Pre GE2025 Paul Makonda asimikwa kuwa Chifu Nsumbantale, yaani Msaidizi wa Chifu Mkuu Hangaya ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Mama Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hakika ni Rais Samia Mpaka 2030 na Fomu ni moja tu ndani ya chama kwa ajili yake hapo mwakani
Zinafyatuliwa tano,na hapo tutaziona sana namba za simu za Lucas🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️
 
Mheshimiwa Makonda ni Rais kuanzia 2030,kwa hiyo hilo kila mtu akae akijua hivyo
Kila la kheri 😅😅🙏
Ila ukumbuke ipo KARMA !!
KARMA huwa haikosei anuani !
Kama aliwafanyia watu ubaya ujue ipo siku atalipiziwa na hiyo KARMA !
Na mema pia ni vivyo hivyo !!
KARMA huwa haikosei haisahau na haimuonei mtu 😅🙏🙏🙏 !
 
Siyo roho ngumu, ni roho ya shetani yaani ni kama ile roho ya Jiwe
Aliwataja mpaka waliomsaidia kumpandisha 😅😱
Ngoja Tusubiri tuone huu mziki utaishaje !!
Jamaa ana Roho ngumu na instincts zake zimeshamnusisha harufu nzuri za Magogoni 😅😂🔥
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mwenyekiti wa machifu mkoa wa Shinyanga Kidola njange amesema ya kuwa umoja wa machifu na watemi mkoa wa Shinyanga kwa pamoja na umoja wao wamekubaliana kumsimika katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda kuwa Chifu Nsumbantale,yenye maana ya Msaidizi wa Chifu mkuu Hangaya ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa. Ambapo sasa baada ya usimikwaji huo atakuwa msaidizi wake katika masuala ya siasa.

Ambapo katika usimikwaji huo Mheshimiwa Makonda amevishwa shuka jeusi lenye maana au lenye kuashiria wingu zito la mvua ambalo ni neema kwa watu ,kwa kuwa linashusha mvua ambapo mvua siku zote ni baraka na neema,kwa kuwa ni katika mvua tupatapo mazao ya aina mbalimbali ikiwepo ya chakula na biashara.

Mheshimiwa Makonda alivishwa pia shuka jekundu lenye maana au kuashiria utayari wa kulinda chama na serikali ya chama cha Mapinduzi.

Lakini pia Mheshimiwa Makonda alikabidhiwa mkuki wenye maana ya kumkumbusha juu ya ulinzi wa chama na serikali ya chama cha Mapinduzi

Pia alivalishwa mkufu wenye kuashiria kuwa watu wa Shinyanga wapo pamoja naye wakati wote na yeye ndiye anayetegemewa sana.

Kwa hiyo sasa Mheshimiwa Paul Makonda ukienda kule Shinyanga anatambulika na kufahamika kama Chifu Nsumbantale yaani msaidizi wa chifu Hangaya ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa.

Bila shaka hii yote ni kutokana na kuguswa na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda nakuona namna anavyofanya kazi kubwa ya kumsemea Rais Samia na mwenyekiti wa CCM Taifa kila anakopita na kukanyaga lazima alitajwa jina la Rais Samia kwa heshima kubwa sana na kueleza mambo makubwa aliyoyafanya katika kila sehemu.

Kwa hakika Paul Makonda siyo mtu wa kawaida ndugu zangu. Ni mtu mwenye ushawishi na nguvu kubwa sana isiyopimika . Angalieni anakopita huko namna wananchi wanavyofurika na kumiminika kama mafuriko ya maji.anavuta maelfu ya watu kama sumaku ikutanapo na chuma. Kwa hakika Rais Samia alicheza karata ya karne kwa kumleta Paul Makonda wakati huu.angalia namna anavyompigania na kumsemea kwa nguvu zote kwote apitapo huko mikoani.

Mungu aendelee kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kupambana kuhakikisha kuwa anawafikia wananchi wengi sana na kuwasikiliza kero zao ili kuziwasilisha kwa viongozi wa serikali kwa utatuzi zaidi.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
L drama on the beat😊😊😊
 
Ni kawaida ya Binadamu wenye roho mbaya kuwachukia wale watu wanaoipigania haki japo kwa kuisemea tu hiyo Haki !
Kwahiyo hata yeye Makonda atachukiwa na wenye roho mbaya wasiopenda kuiona Haki ikipiganiwa kama anavyoonekana kuipigania !
Lakini pia hata yeye Makonda amekuwa na ataendelea kuwachukia watu wowote wale ambao wamekuwa au wanaendelea kuipigania Haki wakiwa nje ya Chama Chake !!
Na pia atawachukia wale waliomo Chamani ambao wanaitetea Haki itendeke ambayo hiyo haki inaweza kumkwaza kwenye mbio zake za matamanio yake !!😅😅 🙏🙏🙏
 
Huwa naj
Ndugu zangu Watanzania,

Mwenyekiti wa machifu mkoa wa Shinyanga Kidola njange amesema ya kuwa umoja wa machifu na watemi mkoa wa Shinyanga kwa pamoja na umoja wao wamekubaliana kumsimika katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda kuwa Chifu Nsumbantale,yenye maana ya Msaidizi wa Chifu mkuu Hangaya ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa. Ambapo sasa baada ya usimikwaji huo atakuwa msaidizi wake katika masuala ya siasa.

Ambapo katika usimikwaji huo Mheshimiwa Makonda amevishwa shuka jeusi lenye maana au lenye kuashiria wingu zito la mvua ambalo ni neema kwa watu ,kwa kuwa linashusha mvua ambapo mvua siku zote ni baraka na neema,kwa kuwa ni katika mvua tupatapo mazao ya aina mbalimbali ikiwepo ya chakula na biashara.

Mheshimiwa Makonda alivishwa pia shuka jekundu lenye maana au kuashiria utayari wa kulinda chama na serikali ya chama cha Mapinduzi.

Lakini pia Mheshimiwa Makonda alikabidhiwa mkuki wenye maana ya kumkumbusha juu ya ulinzi wa chama na serikali ya chama cha Mapinduzi

Pia alivalishwa mkufu wenye kuashiria kuwa watu wa Shinyanga wapo pamoja naye wakati wote na yeye ndiye anayetegemewa sana.

Kwa hiyo sasa Mheshimiwa Paul Makonda ukienda kule Shinyanga anatambulika na kufahamika kama Chifu Nsumbantale yaani msaidizi wa chifu Hangaya ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa.

Bila shaka hii yote ni kutokana na kuguswa na uchapa kazi wa Mheshimiwa Makonda nakuona namna anavyofanya kazi kubwa ya kumsemea Rais Samia na mwenyekiti wa CCM Taifa kila anakopita na kukanyaga lazima alitajwa jina la Rais Samia kwa heshima kubwa sana na kueleza mambo makubwa aliyoyafanya katika kila sehemu.

Kwa hakika Paul Makonda siyo mtu wa kawaida ndugu zangu. Ni mtu mwenye ushawishi na nguvu kubwa sana isiyopimika . Angalieni anakopita huko namna wananchi wanavyofurika na kumiminika kama mafuriko ya maji.anavuta maelfu ya watu kama sumaku ikutanapo na chuma. Kwa hakika Rais Samia alicheza karata ya karne kwa kumleta Paul Makonda wakati huu.angalia namna anavyompigania na kumsemea kwa nguvu zote kwote apitapo huko mikoani.

Mungu aendelee kumjalia afya njema na nguvu za kuendelea kupambana kuhakikisha kuwa anawafikia wananchi wengi sana na kuwasikiliza kero zao ili kuziwasilisha kwa viongozi wa serikali kwa utatuzi zaidi.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
huwa najiuliza wale wanaoenda kwenye mikutano ya makonda na kudanganywa kiasi kile ni watanzania wa wapii?
 
Makonda Ana vituko kweli kweli
Makonda anapenda amshaamsha
[emoji1]

Ova
 
Watanzania tulivyo wajinga na tusiotumia akili na tusio na upeo wa kuona hata dakika chache mbele!
Hao machifu uchwara waliokuwa wanampa uchifu wa kila kabila sijui wanajisikiaje huko walipo muda huu!

Kila ufanyalo jaribu kufikiri kesho pia.
 
Kwani walikosea nini.
 
Back
Top Bottom