Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
Mkuu watoto wa mjini wamemfanya vibaya sana! Ana maumivu makubwa mno!

Hajaelewa kuwa hata Samia mwenyewe hawawezi na hadhubutu kwenda kwenda kinyume nao!

Makonda alijua atawafanya kitu mbaya kwenye mchucho wa ubunge uchaguzi ujao ndani ya chama, kumbe wenzie walikuwa mbele ya mahesabu yake kwa miaka miwili mbele!

Hizo ni kelele za chura tu, the last kicks of a dying horse! Ajiandae kupotea kwenye siasa! Haamini, Mlango wa kutokea uko dhahiri.

Haaminiki kamwe!
 
Mkuu watoto wa mjini wamemfanya vibaya sana! Ana maumivu makubwa mno!

Hajaelewa kuwa hata Samia hawawezi na hadhubutu kwenda kwenda kinyume nao!

Makonda alijua atawafanya mbaya kwenye mchucho wa ubunge Dani ya chama, kumbe wenzie walikuwa mbele ya mahesabu yake kwa miaka miwili mbele!

Hizo ni kelele za chura, the last kicks of a dying horse! Ajiandae kupotea kwenye siasa! Haamini, Mlango wa kutokea uko dhahiri.

Haaminiki kamwe!
Akipigwa bench ndiyo itakuwa furaha kuu kwa watanzania
 
The statement of the gentleman was right and ofcoz , he is doing a very great job to the country 🐒

The man is the sokoine of modern Times 🐒
Eti sokoine haha 😄
Makonda fisadi kama mafisadi
Wengine tatizo mnapelekeshwa
Na siasa za umbea,udaku,maneno msneno

Ova
 
Eti sokoine haha 😄
Makonda fisadi kama mafisadi
Wengine tatizo mnapelekeshwa
Na siasa za umbea,udaku,maneno msneno

Ova
you are free to express your opinions and emotions, its your right

but the truth is that,
the gentleman is among very strong and committed young politician we ever had in TZ AFTER SOKOINE :NoGodNo:
 
Huyo roporopo anataka Ubunge wa Arusha mjini mana anadhani atakuja kuwa PM baada ya uchaguzi wa 2025.Kuwa RC wa Arusha ni mpango Mkakati kupita njia za Gambo.
Sasa ndugu kweli unaamini Makonda akigombea Arusha kuna wakumshinda?
 
Yeye anawawajua na wao wanaju hivo kwa hiyo wanajuana sasa inakuwaje au imetokeaje?
 
Akipigwa bench ndiyo itakuwa furaha kuu kwa watanzania
Kwako wewe sio Watanzania wote! Hivi wewe unadhani watu wote wanafana?
Hata hao Mawaziri wanaosemwa mnaona kama wanaonewa ila ndo washezi wakubwa sana!
 
Hakuna waziri anafanya hicho kitu bali Makonda anatafuta namna ya kuwapaka shombo mawaziri ambao hana mahusiano nao mazuri kama; Nape Nnauye, Januari Makamba, Hussein Bashe, Riz 1 Kikwette.

Kupata uwaziri ndiyo ndoto ya wabunge wengi baada ya uchaguzi. Rais Samia amekupa Uwaziri, unaanzaje kulipa watu
Kila muwamba ngoma huvutia kwake ngozi.

Kwamba Makonda hafai maneno yake kwa Rais naye ni mkuu wa mkoa na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa ila wewe Kiluilui Mwananchi wa JF usikilizwe?!

Rais Samia kazi anayo!
 
Na hapo alipo Arusha ataondolewa na sababu itakuwa hawezi kufanya kazi na viongozi wenzake, kiherehere kikizidi ndo huwa kama hivyo, walioko chini yake wengine ni umri wa baba yake lkn anawananga kama watoto wake hata mdogo wako hauwezi kumpereka kama mbuzi, wakuu wa wilaya wataomba kupangiwa kazi nyingine au kuhamishwa, wakuu wa vitengo wataomba kuhama, tusubiri ....
You sound more like a blackmail and not a statement.
 
Nadhani huyu alitisha sana viongozi wakati wa JPM, ni Bingwa wa Fitna, ana uwezo wa kufanya lolote kama tunavyojua.

Fitna ya uongo madawa ya kulevya , si uliona wakati huo SSH akiwa VP, Mjaliwa PM walikuwa kimyaa
Fitna kwa Sirro akiwa kanda maalum, nani alikemea
Akina VP, PM, NWM n.k. wanamuogopa huyu bingwa wa Fitna. Lakini pia aliyempa madaraka hawezi kumdhibiti!! ???
Kwamba leo hii Makonda ni bingwa wa Fitna kumzidi Rais mstaafu Kikwete kwa mujibu wa wana JF?

Hapa Makonda alipogusa kuna kitu, hasiachie.
 
Alipiga naye picha Marekani.Naona Samia hajampa alichokitaka. Chickens are coming home to roost.
Mtangulizi wake ametukanwa sana huyo mwanamke, mitandaoni, wapinzani na wengi ndani ya baraza lake la mawaziri hajawahi kutoa tamko kukemea chochote.

Ndio kwanza alikuwa anachochea moto kwa kauli zake za kimafumbofumbo akionyesha kuwaunga mkono.

Kwamba Muosha naye huoshwa?

Tatizo meza imepinduliwa ghafla sana watu wamepeperushwa na kimbunga chake!
 
Kwamba leo hii Makonda ni bingwa wa Fitna kumzidi Rais mstaafu Kikwete kwa mujibu wa wana JF?
Hapa Makonda alipogusa kuna kitu, hasiachie.
Kila mtu ana lake na linajadiliwa kwa lake. Mimi nilishasema wazi kuhusu JK lakini hapa si mahali pake
Mada ni Makonda. Ni bingwa wa Fitna! tueleze kesi ya madawa nani alishtakiwa? Kesi ya Wanaume na watoto nani alishtakiwa? Kesi ya kupima Wanaume tezi dume kwa lazima, nani alipima?
Roma alikuwa wapi na alirejeshwa vipi na makonda si aliyosema?

Orodha ya Fitna ina kurasa 999, inatosha kusema ni Bingwa mbobevu katika Fitna.
Kifo cha Sokoine kinahusiana vipi na matusi ya mitandaoni? Sokoine alifariki hata internet haijagunduliwa, wapi na wapi!
 
Kila mtu ana lake na linajadiliwa kwa lake. Mimi nilishasema wazi kuhusu JK lakini hapa si mahali pake
Mada ni Makonda. Ni bingwa wa Fitna! tueleze kesi ya madawa nani alishtakiwa? Kesi ya Wanaume na watoto nani alishtakiwa? Kesi ya kupima Wanaume tezi dume kwa lazima, nani alipima?
Roma alikuwa wapi na alirejeshwa vipi na makonda si aliyosema?

Orodha ya Fitna ina kurasa 999, inatosha kusema ni Bingwa mbobevu katika Fitna.
Kifo cha Sokoine kinahusiana vipi na matusi ya mitandaoni? Sokoine alifariki hata internet haijagunduliwa, wapi na wapi!
Kweli mambo mchakamchaka 🙆‍♀️

Leo hii Paul Makonda ni bingwa na mbobevu wa Fitna za kisiasa ndani ya JMT?

I never thought I would live to read this from you, Nguruvi.

Pascal Mayalla naomba uje ushuhudie hii.
JokaKuu msome Nguruvi.
 
Kweli mambo mchakamchaka 🙆‍♀️

Leo hii Paul Makonda ni bingwa na mbobevu wa Fitna za kisiasa ndani ya JMT?

I never thought I would live to read this from you, Nguruvi.

Pascal Mayalla naomba uje ushuhudie hii.
JokaKuu msome Nguruvi.
Pengine tofauti na Fitnati wengine yeye anajiweka wazi at least kwa kujua au kutojua.

Nimekuuliza, nitajie jina moja tu la mtu aliyeshtakiwa kwa madawa ya kulevya! kama huna , je hiyo siyo FItna ya uzamivu? Unahitaji tuweke Fitna zake nyingine kuanzia Dar hadi Dodoma!
 
Back
Top Bottom