Paul Makonda kufikishwa Mahakamani Februari 3, 2022 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka

Paul Makonda kufikishwa Mahakamani Februari 3, 2022 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka

Hamna kitu hapo,Clouds walishakataa wasihusishwe kwenye hiyo kesi.
 
Hivi jinai mshtakiwa anaombwa kufika mahakamani tarehe tajwa au anatakiwa atokee mahabusu ndani ya karandinga? Sijaelewa.
Ndo mana nasema hamna kesi hapo, kesi kama hiyo ingekua na maana kama angeshitakiwa na jamhuri sio mtu binafsi
 
Ama kweli ukipenda chongo utaona kengeza tu. Yaani uhalifu uliofanyika clouds kila mtu aliuona na tume iliyoundwa kuchunguza ikaja na majibu kwa Makonda kuhusika bado huoni ni jinai?

Kwakweli kuna baadhi ya watu mna asili ya ubishi unaweza kusema kubisha kwamba Dodoma haipo Tanzania na ukaamini hivyo wakati unajua kabisa ipo Tanzania.
We jamaa una kichwa kizito sana. Ulikua unajua uhusiano wa Makonda na Clouds before hizo Propaganda za uvamiz?Nape kama Waziri ana mamlaka gani ya kuunda tume ya kumchunguza RC?RC anawajibika kwa Rais, Waziri ni mamlaka ya uteuzi ya RC?Usinchukulie makonda kama makonda, mchukulie Makonda kama RC.Waziri hana mamlaka ya kunchunguza RC hili weka KICHWANI.
 
Kwa kushitakiwa na kubenea?

Ingekua jamhuri, hapo mtu unaweza kuwaza!

Vipi clouds wakigoma kutoa ushirikiano! mutawalazimisha?

Maana huo ndio ushahidi pekee kila mjinga anashabikia!

Kuhusu mauaji hata USA wameshindwa kutoa ushahidi!

Clouds hawawezi kukwepa kutoa ushahidi wakihitajika kisheria. Wanapigwa subpoena.

US hawakudaiwa ushahidi. Haikuwa kesi bali uamuzi wao wa kidiplomasia na masuala ya uhamiaji.
 
Wanasheria hebu mtusaidie. Kwa mujibu wa habari hii Makonda amefunguliwa makosa ya jinai.

Swali: Mtu anapokuwa na makosa ya jinai, anaitwa mahakamani kutokea nyumbani kwake bila kwanza jambo hilo kuhusisha vyombo vya dola, kwa maana ya mhusika kukamatwa, kuhojiwa na kisha ndipo anafikishwa mahakamani?
 
Itumike busara ili isijeonekana kama kulipizana visasi.
La msingi ni kupima kwanza mazuri aliyofanya na mabaya yake ili upatikane uzani.
Na kama uzani utabalance ni mara mia kupotezea kwa kutoa tahadhali/notification kwa mamlaka za uteuzi kufanya review/kuangalia upya vigezo vya uteuzi/vetting ili baadae yasijirudie makosa mengine ya utendaji kwa wateuliwa.

Mizani? Inapimaje? Kosa moja la kuua na zuri moja la kulipia mtu operesheni ya moyo yana tofauti au mlingano wa kilo ngapi?
 
Ni aibu kwa taifa,viongozi kwa Mihimili kutokujitegea.na kufuata sheria.hii yote ni katiba kuwapa ma DC na na RC ukuu wa usalama kwenye maeneo yao inawafanya waendeshwe na wanasiasa badala ya sheria.ndio zao la usalama wa ccm,policcm na tayari mahakaccm.tz yaitaji maombi
 
ALIYEKUWA Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Paul Christian Makonda, sasa ameamriwa kufika mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kinondoni, Dar es Salaam, tarehe 3 Februari 2022, kujibu mashitaka ya jinai yanayomkabili.l

Taarifa kutoka Mahakama hapo na ambazo zimethibitishwa na mwandishi wa habari mwandamizi, Saed Kubenea, ambaye ndiye aliyefungua shauri hilo zinasema, tayari mhimili huo umetamtaka Makonda kufika siku hiyo.

Katika kesi hiyo ambayo imevuta hisia za wengi na kuibua mjadala mzito kila kona ya nchi hususani katika mitandao ya kijamii, Kubenea anamtuhumu Makonda kwa makosa mbalimbali.

Miongoni mwa makosa hayo, ni matumizi mabaya ya madaraka ya umma, wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kesi dhidi ya Makonda, imesajiliwa mahakamani kama Miscellaneous Criminal Application Na. 1 ya mwaka 2022 na imepangwa kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi, Aron Lyamuya.

“Ni kweli kwamba kesi tayari imesajiliwa na kupangiwa hakimu wa kuisikiliza na kwamba, Mahakama imetoa amri (summons), inayomtaka Bwana Makonda kufika mahakamani, Februari 3 mwaka huu,” ameeleza Kubenea

Katika kesi hiyo, Kubenea anawakilishwa jopo la mawakili wakiongozwa na Nyaronyo Mwita Kicheere na Hekima Mwasipu.

Kupatikana kwa taarifa hizi kunakuja siku tatu, baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imeziagiza Mahakama za Kinondoni na Kisutu, kufungua shauri la jinai dhidi ya Makonda.

Mahakama ilitoa maelekezo hayo, baada ya Kubenea kuandika barua ya malalamiko kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, akisema Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Kinondoni, zimegoma kufungua kesi yake.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Joseph Luambano, Januari 14 mwaka huu, ni kwamba Kubenea “anayo haki ya kufungua shauri hilo la jinai, iwapo anataka kufanya hivyo.”

Kabla ya hatua hiyo, Kubenea alikuwa amefungua shauri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni na kusajiliwa kama – Miscellaneous Criminal Application No. 7/2021 – akiomba kuruhusiwa kumshitaki Makonda.

Aidha, Desemba 3 mwaka jana, akawasilisha maombi Mahakamani ili kuondoa shauri lake, kwa ajili ya kufanyia marekebisho baadhi ya maeneo, jambo ambalo Mahakama ililikubali; lakini katika mazingira ya kutatanisha, baadaye Mahakama hiyo hiyo, ikagoma kupokea kesi hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Makonda anadaiwa kuwa siku ya tarehe 17 Machi 2017, akiwa na watu waliobeba silaha za moto, alivamia Clouds TV na kumuagiza mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu kurusha video inayomwonesha mwanamke aliyejulikana kwa jina la Grace Athuman.

Katika video hiyo, ambayo haijulikani nani ameiandaa, mwanamke huyo alidaiwa kuonekana akifanya tendo la ndoa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Kwa mujibu wa ushahidi wa video za CCTV, Makonda anaonekana kuvamia kituo cha Clouds saa nne usiku, akiwa anaendesha mwenyewe gari namba T553BFM.

Vilevile, Camera za CCTV pamoja na kitabu cha kumbukumbu za walinzi, vinamuonesha Makonda aliingia Clouds akiwa na askari wanne waliokuwa na sare tofauti za majeshi ya ulinzi na usalama, kati yao watatu wakiwa na silaha za moto.

Askari hao waliingia hadi chumba cha utangazaji, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za utangazaji, huku Makonda akitumia vitisho dhidi ya wafanyakazi wa Clouds kwa kutumia silaha za moto.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo ya Kubenea, kitendo cha Makonda cha kuvamia televisheni ya Clouds, tena akiwa ameongozana na askari waliobeba silaha za moto, ni kinyume cha sheria ya Kieletroniki na Posta ya mwaka 2010.

Maombi ya kutaka kumshitaki Makonda yamewasilishwa mahakamani, chini ya kifungu cha 99 (1) cha Sheria ya mwenendo wa mashauri ya Jinai, Sura ya 20.

Kubenea ambaye amewahi kuwa mbunge wa Ubungo (Chadema), katika Bunge lililopita anasema, hatua ya Makonda kuvamia Clouds, ni matumizi mabaya ya madaraka, chini ya kifungu cha 96 ya Kanuni ya adhabu (Penal Code), Sura ya 20 na kuingilia moja kwa moja, mawasiliano ya Kieletroniki.

Mbali na Makonda, wengine walioitwa mahakamani siku hiyo, ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Wawili hawa wanadaiwa wameshindwa kuchukua za kumfungulia mashitaka ya jinai mtuhumiwa huyo.

Maombi ya kumshitaki Makonda yameambatanishwa na wito maalum (Chamber Summons) na hati ya kiapo (Charge Sheet).

Katika kujenga hoja yake mahakamani, wakili wa Kubenea ameambatanisha ripoti ya uchunguzi ya Kamati Maalum iliyoundwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye.

Ripoti ya Nape iliyochunguza tukio la kuvamiwa Clouds, ilimtia hatiani Makonda na kupendekeza kwa mamlaka yake ya uteuzi, kumchukulia hatua za kinidhamu; Makonda mwenyewe kuwajibika binafsi na kuwaomba radhi Clouds na wananchi kwa ujumla.

Hata hivyo, mapendekezo yote ya Kamati ya Serikali hayakutekelezwa. Muda mfupi baada ya Nape kumaliza kusoma ripoti yake kwa waandishi wa habari, Rais John Magufuli alitangaza kumfuta kazi.

Nape alirejea kwenye baraza la mawaziri wiki iliyopita, kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alishika madaraka ya urais baada ya kifo cha Magufuli, kuamua kumrejesha katika wizara hiyo.

Kamati ya Nape ilithibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho cha televisheni akiwa anaendesha mwenyewe gari lenye namba T553 BFM na kuingia hadi chumba cha utangaji, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za utangazaji.

Tangu kuripotiwa kufunguliwa kwa shauri dhidi ya Makonda, kumekuwa na matukio mbalimbali yanayojitokeza. Katika gazeti la Jumatano iliyopita, wakili mwingine wa kujitegemea, Peter Madeleka, alinukuliwa akisema, yuko tayari kujiunga na mawakili wengine watakaoteuliwa na Kubenea, kuendesha kesi hiyo.

Madeleka ambaye alikuwa ofisa wa Jeshi la Polisi alisema, anataka kutumia ujuzi wake wa kisheria na kiuchunguzi, kuendesha kesi hiyo aliyoita, “imebeba maslahi ya taifa.”

“Lengo siyo kushinda tu. Kesi hii, inalenga kuzionyesha mamlaka za kuendesha mashitaka ya Jinai (DPP), kwamba kuna mtuhumiwa mmoja anastahili kuburuzwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili. Lakini hawajaweza kufanya hivyo na kunyamaza kwao, ni kuvunja Ibara ya 59 (B) Ibara ndogo ya (4) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” ameeleza Madeleka.

Alisema, “ikumbukwe kuwa hata mataifa makubwa kama Marekani, yamewahi kumuwekea vikwazo vya kwenda nchini humo Makonda na familia yake, kutokana na tuhuma za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

“Pamoja na Marekani kuwa taifa mshirika na Tanzania kwenye mambo kadhaa kihistoria, pamoja na uwezo wa Marekani kuweza kutambua mambo mbalimbali yanayotokea duniani, lakini serikali imeshindwa kufanyia kazi taarifa ya Marekani kuhusiana na matendo ya Makonda.”

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, 31 Januari 2020, ilieleza kuwa serikali ya nchi hiyo, imempiga marufuku Makonda na mke wake, Mary Massenge, kufuatia tuhuma za ukandamizaji wa haki za wananchi; kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na usalama wa watu.

“Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki kupitia nafasi yake kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Michael Pompeo alitumia mtandao wake wa Twitter kutangaza marufuku hiyo.

Alisema, “…leo tumetangaza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Christian Makonda, hataruhusiwa kuingia Marekani, kutokana na kushiriki kwake katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.”
Watanzania wengi tunapotea kwa kukoswa maarifa. Mfano taarifa hii ya telegram ina uwalakini ndani yake na katika comments nilizopitia sijaona aliyetaka uthibitisho na usahihi wa habari hii. Ukisoma shauri lenyewe, kama taarifa ya telegram inavyoonesha, limesajiliwa kama ‘criminal application’ sasa mtu hataki hata kujiuliza kwa nini haijasajiliwa kama ‘criminal case.’

Kumbukeni msemo kuwa ‘wajinga ndiyo waliwao.’
 
We jamaa una kichwa kizito sana. Ulikua unajua uhusiano wa Makonda na Clouds before hizo Propaganda za uvamiz?Nape kama Waziri ana mamlaka gani ya kuunda tume ya kumchunguza RC?RC anawajibika kwa Rais, Waziri ni mamlaka ya uteuzi ya RC?Usinchukulie makonda kama makonda, mchukulie Makonda kama RC.Waziri hana mamlaka ya kunchunguza RC hili weka KICHWANI.

Mfungwa sabaya naye si alisema hivyo hivyo kwamba anawajibika kwa mamlaka yake ya uteuzi ila akalamba miaka 30.
Sasa kwa taarifa nape karudishwa wizarani ripoti yake ipo huyo matako makonda ni raia tu.
Mwambia ajiande kwa maisha aliyojiandalia kama ya sabaya
 
Ungeacha kupapatika kama kuku asie na kichwa ungeona niliandika kama serikali ikiamua kufungua criminal case sawa.

Kama Clouds media ikiamua kumfungulia civil case pia sawa.

Kubenea hana sifa ya kufungua criminal case kwa sababu ni serikali tu ndio inayoweza fungua hizo case.

Na kubenea awezi fungua civil case ya Clouds kwa sababu claimant/plaintiff kwanza kabisa kabla mahakama aijasikiliza case lazima athibitishe uhusiano wake na tukio. Pamoja na madhara ya action kwake yeye.

Sio kila mpuuzi anaweza kwenda kufungua civil dispute ya mambo yasiyo muhusu.

Huu upuuzi inabidi uangaliwe kuna watu wanasubiri miaka case zao azijasikilizwa alikadhalika mahakama ina entertain wapuuzi kama Kubenea na Mbatia.
Taga linalia Lia ka chizih.
 
Taga linalia Lia ka chizih.
16EBD0CB-7D6A-4734-9CC7-60996E1F4636.jpeg


Here are the facts about the universe I am sure you don’t know about.
..................................

Jua kumbe alipo still na lenyewe linazunguka galaxy kwa speed ya kilometre 210 kwa sekunde. Galactic year for the sun ni sawa na miaka 230 ya dunia.

Kwa maana hiyo sasa dunia, sayari zote na kila celestial body ndani ya solar system vinalikimbiza jua kwa speed yake 210km/second.

Hapo hizo celestial bodies linaizunguka jua; dunia kwa mfano inatumia siku 365 na kwenye kufanya ivyo inaenda 67000 miles per hour, hapo hapo tena dunia inazunguka katika mhimili wake 1000m/h (wewe unaishi kwenye surface ya dunia wala uoni kitu).

Halafu kuna masela huko NASA kwa kutumia law of physics and applied mathematics modelling wanatengeneza chombo kinaitwa ‘Parker Solar Probe’ jamaa kwa hesabu zao wanakwambia hiko chombo wakitaka kifike karibu na jua haraka wakipeleke kwanza Jupiter na kutumia magnetic fields zake kitakipeleka mapema zaidi kuliko kwenda moja kwa moja through Venus and all that requires timing,

Kifaa kinaruka kinakwenda mpaka Jupiter na kweli kinapelekwa mpaka wanapotaka siku zile zile zilizopangwa. Kinanasa kwenye gravity ya jua kama walivyopanga, wanakifungua wakati wapo million miles apart, kina record; all that just to learn about the outer core of the sun solar flares (not sure ata unajua impact zake kwa dunia ili wachukue tahadhari).
............. ............

What’s the point of all that, there are so many things to amuse the mind with kuliko uthenge mnaojaza kwenye vichwa vyenu yaani binafsi inanisikitisha how is it possible kuna binadamu wapo so shallow minded.

I don’t understand yaani mtu unapata wapi muda wa kuangaika na binadamu mwingine, seriously. Ama kweli akili ni nywele na kila mtu na zake.
 
We jamaa una kichwa kizito sana. Ulikua unajua uhusiano wa Makonda na Clouds before hizo Propaganda za uvamiz?Nape kama Waziri ana mamlaka gani ya kuunda tume ya kumchunguza RC?RC anawajibika kwa Rais, Waziri ni mamlaka ya uteuzi ya RC?Usinchukulie makonda kama makonda, mchukulie Makonda kama RC.Waziri hana mamlaka ya kunchunguza RC hili weka KICHWANI.
Kwa hiyo ukiwa RC kwa tanzania unaweza ukawa unabaka kabisa na kuua alafu hakuna mamlaka inaweza kukufanya kitu???[emoji3][emoji3][emoji3][emoji846]
 
Back
Top Bottom