Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba..Upo utaratibu wa wazi wa kushughurikia tuhuma za kijinai au madai (Tort)
Yapo makosa makubwa na madogo kijinai lakini kuna mfumo na utaratibu sawia wa kutoa taarifa..Kupeleleza,Kushitaki na kuhukumu..
Rais wa nchi ni mkubwa sana,Urais ni taasisi kubwa mno na ni zaidi ya mtu..Kuna makosa ukituhumiwa au akituhumiwa yeyote kutaka kutenda/Kujaribu kutenda yanaweza kuwa uhujumu Serikali;Uasi au uhaini..
Hivyo tuhuma zozote zenye chembechembe za uhujumu,Uasi,Uhaini hazipaswi kuchukuliwa kwa wepesi..Mtoa taarifa,watuhumiwa wote wanapaswa kuchunguzwa kwa kina na kwa haki..Kisha ikiwa kuna mapana ya ushahidi basi taratibu na hatua kali za kisheria zapaswa kuchukua mkondo wake..
Lakini pia zisipothibitika na kuwa uzushi/Fitina/Faraka/Husuda basi mtoa taarifa anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria ili iwe fundisho.