Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Hutu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati
Pumbavu zako Makonda! Kwani hufahamu mahali pa kutoa taarifa au na wewe unatafuta umaarufu wa mitandaoni!

Kutwa kucha kuchongea na kuwabamnikizia makosa wenzako!
msaka umaarufu tu huyu , mama atajutia sana kosa la kumrudisha huyu jamaaa …
 
Hiyo inauhusiano gani na umkuu wa mkoa Arusha.
Hajakubali Ukuu wa Mkoa, hata mimi ningekataa. Wamemtoa uraiani kwenda kuwa mwenezi kuiokoa a failing Samia administrion, ghafla wanamrusha Arusha makusudi akatulize Wamasai wanaohamishwa kupisha vitalu vya Waarab, na akajibizane na Godbless Lema, hell no.... kasema kwenye inaugural speech yake he ain't doing all that dumb crap.

Paul Makonda ni mkubwa kuliko Ukuu wa Mkoa, way bigger than kujibizana na mpinzani Arusha. And when the whole nation is watching Makonda hawezi kusimama kuongelea matundu ya vyoo vya wasichana Monduli...

He was the right hand man of Magufuli administration, he harbors state secrets, he knows where the bodies are burried. He has information the president doesn't. CDF Mabeyo alimwambia rais mpya msiba ukiisha nitafute nianze kukupa state secrets. She had been kept in the dark all along, clueless. Na juzi CDF Mabeyo karudia tena, kasema Vice President Samia did not have the faintest clue the president was dying... Walimwita Askofu Pengo kabla ya Vice President. Likewise, kama Mkuu wa Kamati ya Uinzi na Usalama D'Salaam, Paul Makonda had better access and security clearance to state secrets than the former Vice President, and he still knows more!

Na wakimfirigisa ndani ya CCM anaingia mtaani yeye kama yeye! Edward Lowassa 2 point O. It won't be the same this time around, yule Mzee alikuwa slowed down by Alzheimer's, kutembea mpaka ashikiliwe anasumbuliwa na Rheumatoid Arthritis, couldn't read a speech to save his life, sijui Parkison's Desease, Multiple Sclerosis and all the rest of it. Paul Makonda has fresh legs and a chip on his shoulder, you don't wanna go down that road with him!
 
Aisee hatari sana,hela za kutengeneza barabara anaombwa Rais au zinatoka serikalini?Kodi?
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Ndugu zangu Watanzania,

Kauli iliyotolewa na Mwamba Mwenyewe Paul Christian Makonda ni nzito kwelikweli,imeitetemesha nchi,imeleta sintofahamu kwa wananchi ,imeleta amsha amsha na kila mtu na neno lake.ni kauli ambayo imeacha maswali mengi kila mtu na majibu yake.kila mtu anawaza ni akina nani hao wanaomhujumu Rais wetu na nini dhamira yao.kwanini walipe watu kwa ajili ya kumtukana Mheshimiwa Mitandaoni? Dhumuni lao wanataka nini? Wanataka Rais Samia akichafuka kwa matusi wao wapate nini? Wana malengo gani?

Nini malengo yao baada ya kuwa Rais ametukanwa sana? Wanataka wampindue Rais uchaguzi ujao? Wanataka kumhujumu? Kwanini wamhujumu? Je ikiwa hao watu wataacha kuwalipa kuwalipa hao watu wanomtukana Mheshimiwa Rais mitandaoni,unafikiri ni njia ipi ya pili au mipango gani mingine watafanya kuendelea kumuhujumu Mheshimiwa Rais? Je ndio utakuwa mwisho wa wao kuachana na mipango wao ovu? Je usalama wa Rais upo kiasi gani kwa yeye kuendelea kuwa na kufaya kazi na watu ambao amewaamini lakini wao wameshindwa kuwa waaminifu kwake mpaka kufikia kulipa watu pesa ili Rais atukanwe na kuhujumiwa kupitia mitandao? Je watu hawa ni vipi wanaweza kufanya kazi kwa weledi wakati hawampendi Rais? Ni vipi wanaweza kutunza siri za baraza la mawaziri? Ni vipi wanaweza shindwa kuvujisha siri za vikao?

Kauli hiyo ni muhimu vyombo vyetu vya usalama kuifanyia kazi kauli hiyo na kumshauri Mheshimiwa Rais kufanya maamuzi ya haraka.maana haiwezekani Mh Rais awe na watu ambao hawapo pamoja,hawana mawazo ya pamoja.ni hatari sana.kwa sababu watu hao watatoa na kuvujisha siri zote za baraza la mawaziri,watavujisha nyaraka za serikali,watavujisha mipango na mikakati yote ya serikali,watamhujumu Rais na serikali yake na nchi kwa ujumla.watafaya kazi chini ya viwango ili Rais alaumiwe na kutukanwa zaidi na zaidi.watafanya maamuzi na kutoa kauli zitakazokuwa zinajenga chuki na kuichongaisha serikali na wananchi.watafanya kila linalowezekana ili Rais Samia aendelee kuchukiwa zaidi na zaidi.

Huwezi ukalala na nyoka ndani na ukasema nyoka hatakuwa na madhara kwako kwa sababu tu unalala juu ya kitanda.kwahakika utakuwa unajidangamya. Nyoka mmoja aliye ndani ya nyumba yako ni hatari zaidi kuliko koboka aliye nje pamoja na Kundi la Simba walio nyuma ya nyumba yako.kama kuna nyoka ndani ni bora upambane kumtoa haraka sana ili ndani kuwe na amani na usalama.

Kauli ya Mheshimiwa Makonda siyo ya bahati mbaya na haiwezi kutolewa kwa bahati mbaya wala kisiasa.hivyo naamini anafahamu anachokizungumza na alichozungumza na mawaziri wanaomhujumu Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais hawezi kufanya kazi na kuwa pamoja na watu ambao viapo vyao wameshavisigina na kuingia kazini kumhujumu. Ni lazima hatua zichukuliwe haraka ili kujenga imani na kuaminiana ndani ya baraza.hakunaga jambo dogo na la bahati mbaya katika siasa. Ni hatari sana kuendelea kuishi na shetani kwa matarajio kuwa atabadilika na kuwa malaika mkuu.chui hata aloane hawezi kubadilika na kuwa kondoo wala nyoka akijivua gamba habadiliki na kupunguza sumu yake.atabaki kuwa nyoka yule yule mwenye sumu ile ile na tabia zile zile za nyoka.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Mkuu kuwa na maneno ya Akiba. Pili kuwa mwangalifu maana nyumba uliyomo ni kioo, usirushe mawe!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine

Mambo ya madawa ya kulevya yamerudi😂
 
Kama anabisha kuna kwenye mtandao wa X kuna kundi ambalo linaongozwa wa Waziri fulani na kuwalipa watu wamtukane Rais lengo lao kubwa Mama achafuke ili asigombee 2025 ili team yao iingie!
Mkuu si ulitaje hilo kundi tulijue hapa, bila hivyo ni uongo tu kama uongo mwingine mpaka uutibhitishe.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli

=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
Sidhani kama hii ndio mojawapo ya kazi ya Ukuu wa mkoa.
Tanzania kila mtu anataka kujipendekeza kwa rais yani kila mtu anajifanya ana mapenzi makubwa kwa rais badala ya kufanya kazi zake.
 
Hajakubali Ukuu wa Mkoa, hata mimi ningekataa. Wamemtoa uraiani kuwa mwenezi kuiokoa Samia administrion, ghafla wanamrusha Arusha makusudi akajibizane na Godbless Lema, hell no.... he ain't doing all that dumb crap.

Paul Makonda ni mkubwa kuliko Ukuu wa Mkoa, way bigger than kujibizana na mpinzani Arusha. And when the whole nation is watching Makonda hawezi kusimama kuongelea matundu ya vyoo vya wasichana Monduli...

He was the right hand man of Magufuli administration, he harbors state secrets, he knows where the bodies are burried. He has secrets the president doesn't. CDF Mabeyo alimwambia rais mpya msiba wa Magufuli ukiisha nitafute nianze kukupa state secrets. She had been kept in the dark all along, a deer in the headlight. Na juzi CDF Mabeyo karudia kusema Vice President Samia did not have the faintest clue the president was dying.... Walimwita Askofu Pengo kabla ya Vice President. Likewise, Mkuu wa Kamati ya Usalama D'Salaam, Paul Makonda, had better access to state secrets than the former Vice President, and he still does.

Na wakimfirigisa ndani ya CCM anaingia mtaani yeye kama yeye! Edward Lowassa 2 point O. It won't be the same this time around, yule Mzee alikuwa slowed down by Alzeihmers, kutembea mpaka ashikiliwe anasumbuliwa na Arthirist, couldn't read a speech to save his life, sijui Parkison's Desease, Multiple Sclerosis and all the rest of it. Paul Makonda has fresh legs and a chip on his shoulder, you don't wanna go down that road!
umeeleza vizur mkuu.

Naomba nikusahihishe kidogo. wakati JPM anafariki huyu jamaa hakuwa RC wa DSM. Si unakumbuka 2020 baada ya kushindwa kura za maoni za ubunge wa Kigamboni alitemwa.

Wakati JPM anatangulia mbele za haki, mtu aliyekuwa RC wa DSM ni Kunenge.
 
Hakuna waziri anafanya hicho kitu bali Makonda anatafuta namna ya kuwapaka shombo mawaziri ambao hana mahusiano nao mazuri kama; Nape Nnauye, Januari Makamba, Hussein Bashe, Riz 1 Kikwette.

Kupata uwaziri ndiyo ndoto ya wabunge wengi baada ya uchaguzi. Rais Samia amekupa Uwaziri, unaanzaje kulipa watu wamtukane mtu alikupa Uwaziri ambayo ni privilege adimu?

Yaani huyu Makonda anaweza kuwa na TAARIFA za ndani kuliko TISS wenye kazi yao?

Kama ambavyo akiwa Mwenezi wa CCM hakujua majukumu yake, huku nako kwenye u RC wa Arusha bado Makonda hajui kazi yake.

USHAURI KWA RAIS SAMIA:
Chonde chonde Rais Samia USIINGIE mtego huu wa Makonda. Huyu NI ZEROBRAIN atakuharibia uRais wako.

Haiba yako Rais Samia na ya Makonda haziendani. Wewe ni muungwana na mpenda haki na uhuru wa maoni. Huyu ananuka damu za watu aliowaua na anatamani na wewe umruhusu aanze kuteka na kuua.

Piga chini, muache na maisha yake maana hata Magufuli aliyemleta mwaka 2016 kama RC Dar alikuja akamchoka na akamtema mwaka 2020.
Huyu mbona anaongea kama Waziri Nepi!
 
Back
Top Bottom