Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Makonda anajisahau, anadhani yeye bado ni Katibu wa Itikadi na Uenezi (propaganda).
 
Hakuna waziri anafanya hicho kitu bali Makonda anatafuta namna ya kuwapaka shombo mawaziri ambao hana mahusiano nao mazuri kama; Nape Nnauye, Januari Makamba, Hussein Bashe, Riz 1 Kikwette.

Kupata uwaziri ndiyo ndoto ya wabunge wengi baada ya uchaguzi. Rais Samia amekupa Uwaziri, unaanzaje kulipa watu wamtukane mtu alikupa Uwaziri ambayo ni privilege adimu?

Yaani huyu Makonda anaweza kuwa na TAARIFA za ndani kuliko TISS wenye kazi yao?

Kama ambavyo akiwa Mwenezi wa CCM hakujua majukumu yake, huku nako kwenye u RC wa Arusha bado Makonda hajui kazi yake.

USHAURI KWA RAIS SAMIA:
Chonde chonde Rais Samia USIINGIE mtego huu wa Makonda. Huyu NI ZEROBRAIN atakuharibia uRais wako.

Haiba yako Rais Samia na ya Makonda haziendani. Wewe ni muungwana na mpenda haki na uhuru wa maoni. Huyu ananuka damu za watu aliowaua na anatamani na wewe umruhusu aanze kuteka na kuua.

Piga chini, muache na maisha yake maana hata Magufuli aliyemleta mwaka 2016 kama RC Dar alikuja akamchoka na akamtema mwaka 2020.
 
cheki sasa hapo hao mawaziri wamepewa muda gani wa kuacha tabia ya kumchafua Rais mitandaoni. Tarehe 11 hadi 14/4/2024., sasa ndani ya hizo siku mbili atajua kuwa wameacha ama la?!


Afrika kuna mahali tuliharibu, kisha tukaharibikiwa


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Tapeli huyo, Hana uwezo huo maana wakati kigogo anamtukana Magufuli walijifanya pia wanamjua, na haikuwa kweli.
 
Hana lolote mpiga kelele tu Huyo. Leo Ijumaa na spana shidi ya bebi wake zitaendelea mtindo mmoja.
 
anatafta mbeleko hanalolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…