Paul Makonda: Kuna makundi matano yanataka kuniua, likiwemo wanaotafuta kulipa kisasi kwa Wasaidizi wa Magufuli

Hii ni mbinu ya kutafuta huruma na kutaka kuwafanya watu wasahau madhambi yake hasa ufisadi aliofanya wa kupora mali za watu.
Someone help me please. Hiyo post ya insta kama imeandikwa na mwanafunzi wa kidato cha pili.

Eti kina nikilefu! Alipenya vipi hadi ukuu wa mkoa?!
 
Nashangaa huko Takukuru, hizi kesi zipo wazi ila wanachelewa kuzifungua, Matumizi mabaya ya Madaraka, Kujipatia Mali Kwa njia ya udanganyifu, Kumiliki Mali zaidi ya Kipato chako, Sasa wanasubiri nini!?
Sijui kwanini linacheleweshwa!
 

Makonda tangu akataliwe kigamboni hayuko vizuri. Halafu yet mbona ameiba Sana pesa.
 
hahahahaha wanamfinya kimyakimya, Makonda le' general......unawalalamikia wauza unga tena, kwani rafiki yako Kinje na yule mrangi pale SA wanasemaje.... Hivi akiendaga SA pale midland anafikiaga kwa nani?..

Le' general kaa kimya tu na jaribu kuwa mtulivu, wale macow boy wanafaili lako lenye kila kitu, ukijitingisha tu wanawewe, huwa hawasahau wale....
 
Damu za wale alioua zinaanza kumuwehusha hana lolote huyo
 
Kuna tuhumu kama hizi:-

-Kujaribu kumdhuru lissu
-kumtegea sumu ruge

Ila watu ndivyo wanavyosema kwenye mitandao ya kijamiii.... Ila ukweli unaujua wewe na Mungu mwenyezi. Ila kama kweli unahusika na hayo basi huna uhalali wa kulalama ivooo subiri unyolewe. Ila kama hizo tuhuma hazikuhusu basi huna baya RELAX Mungu atakupigania maana una mazuriii mengi ila mazuri hayo hata kama yatakuwa mengi kiasi gani bado roho za watu zina thamani kubwaaa sanaaa

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani angekaa kimya japo nahisi inawezekana kuna jambo analiona linakuja kumletea madhara si muda ndiyo maana amewahi kutafuta public sympathy
Huyu mtu siyo wa kuachwa hata kidogo. Alitenda madhambi mengi mno. BTW mtu ukiambiwa Makonda aliyekuwa na mkoa anaouita wake tena akafikia hatua ya kukataza baadhi ya watu kuingia kwenye ''mkoa wake'' ndiye anayelia namna hii huwezi kuamini.
 
Nimejiuliza sana mahoga wanaua kwa kutumia nini
 
Someone help me please. Hiyo post ya insta kama imeandikwa na mwanafunzi wa kidato cha pili.

Eti kina nikilefu! Alipenya vipi hadi ukuu wa mkoa?!
Mkuu hivi ulikuwa unadhani Makonda kichwani zimo kielimu? Hakuna kitu na kila mtu alikuwa anashangaa aliwezaje kuwa juu ya watu wengi namna ile. Ila sisi watanzania pia tuna udhaifu mkubwa sana. Katika watu walisababisha awamu iliyopita ikachukuwa sana huyu anashika namba moja.
 
Mimi huwa sikubaliani na hii ya kumpa Mungu kazi ya kila kitu. Ukweli wa Makonda kushiriki kwenye uhalifu na ufisadi ni kitu kinachoweza kuchunguzwa kwa muda mfupi mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…