dume.
 
Back
Top Bottom