Paul Makonda ni kiongozi kijana jasiri/ energeticist

Paul Makonda ni kiongozi kijana jasiri/ energeticist

Kuzabwa vibao mzee warioba?, mkuu vyeo havitafutwi hivyo
Na hapo ndipo siri ya mafanikio ya Makonda ilipo lalia, amesingizwa, kumbe sii wengi ndio wanaojua ni yeye ndiye alimuokoa Warioba kwa kuzuia asishambuliwe na yeye ndiye akamsindikiza nje, nyota yake ikaanza kung'ara!.

Fuatilia hizi nyuzi hii usipobadili mawazo, nitaamini kuwa shetani hata humu jf yumo


P
 
Dogo ivi umeshamaliza shule? Maana Janeth Mbene(MP) alikutumia na kufanya u disco Udom......bado unawashangilia hawa wanasiasa? Maliza shule kwanza kama bado upo hapo Mzumbe mbeya,Siasa zipo tu,si unakumbuka ulivyokuwa umepigika hadi ukaenda kwa Tulia (naibu spika) kuomba support akulipie ada chuo?.
 
Wakati kuna kundi nchini linapinga kila jambo ambalo linaonyeshwa kufanywa na mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Makonda, leo ninajitokeza kumtetea na kuwaambia kuwa huyu ni kijana shujaa. Ifahamike ili mtu kuitwa shujaa lazima awe amefanya jambo ambalo linabeba kila nukta ya uzalenzo, weredi, ushupavu na kuondoa uoga. Makonda anafanya haya.

Ninatambua nguvu ya wapinga yote/DEFRAYERS, mlishaanza kupingana na andiko hili hata kabla hamjasoma. Kwa kuwa kupinga ni asili ninaimani wapo ambao mtaponywa kupitia makala hii fupi ya ujasiri wa Mh Makonda. Bahati mbaya ujasiri wa Makonda ndio uliosaidia kumpa maadui wengi. Nikukumbushe tu kuwa Mh Makonda kwenye utumishi wake hatazami kesho yake bali anaangalia kesho ya Tanzania. Kiongozi yeyote ambaye haangalii kesho yake bali kesho ya Taifa ni kiongozi shupavu na jasiri na kiongozi asiyeangalia kesho ya Taifa ni kiongozi bandia(PUPPET LEADER).

Yapo mambo Mh. Makonda anayafanya yalipaswa kufanywa na watu wengine, lakini kwa sababu ya hofu ya kesho yao hawafanyi. Wanaona bora kesho yao kuliko kesho ya Taifa. Nikupe mambo matatu tu ambayo leo ninataka nikushawishi kuwa RC Makonda ni energeticist.

KUPINGA MADAWA YA KULEVYA/INTOXICANTS: Ni RC Makonda aliyesimama hadharani kumsaidia Mh. Rais kupambana na biashara ya madawa ya kulevya. Pamoja na ugumu wa vita ambayo Mh. Makonda wakati anaiendea alijua ni ngumu na ina watu wengi wazito na ina mtandao mrefu, lakini aliamua kuiweka roho yake mkononi na kuamua kuwa mstari wa mbele kupambana nayo. Hatua ya Makonda kutangaza hadharani kupambana na mihadarati alikuwa analitangazia taifa na dunia kuwa yupo radhi kufa akiwa anawatetea watanzania ambao wanapukutika kwa matumizi ya madawa haya na Tanzania ikabaki salama. Huu ni ujasiri kwani mawaziri wengine wangeweza kuwa front lakini kwenye suala la vipao mbele ndilo linakuja kuwatofautisha watu. Wapo wanaoangalia nafsi zao na wapo wanaoangalia kesho ya taifa.

KUPINGA USHOGA HADHARANI: Itakumbukwa kuwa pamoja na upepo uliokuwa unavumishwa na mataifa makubwa duniani na kujaribu kuungwa na badhi ya Watanzania, Makonda aliitangazia dunia kuwa DSM ushoga/HOMOSEXUALISM hairuhusiwi na atakayekamatwa atawajibishwa. Haikuwa jambo rahisi kuyasema mambo kama haya wakati unajua mataifa yenye nguvu yanaridhia. RC Mkonda alijitoa kama sadaka kwa Taifa kupinga hadharani. Alijua matokeo ya kupinga lakini alisema taifa kwanza na makonda baadae. Huu ni uzalenzo wa hali ya juu/patriotism. Mh Makonda angeweza kukaa tu akamwachia Mh Rais ili kulinda kesho yake lakini alisema NO! Na hii bila shaka ndiyo iliyopelekea kupigwa bann/ marufuku kwenda USA

Jambo la tatu, jana kwenye mkutano wa kimataifawa uwekezaji sekta ya Madini Tanzania,makonda alikaririwa akisema vita ya uchumi ni ngumu. Alisema Afrika sasa inaweza ikawa inapambana na nzige/locusts kumbe kuna mtu amekaa maabara anawatengeneza ili waje waharibu mazao na Afrika kukumbwa na baa la njaa. Si rahisi kumuelewa Makonda kwa leo huenda kwa kuwa una bad attitudes kwake. Lakini ukweli Nzige wanaweza kuwa wameletwa. Hivi umewahi kujiuliza kwa nini mataifa makubwa husikii kelele za UKIMWI? Hivi unadhani CORONA ni ugonjwa ambao upo CHINA tu? Mambo mengine ni man made just for economic war.

Dunia inakoelekea sasa tunahitaji akina Makonda wengi watakao msaidia Rais Magufuli kumpunguzia majukumu. Makonda angeweza kutulia kimya akiendelea na mipango yake ya kesho, lakini yeye ameamua kuangalia kesho ya Tanzania na si kesho yake.

Jana baada ya hotuba ya Makonda nilikuwa ninabadilishana mawazo na moja ya kiongozi wakitaifa wa CHADEMA(simtaji). Aliniambia mimi ni mpinzani, na nimpinzani kweli kweli. Lakini yapo mambo yanafanywa na viongozi wa CCM ninakuwa very impressed. Akasema wapo watu wengi ninawahusudu wanapofanya mambo yao. Akaniambia nikwambie tu vijana wawili ambao leo hata media ikija nitasema hata kama wenzangu watanielewa vibaya basi siwezi kuwa mnafiki/hypocist kutokuonyesha hisia zangu kwa Makonda. Akasema Makonda anapaswa kuheshimiwa na kupongezwa. Akasema unaweza kuwa umefuga mbwa kumi, lakini wengine hata usiku kama kuna jambo la hatari hawabweki. Hao mbwa hawana msaada.

Mwisho niombe maneno haya yasimpe kiburi Makonda, bali yamuongeze nguvu na kumuimalisha. Atambue kuwa Mh Rais ana imani kubwa na wao na kazi kubwa waliyonayo ni kumsaidia Rais usiku na mchana bila kujali mapokeo. Wapo watakao elewa kesho. Kisayansi Umri wa Makonda ni umri wa ndoto nyingi za kesho. Lakini endelea kulisimamia Taifa na ndoto yako ni imara kama Taifa litaendelea kuwa imara.

Na Elius Ndabila

0768239284
Noted subiri teuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dogo ivi umeshamaliza shule? Maana Janeth Mbene(MP) alikutumia na kufanya u disco Udom......bado unawashangilia hawa wanasiasa? Maliza shule kwanza kama bado upo hapo Mzumbe mbeya,Siasa zipo tu,si unakumbuka ulivyokuwa umepigika hadi ukaenda kwa Tulia (naibu spika) kuomba support akulipie ada chuo?.
MUDA huu si wa darasani? Unafundisha saa ngapi?
 
Toka lini buku saba wakawa na akili au hekima, hata humu kwenye jukwaa ukiambiwa taja mmoja tu hutopata yeyote. Yani mwanaume mzima unakuja na habari za kumtetea bashite!!!
Hawa fisi wote wanalipwa na bashite,Angalia wameanzisha uzi wameshtuana wanacomment wenyewe,angalia comment ya kwanza hadi nne utagundua hawa fisi wametarget kwa kushtuana


Hahahaha buku saba wengi akili hawana

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye kipindi cha Konani, Warioba aliulizwa kama alishawahi kupigwa na Makonda, kama wanavyomzushia, Warioba alikana kuguswa.

Cha ajabu Makonda akiomba form ya urais kwenye hivyo vyama vinavyompinga atapita bila kupingwa.
Nitamkubali kama ataanika orodha ya watu wasiojulikana ambao ni tishio kwa maisha ya wenzao.
> Aliwezaje kuwataja wauza na watumiaji wa madawa ya kulevya akiwemo mwenyekiti wa CHADEMA, na
> Wanaume waliotelekeza watoto akiwemo Lowasa.
Hawatakiwi viongozi waongo, wanafiki, wenye visasi, na wategemea matukio kama mitaji ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom