Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

šŸ˜‚šŸ˜‚
Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli
nimecheka hapo kwenye kama ni mama yake kweli
 
Nchi Ya Kutishia Kutaja Halafu Hakuna Kinachoendelea Popote
Hii Mikwara Tanzania Ni Ya Hovyo Hakuna Anayeweza Kutaja
 
Chama Kimepasuliwa Na Kimesuka Sasa Vipande Vipande, CCM Inakufa Kibudu Ndugu Zangu
 
Nchi inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba..Upo utaratibu wa wazi wa kushughurikia tuhuma za kijinai au madai (Tort)

Yapo makosa makubwa na madogo kijinai lakini kuna mfumo na utaratibu sawia wa kutoa taarifa..Kupeleleza,Kushitaki na kuhukumu..

Rais wa nchi ni mkubwa sana,Urais ni taasisi kubwa mno na ni zaidi ya mtu..Kuna makosa ukituhumiwa au akituhumiwa yeyote kutaka kutenda/Kujaribu kutenda yanaweza kuwa uhujumu Serikali;Uasi au uhaini..

Hivyo tuhuma zozote zenye chembechembe za uhujumu,Uasi,Uhaini hazipaswi kuchukuliwa kwa wepesi..Mtoa taarifa,watuhumiwa wote wanapaswa kuchunguzwa kwa kina na kwa haki..Kisha ikiwa kuna mapana ya ushahidi basi taratibu na hatua kali za kisheria zapaswa kuchukua mkondo wake..

Lakini pia zisipothibitika na kuwa uzushi/Fitina/Faraka/Husuda basi mtoa taarifa anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu na kisheria ili iwe fundisho.
 
Yaani aibu tupu. RC anawapa onyo Mawaziri tena kwa vitisho!! Ndiyo maana tunasema CCM na Serikali yake imeishiwa maarifa.

Hebu fikiria wakati Konda Boy anatoa upupu wake ule, Kuna Watendani Wakuu wa Chama na Serikali walimshangilia.
Nadhani TISS wanapita humu, watafute namna ya kumshauri Rais vizuri kuhusu huyu mwendawazimu
 
Back
Top Bottom