mzeewaSHY
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 8,916
- 8,630
Duh 🙄 !Kwa namna fulani uko sawa. Ingawa kwa upande mwingine unaweza kuona kuwa wananchi wameshaona jinsi serikali ilivyoandaa majeshi yetu kutesa, kujeruhi na hata kuua wale wote wanaopinga yake. Matukio ya 2001 kwenye uchaguzi mkuu kule Pemba; mauaji ya Mwangosi, Akwilina, risasi za Lissu, n.k. Na mengi mengine dhidi ya wapinzani hasa CHADEMA. A really murderous-ready regime when it comes to combatting dissent.
Halafu ukijumlisha na propaganda za kuwanasibisha wakosoaji/wapinzani na wasaliti. Na pia kuwalinganisha wanasiasa wote kama wasaka madaraka, pesa na waroho; kwamba wote ovyo tu: CCM=upinzani (CHADEMA) - hivyo afadhali CCM mnayoijua (Kazı wewe unayofanya hapa.), Watanzania wanaingia mashaka makubwa na kukosa guts za kujitoa muhanga kupigania haki zao.
Uoga+mashaka sio kukubali status quo. Certainly, the brink point will soon be reached. Natarajia sitakuwepo. Tutaanza kushuhudia civil wars kama za Ethiopia, Sudan, Somalia. Sasa hivi CCM wana-enjoy kipindi cha bliss ya ubabe (dominance). Hawajali kufanya siasa za brinkmanship. Ila waajue kuwa vizazi vinabadilika. Hizo kauli za kuwasemea wananchi kuwa wanalikubali zimwi walijualo ipo siku zitafika mwisho na moto utawaka.
😱 Japo mimi sidhani kama nitakuwa hai wakati huo lakini ninaomba Mungu awaongoze watakao kuwepo Taifa lisifike huko !! 🙏🙏🙏