Uchaguzi 2020 Paul Makonda, hawezi kupita Kigamboni kura za Maoni

Uchaguzi 2020 Paul Makonda, hawezi kupita Kigamboni kura za Maoni

Uliongea point watu wakabeza
Binafsi ninaamini Bashite hawezi kutoboa Kigamboni. Liwe jua, iwe mvua, sioni akipenya kwenye kura za maoni za CCM.

Kwa watu msiofahamu tu, viongozi wengi wa CCM Dar na wanaCCM walikuwa wanamchukia Makonda kuliko hata mpinzani. Ukuu wa mkoa ulimfanya Makonda awaone watu wengine wote ni wapuuzi, wajinga na wapumbavu.

Muda ndio huu.
Makada waamue sasa.
 
Watumishi wa umma mateso ya miaka 5 ya hakuna increments, kupanda vyeo (walimu),ongezeko la mshahara,kutolipwa malimbikizo yenu n.k iwe ni fundisho na akili zenu kuikataa ccm kwa nguvu zote.Familia zenu ziikatae ccm.

Msiwapigie kura ya urais,wabunge wala madiwani.Ndiyo wadhalilishaji wenu
 
Nadhani kilichotokea ni kuwa baada ya makonda kuota mapembe na kumchukulia poa kila kiongozi awe wa chama au serikali isipokuwa rais tu karibu kila mtu alimchoka na wengi kumchukia. Aliendelea kuwa alipo kutokana na kushikiliwa na rais tu ila sasa kajichanganya kaamua kumchukulia poa rais pia kwa kuondoka kwenye nafasi aliyomuweka. So hata rais anaweza kuwa na mapenzi ya ndani kwa mtu lakini pia hua anajali sana maoni ya walio wengi kuepusha sintofaham za baadae. Wengine wanaweza kuwa waliondoka kwenye nafasi walizopewa ila hawakuwaudhi wengi kwahiyo hata ukimpa nafasi tena haiwaumizi wengi.



Lakini pia niliwahi kufikiria scenario flani kwamba kwa makonda alipokuwa amefikia alikuwa kamuudhi kila mtu hadi rais ila kwa jinsi rais alivo hana tabia ya kufanya maamuzi kwa kushinikizwa na mtu ilibidi Makonda atengenezewe mtego ale ndoano wamnyoe. Umeshanichosha, kukutumbua direct itaonekana nafanyia kazi maagizo ya mange kimambi na kigogo so nakutafutia wajanja wakujaze upepo kuwa ulipo ni padogo so kagombee ubunge na kwa kuwa unaamini nina kukubali sana unajihakikishia kushinda. Unachukua form natoa maelekezo upigwe spana katika level zote movie linaisha steringi umefia kwenye maua na lawama kubwa zinaenda kwa wajumbe sio mimi nilieaminiwa ni baba yako.



By the way bado muda upo na mengi yanaweza kutokea so tuwe na akiba ya maneno
 
Back
Top Bottom