Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Pengine tofauti na Fitnati wengine yeye anajiweka wazi at least kwa kujua au kutojua.

Nimekuuliza, nitajie jina moja tu la mtu aliyeshtakiwa kwa madawa ya kulevya! kama huna , je hiyo siyo FItna ya uzamivu? Unahitaji tuweke Fitna zake nyingine kuanzia Dar hadi Dodoma!
Ukiniuliza hivyo nami nitakuuliza majukumu ya mkuu wa mkoa ambae ni mwakilishi wa Rais na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa husika.

Siku zote, sheria, protocol na hata history + mazoea vinaonyesha mkuu wa mkoa ni mouth piece na kitendea kazi cha Rais kwenye eneo husika.

Mimi kinachonistaajabisha kutoka kwako ni kumpa Salute ya ubingwa na ubobevu wa Fitna za kisiasa Paul Makonda, Salute ambayo ameishi na kudumu nayo Rais mstaafu Mzee Kikwete!

Tukivuta pumzi kidogo, tukumbushane chanzo/mwanzo wa Paul Makonda katika siasa za Tanzania.

Alitambulishwa na nani rasmi katika mduara wa siasa za Kitaifa?

Ni nani mwalimu/coach/mentor wake wa siasa za Kitaifa na siasa za JMT?

Majibu ya hapo juu yatatupa mwanga halisi.
 
Ni Samuel Sitta ndiye aliyem mentor Makonda kisiasa kwa kumuingiza kwenye bunge maalum la Katiba. Japo alimvua na ubingwa
 
Hakuna waziri anafanya hicho kitu bali Makonda anatafuta namna ya kuwapaka shombo mawaziri ambao hana mahusiano nao mazuri kama; Nape Nnauye, Januari Makamba, Hussein Bashe, Riz 1 Kikwette.

Kupata uwaziri ndiyo ndoto ya wabunge wengi baada ya uchaguzi. Rais Samia amekupa Uwaziri, unaanzaje kulipa watu wamtukane mtu alikupa Uwaziri ambayo ni privilege adimu?

Yaani huyu Makonda anaweza kuwa na TAARIFA za ndani kuliko TISS wenye kazi yao?

Kama ambavyo akiwa Mwenezi wa CCM hakujua majukumu yake, huku nako kwenye u RC wa Arusha bado Makonda hajui kazi yake.

USHAURI KWA RAIS SAMIA:
Chonde chonde Rais Samia USIINGIE mtego huu wa Makonda. Huyu NI ZEROBRAIN atakuharibia uRais wako.

Haiba yako Rais Samia na ya Makonda haziendani. Wewe ni muungwana na mpenda haki na uhuru wa maoni. Huyu ananuka damu za watu aliowaua na anatamani na wewe umruhusu aanze kuteka na kuua.

Piga chini, muache na maisha yake maana hata Magufuli aliyemleta mwaka 2016 kama RC Dar alikuja akamchoka na akamtema mwaka 2020.
Mm pia siamini kama kuna mawaziri wanaweza kumtukana raisi wakiwa kwenye nafasi zao labda kama angesema MAWAZIRI walio tenguliwa. Lakini pia maoni yangu naona kama Makonda ndiye anaye sambaza kwa watu wajue kwamba raisi katukanwa. Mfano kama leo, alivyo ongea hivyo ata mimi binafsi nilikuwa sijui kama kuna jambo hilo so baada ya kusikia nikaanza kufuatilia.

Serikali ina mkono mrefu, chama cha CCM kina uongozi mpana sana, Kwanini Makonda asingepeleka kwenye vyombo husika alafu watu waka kamatwe kimia kimia badae jeshi la police litoe taarifa? sioni kama ni sahihi kusemea pale kwenye jukwaa. Lakini pia mheshimiwa raisi ni kiongozi mkuu anaestahili kuheshimiwa so suala la kumtukanwa ni kosa kubwa la jinai, halitakiwi kukemewa na makonda tu kwenye jukwaa na kusema eti mama yangu, yule ni kiongozi mkuu tulikemee wote ila kupitia njia sahihi siyo kwenye majukwaa kama alicho fanya makonda leo. Kwanza alichofanya makonda ata Jeshi la police tayari kaisha likosesha baadhi ya ushihidi maana watu waovu wa matusi wengine wataacha gafra kumbe ishu inge enda kimia kimia police wangekamata wengi tu.
 
Nitakuuliza majukumu ya mkuu wa mkoa, mwakilishi wa Rais na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa husika.
Sheria, protocol na hata history + mazoea, mkuu wa mkoa ni mouth piece na kitendea kazi cha Rais kwenye eneo husika.
Hakuna aliyehoji kwanini aliongea. Hakuna anayehoji aliyoongea kuhusu Mkoa wake.
Watu wanahoji katika Msiba wa Sokoine mbali na ya Mkoa wake, haya ya Mtandaoni yanaingiaje?
Hata kama yanaingia, hiyo si dhamana ya RC kwasababu hayakutoke katika Mkoa wake.

Fitna ni pale anaposhindwa kumweleza Rais aliyekaa naye anatangazia Umma jambo lisilo na ushahidi.
Yes halina ushahidi kwasababu matusi si jambo zito kuliko madawa ya kulevya! alishindwa huko.

Mimi kinachonistaajabisha kutoka kwako ni kumpa Salute ya ubingwa na ubobevu wa Fitna za kisiasa Paul Makonda, Salute ambayo ameishi na kudumu nayo Rais mstaafu Mzee Kikwete!
Hoja ni kwamba Jana wakati wa Msiba wa Sokoine aliyeanzisha sokomoko lisilohusiana na msiba ni DAB
Hata kama ni sehemu ya Fitnati, hoja ni ile aliyosema na wala hilo halitoi kinga kwa finnati wengine.
Mwizi ni yule aliyekamatwa na ngozi, si aliyeiba.
Tukivuta pumzi kidogo, tukumbushane chanzo/mwanzo wa Paul Makonda katika siasa za Tanzania.
UVCCM akiingizwa na Marehemu Sitta na kutumiwa na JK kumhujumu ELN
Alitambulishwa na nani rasmi katika mduara wa siasa za Kitaifa?
Nimejibu
Ni nani mwalimu/coach/mentor wake wa siasa za Kitaifa na siasa za JMT?
JPM ndiye aliyemkuza kutoka DC, kumpa u-RC na kisha nguvu za ajabu zisizo katika katiba kuliko VP na PM
JPM ndiye aliyempa nguvu za Fitna anayeoeneza leo.

Umesahau Fitna zake kwa Lowassa? alitumwa kwasababu ni Bingwa. Kila Fitna ikiwemo ile maarufu ya Dodoma huyu bwana anahusika. Madawa ya kulevya na akina Freeman Mbowe alitumwa asome na JPM kwasababu ni Bingwa.
Ni Bingwa kwasababu yeye ndiye mwenye uwezo wa kutenda au kunena uchafu bila haya au majuto.

Huyu ndiye alikuwa bega kwa bega na Mwanharakati huru kuleta Fitna kwa wenzake na wengine. umesahau

Umesahau bastola kichwani mwa Nape! Fitna ilianza kwa nani.

JokaKuu
 
Ni Samuel Sitta ndiye aliyem mentor Makonda kisiasa kwa kumuingiza kwenye bunge maalum la Katiba. Japo alimvua na ubingwa
Sasa, Samuel Sitta yeye alikua nani kwenye arena ya Siasa za JMT? Yeye Samuel Sitta ni nani alikua Master wake kwenye Siasa za JMT? Wakati wa uhai wake Siasa zake zilikua za mlengo upi ndani na nje ya Chama chake?

Hapo kwenye bold ulikuwepo wakati hilo jambo linatokea? Wewe ulikua nafasi gani, mshika miguu au mfuta jasho?
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
Isijekuwa kama kijana Zitto alipotishia kuwataja wauza sembe then ghafla akawa kimya mpaka leo hii,, anajipiga vidole tu na haeleweki.
 
Ukuu wa mkoa ,wilaya etc kuwe na job description na objectives za ku achieve vjnginevyo ndio kiwanda kikuu cha uchawa
 
Amani imetawala wana jf , popote mlipo

Rais ni nembo ya Taifa , kitendo cha kutukwanwa sihungi mkono ,nchi ni kubwa kuliko mtu mmoja .

Sasa na mimi kama Mtanzania natoa siku 5 Makonda kuwataja Mawaziri wanaoleta ujinga kumudhalilisha Rais pitia mitandao , na kama sio hivyo ikawa Makonda hajawataja na ushahidi juu, afutwe mara moja kwenye utumishi , wenda anajiona yupo na nguvu sana ila Taifa ni kubwa sana kuliko yeye.

Makonda asitualibie nchi ama kwa makudi au kugizwa ,

Nawakilisha
 
Raisi Samia huyu au mwingine, amtumbue Makonda? Utasubiri sana. Wenzako walishauliza maswali hivi Makonda anajiamini nini kwa Raisi Samia hadi anafikia kufanya yale anayofanya. Usione vinaelea huko ndani vilishaunganishwa siku nyingi
 
Usipende kupewa mualiko wa ikulu, wengi waliopewa mualiko wa kufika hapo walisahau kilichowapeleka hapo wakabaki kushangaa shangaa tu
 
Kumetokeni nini?
Makonda anasema wapo mawaziri wanalipa watu kumchafua rais na anawajua ,tunataka wapenda haki awataje na ushahidi ,nchi hii ni kubwa sana kuliko Makonda , na asipo fanya hivyo , moja atumbulie haraka sana , pili namtaka ulingoni tuzichape ,nchi haiwezi ruhusu wa namna hii
 
Hakuna aliyehoji kwanini aliongea. Hakuna anayehoji aliyoongea kuhusu Mkoa wake.
Watu wanahoji katika Msiba wa Sokoine mbali na ya Mkoa wake, haya ya Mtandaoni yanaingiaje?
Kwamba amewekewa masharti na mipaka ya wapi azungumze na wapi hasizungumze? Toka lini?
Hata kama yanaingia, hiyo si dhamana ya RC kwasababu hayakutoke katika Mkoa wake.
Hayakutokea katika mkoa wake… uhakika unao wa asilimia 100 kwamba wahusika anaowasena hawatoki mkoani kwake?

Fitna ni pale anaposhindwa kumweleza Rais aliyekaa naye anatangazia Umma jambo lisilo na ushahidi.
Vipi Kama anayoruhusa maalum ya kumwaga mafuta ya taa shimoni Kama hivi ili wajue kitakachotoka humo shimoni?

Halafu…
Una uhakika hana ushahidi wa aliyoyasema? Na Kama anao uliopasi na shaka itakuwaje?

Yes halina ushahidi kwasababu matusi si jambo zito kuliko madawa ya kulevya! alishindwa huko.
Kwamba alishindwa kwenye madawa? Kamishna kukabidhiwa file ndiyo kushindwa kwa Makonda?

Aliowataja ni wapi wamewahi kumshtaki kwa kuwadhalilisha na kuwasingizia?

Matusi sio jambo kubwa? Kwenye jamii yetu ni taboo kumtusi mtu mzima tena aliyekalia kiti cha Rais. Ni Sawa kuwatusi wote anaowaongoza.

Hoja ni kwamba Jana wakati wa Msiba wa Sokoine aliyeanzisha sokomoko lisilohusiana na msiba ni DAB
Ni sokomoko kwa mujibu wa nani?

Unafahamu kila linalozungumzwa na anaeshika mic eneo analokuwepo Rais na maafisa waandamizi wa Serikali linakua Lina baraka za kufanywa hivyo?

Hata kama ni sehemu ya Fitnati, hoja ni ile aliyosema na wala hilo halitoi kinga kwa finnati wengine.
Mwizi ni yule aliyekamatwa na ngozi, si aliyeiba.
???
UVCCM akiingizwa na Marehemu Sitta na kutumiwa na JK kumhujumu ELN
Samuel Sitta na Jakaya Kikwete.

Siasa zao katika ulingo wa siasa za JMT ni za aina gani?

Makonda ni mwanafunzi mzuri. 👏

Nimejibu

JPM ndiye aliyemkuza kutoka DC, kumpa u-RC na kisha nguvu za ajabu zisizo katika katiba kuliko VP na PM
JPM ndiye aliyempa nguvu za Fitna anayeoeneza leo.
Maajabu ni walio hai kushindana na wafu.

Kwamba nguvu ya marehemu Magufuli bado imesimama juu ya Siasa za JMT?
Unatania.

Umesahau Fitna zake kwa Lowassa? alitumwa kwasababu ni Bingwa.
Makonda kakuta tayari Lowassa kwenye politics hiyo 2014-2015 amekua loose ball ya kila mwenye msuli kujipigia, wafitini wa Edward wapo hai.

Kila Fitna ikiwemo ile maarufu ya Dodoma huyu bwana anahusika.
Hii naisubiri siku ya uthibitisho wake kwa hamu.

Madawa ya kulevya na akina Freeman Mbowe alitumwa asome na JPM kwasababu ni Bingwa.
Kama aliyoyasema kwa hao wote kuhusu madawa ya kulevya ni uwongo na Fitna, wanasubiri nini kumfungulia mashtaka ya udhalilishaji angalau to set records straight?

Ni Bingwa kwasababu yeye ndiye mwenye uwezo wa kutenda au kunena uchafu bila haya au majuto.
Acha utani Nguruvi! Magwiji wa hizo kazi wapo wanakusoma hapa.

Huyu ndiye alikuwa bega kwa bega na Mwanharakati huru kuleta Fitna kwa wenzake na wengine. umesahau
Sijasahau.

Binafsi niliwaelewa kipindi kile, waliamua kucheza ngoma iliyopigwa wakati ule, kwenda sambamba na beat. Sio kosa, akuanzaye mmalize.

Umesahau bastola kichwani mwa Nape! Fitna ilianza kwa nani.
Kwamba Makonda ndio alishika bastola kichwani kwa Nape?

Mzee Jakaya alizuia vipi Mihemko ya yule askari aliemlipulia bomu la machozi tumboni yule mwandishi wa Habari wa channel Ten?

Usiku wa deni haukawii kucha. Ilikuwa siku, ikawa masaa na sasa jumatatu imewadia.

Nikicheki mitandaoni naona bado mitusi dhidi ya mama inatrend.

Makonda a.k.a jasiri asiye na asili, tunakutaka uwataje mawaziri wanaowalipa hao wanaomtukana "mama yako" mitandaoni.
 
Sasa, Samuel Sitta yeye alikua nani kwenye arena ya Siasa za JMT? Yeye Samuel Sitta ni nani alikua Master wake kwenye Siasa za JMT? Wakati wa uhai wake Siasa zake zilikua za mlengo upi ndani na nje ya Chama chake?

Hapo kwenye bold ulikuwepo wakati hilo jambo linatokea? Wewe ulikua nafasi gani, mshika miguu au mfuta jasho?
Mpumbavu wewe kaa kimya. Mjini umekuja juzi toka Kolomije unauliza maswali ya kipimbi
 
Back
Top Bottom