Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Someone help me please. Hiyo post ya insta kama imeandikwa na mwanafunzi wa kidato cha pili.Hii ni mbinu ya kutafuta huruma na kutaka kuwafanya watu wasahau madhambi yake hasa ufisadi aliofanya wa kupora mali za watu.
Sijui kwanini linacheleweshwa!Nashangaa huko Takukuru, hizi kesi zipo wazi ila wanachelewa kuzifungua, Matumizi mabaya ya Madaraka, Kujipatia Mali Kwa njia ya udanganyifu, Kumiliki Mali zaidi ya Kipato chako, Sasa wanasubiri nini!?
Pole sana Makonda.
Hii nchi watu washazoea kula vya kupiga. Sasa hivi watu wametulia wanakula tu milungula na wametulia tuli. Wanasiasa nao wanapata pesa nzuri toka huko serikalini ili kupunguza joto la ushindani. Siasa za Bongo haziendi bila unafiki.
Ila utafaulu huu mtihani.
Damu za wale alioua zinaanza kumuwehusha hana lolote huyoAliyekuwa RC wa Dar es salaam, Paul Makonda anasema kuna makundi matano yanamuwinda ili kumuua.
Ameandika hayo kupitua ukurasa wake wa Instagram na kusema Makundi hayo ni pamoja na Wauza Madawa ya kulevya, mashoga nk
Ameandika “
Nafahamu kuna mkakati unaoratibiwa na Makundi 5 kuangamiza maisha yangu.
1) WAUZA MADAWA YA KULEVYA
2)WANUFAIKA NA MADAWA YA KULEVYA
3) MASHOGA
4)WANAOKESHA USIKU KUCHA KUTAFUTA KULIPA KISASI KWA WASAIDIZI WA DR MAGUFULI.
5) WALIOWAHI KUWA SEHEMU YA ……. Nafahamu pia juu ya mbinu zinazoandaliwa ili kuniuwa kwa faida ya familia zao pamoja na kutengeneza mashaidi wa uongo ili mnipe kesi ya uhujumu uchumi.
Mambo mawili najiuliza
1)PAMOJA NA KAZI ZOTE NZURI NILIZOZIFANYA KWA CHAMA CHANGU,SERIKALI YANGU NA WANANCHI WA DAR HAYA NDIYO MALIPO YAKE?
2)Hakika ukiwa mtumishi mwaminifu unaetetea haki za wanyonge tena ukitokea kwenye familia masikini haya ndiyo malipo yake ?
MTU aliejemga hospital , aliejenga ofc cha CCM, Magari ya police 👮♀️, ofc za Walimu, vituo vya police, shule za secondary mpaka na msingi, kutibu wagonjwa mpaka Meli kuja Tanzania,kuhudumia Makundi mbali mbali mpaka kuiunganisha Serikali na Viongozi wa Dini. leo hii naonekana eti natakiwa kunyongwa.
Pamoja na kwamba lipo kundi kwenye mitandao linalolipwa ili kuwaanda watanzania pale watakapo nikamata ionekane ni sawa. Hakika ipo siku Walemavu, yatima, wajane na waliotamani watoto WAO wasife kwa MADAWA ya KULEVYA SAUTI ZAO ZITASIKIKA.
#Ukiona maji yametulia jua kina nikilefu.”
Kimeumana team born town vs team born bush.😂😂😂😂😂
Huyu mtu siyo wa kuachwa hata kidogo. Alitenda madhambi mengi mno. BTW mtu ukiambiwa Makonda aliyekuwa na mkoa anaouita wake tena akafikia hatua ya kukataza baadhi ya watu kuingia kwenye ''mkoa wake'' ndiye anayelia namna hii huwezi kuamini.Nadhani angekaa kimya japo nahisi inawezekana kuna jambo analiona linakuja kumletea madhara si muda ndiyo maana amewahi kutafuta public sympathy
Nimejiuliza sana mahoga wanaua kwa kutumia niniSasa shoga anawezaje kuua mtu atampiga na ndala au upande wa kanga?
Kikubwa PM aliishi maisha mabaya wakati akiwa kiongozi alisahau kesho huwenda ikawa si leo ndiyo maana vita imekuwa kubwa kwake kila aliyekwaruzana naye anamtaka, bora hata angetishiwa na wauza madawa tu ila si mashoga.
Ni bush star kiongozi...! 🤣
Mkuu hivi ulikuwa unadhani Makonda kichwani zimo kielimu? Hakuna kitu na kila mtu alikuwa anashangaa aliwezaje kuwa juu ya watu wengi namna ile. Ila sisi watanzania pia tuna udhaifu mkubwa sana. Katika watu walisababisha awamu iliyopita ikachukuwa sana huyu anashika namba moja.Someone help me please. Hiyo post ya insta kama imeandikwa na mwanafunzi wa kidato cha pili.
Eti kina nikilefu! Alipenya vipi hadi ukuu wa mkoa?!
Musiba jamani huyo ndo daaah aisee kweli Bora kupoteza irizi ila sio mganga kufa..Ali Hapi, Heri James, Msiba,
Mimi huwa sikubaliani na hii ya kumpa Mungu kazi ya kila kitu. Ukweli wa Makonda kushiriki kwenye uhalifu na ufisadi ni kitu kinachoweza kuchunguzwa kwa muda mfupi mno.Kuna tuhumu kama hizi:-
-Kujaribu kumdhuru lissu
-kumtegea sumu ruge
Ila watu ndivyo wanavyosema kwenye mitandao ya kijamiii.... Ila ukweli unaujua wewe na Mungu mwenyezi. Ila kama kweli unahusika na hayo basi huna uhalali wa kulalama ivooo subiri unyolewe. Ila kama hizo tuhuma hazikuhusu basi huna baya RELAX Mungu atakupigania maana una mazuriii mengi ila mazuri hayo hata kama yatakuwa mengi kiasi gani bado roho za watu zina thamani kubwaaa sanaaa
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app